Mnaolalamika Saido Ntibazonkiza hana msaada angalieni gemu ilivyo ngumu huko Geita

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kuna mishabiki ndani ya Simba, wao kila siku Saido akipangwa wanalalamika kuwa Saido mbinafsi, Saido mchoyo, anaikaba timu, cjui mganga wake kiboko, maneno mengi.

Leo Saido kawekwa benchi na gemu had half time ni suluhu.

Simba itashinda Saido akiingia uwanjani, huyu mwamba ni majini tu aliyotupiwa na utopolo lkn ana mchango mkubwa sana pale unyamani.
 
Tofautisha washangiliaji na mashabiki.
 
Timu yenu Iko vizuri kulingana na machaguo yenu katika sajili mlizo Fanya, Mnakosea Sana pale mnapotaka kujifananisha na Yanga.
Mkifanya hivyo hamtaona Jema kwa wachezaji wenu.
Jikubalini, mnachokiona uwanjani ndio juhudi za timu yenu yaani uongozi, kocha na wachezji wenu.
 
Timu nzima iko hovyo.kutupa lawama kwa mchezaji mmojo mmoja sio sawa.tena wakati mwingine bora ata huyo ntibanzokiza anaonekana anapambana kwa juhudi kutafuta matokeo kuliko wengine wanacheza kifadha mradi dakika ziende.Mashabiki wa bongo niwakuzoea tu kwasababu hawanaga hoja zaidi yakufuata mkumbo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliye kuja kulainisha mechi ya leo ni Luis Miqison acha kututisha na kizee chako kinacho anguka hovyo hovyo.
Anaanguka mwenyewe au anachezewa faulo?.Na ni mara ngapi faulo anazochezewa zimeinufaisha timu.hebu jadili kama mwanamichezo badala ya ushabiki maandazi.Huuo mikson mwenyewe kuna ambao wanamuona mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeutofauti aina ya uchezaji na pressing ilivyokuwa angekuwa yy wasingepata vile
 
Kabla haujaanza kuwatukana watu, tambua kuwa Ntibazonkiza ukiacha suala la majini, issue yake kubwa inayoleta ukakasi ni kwenye maeneo matatu.

Kwanza, hajajua madhaifu yake yanayotokana na maumbile yake. Yeye ana umbile fupi na kwa hiyo miguu nayo ni mifupi, mipira mingi anayopoteza ni ile anayojaribu kuitanguliza mbele akimbie na mpira lakini kwa kuwa touch zake zimekuwa mbovu na zinakuwa na nguvu anashindwa kwenda na kasi ya ule mpira alioupiga anajikuta mara nyingi anagombea mpira 50/50 na mabeki wakati mwanzo alikuwa nao yeye. Matokeo yake ndiyo hayo kuanguka au kupoteza mipira.

Pili, angekuwa zaidi mchezeshaji wa timu badala ya kujaribu kufunga. Mipira yake mingi kuanzia ya kwenye move au dead balls inawababua wapinzani kwa sababu analazimisha kufunga badala ya kutafuta wenzake walipo.

Tatu, upigaji wake wa faulo na kona pia ni tatizo. Hizi zote anazikimbilia kwa sababu anajijua mfupi anaona hataweza kugombea mipira hii akikaa golini lakini niambie mara ya mwisho hizi faulo na kona zake ni lini zimezaa goli. Kwa timu zinazojielewa, set pieces zinatakiwa kutoa nafasi kubwa ya magoli lakini haijawa hivyo kwa Simba.

Ambapo ameisaidia Simba ni kwenye penati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…