Mnaonaje hela ya kuzoa takataka ikatwe juu kwa juu kama ile ya kodi ya nyumba katika luku?

Mnaonaje hela ya kuzoa takataka ikatwe juu kwa juu kama ile ya kodi ya nyumba katika luku?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Sijui niseme halmshauri zetu zimeshindwa hili suala la uzoaji takataka kwani miji mingi naona ni michafu sana na pia wananchi wenyewe wabishi kutoa hela za taka wajumbe wa halmshauri ya kijiji wanalalamikia hili.

So me naona japo ni suala dogo ambalo hata private sector inaweza kuifanya ikipewa tender ila naona hela Kwa watu wa mjini ikatwe tu juu Kwa juu aidha kwenye vocha au luku au hela ya maji kiasi kidogo hata 1000.

Kwa mwezi ikikatwa inatosha kabisa kuajiri watu na Shirika likafanya vizuri.
 
Sijui niseme halmshauri zetu zimeshindwa hili suala la uzoaji takataka kwani miji mingi naona ni michafu sana na pia wananchi wenyewe wabishi kutoa hela za taka wajumbe wa halmshauri ya kijiji wanalalamikia hili. So me naona japo ni suala dogo ambalo hata private sector inaweza kuifanya ikipewa tender ila naona hela Kwa watu wa mjini ikatwe tu juu Kwa juu aidha kwenye vocha au luku au hela ya maji kiasi kidogo hata 1000 Kwa mwezi ikikatwa inatosha kabisa kuajiri watu na Shirika likafanya vizuri..
kwanini isipangiwe bajeti kama zinavyopangiwa zingine toka kwenye pato la nchi? kama tupo serious kua wasafi.
 
Tukitumia akili hii inaweza kuwa chanzo cha mapato kizuri na ajira, sasa hivi ukitupa chuma dakika kumi nyingi hukikuti kimeshaenda kupimwa chuma chakavu, ukitupa chupa ya maji dakika kumi ishabebwa.

Kinachopaswa kufanyika ni kuweka mfumo wa vituo vya kuzoa taka, ukipeleka kiroba cha taka unalipa shs mia kwa kilo, nae mwenye kituo likija gari analipa elfu tano kwa tani moja, na huyu wa gari akipeleka dampo atalipa elfu moja kwa tani moja, mwenye dampo atatengeneza mbolea atauza, atatoa plastic atauza, atatoa chuma aluminium atauza, hapa hautaona hata ganda la ndizi mtaani
 
Shida hawa jamaa wana operate kibahiri sana. Hizi tenda za kutoa takataka hazitakiwi kukaa serikalini maana upuuzi wa watendaji wa serikali unajulikana.

Kuna muda wanaweka matakata muda mrefu hadi yanaanza kunuka sababu ya kurundikwa sehemu moja na kunyeshewa na mvua na kupigwa na jua.

Sasa sijui wanakuwa na mpango gani kuyaacha yajae. Siku wakija kuzoa utaona mtaa mzima umejaa mafurushi yanayonuka vibaya sana. Huwa nawaonea huruma sana wale wazoa taka kubeba zile taka sababu sio ubinadamu kuwaweka watu na takataka namna ile hata kama ni kazi waliyochagua.

Gari nzuri za kuzoa takataka zipo kwann wanatumia migari mibovu ambayo ni hatari kupita maeneo fulani fulani?

Mimi huwezi nambia kuwa hii kazi ni lazima ifanywe na halimashauri wakati tunajua kabisa kuwa halimashauri uzembe ni sehemu ya shughuli yao.

Ndio maana kuna raia hawapendi kulipia maana wanaona kama wanapoteza pesa zao, ukiwa haupo serious na shughuli yako hata raia hawatakuwa serious kukulipa sababu kuna muda unawasumbua kuwapa huduma so watadharau kukulipa kwa wakati. Sio tu takataka hata ulinzi.
 
Tukitumia akili hii inaweza kuwa chanzo cha mapato kizuri na ajira, sasa hivi ukitupa chuma dakika kumi nyingi hukikuti kimeshaenda kupimwa chuma chakavu, ukitupa chupa ya maji dakika kumi ishabebwa.

Kinachopaswa kufanyika ni kuweka mfumo wa vituo vya kuzoa taka, ukipeleka kiroba cha taka unalipa shs mia kwa kilo, nae mwenye kituo likija gari analipa elfu tano kwa tani moja, na huyu wa gari akipeleka dampo atalipa elfu moja kwa tani moja, mwenye dampo atatengeneza mbolea atauza, atatoa plastic atauza, atatoa chuma aluminium atauza, hapa hautaona hata ganda la ndizi mtaani
Hii inabidi ifanyike sambamba na ku arrange takataka kwa categories. Mfano chupa zikae eneo lake, plastics eneo lake,makaratasi eneo lake,vitu vya kufanana materials vinawekwa pamoja,takataka za kuoza mfano maganda ya mbogamboga, matunda,mabaki ya vyakula hivyo vinakaa sehemu yake. Halafu marufuku kuweka maji kwenye hizo vyombo ili kupunguza risk ya kuleta uozo.

Then zikitoka hapo zinakwenda eneo husika. Watanzania wanaipenda sana inchi yao na wanapenda maendeleo ila kuna washenzi wachache wanaojaribu kila uchao kuwakwamisha sababu katika mikwamo wanayoweka ndipo wao wanapata pesa na hongo za kujipatia maisha.

Hawa washenzi wachache siku zao zinahesabika na kwasasa nikitazama naona kila mtanzania akili zinaanza kufanya kazi sawa sawa kwa maana ya kwamba watu wanaanza kuamka na kuwa stable kiakili.
 
Back
Top Bottom