ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
kwanini isipangiwe bajeti kama zinavyopangiwa zingine toka kwenye pato la nchi? kama tupo serious kua wasafi.Sijui niseme halmshauri zetu zimeshindwa hili suala la uzoaji takataka kwani miji mingi naona ni michafu sana na pia wananchi wenyewe wabishi kutoa hela za taka wajumbe wa halmshauri ya kijiji wanalalamikia hili. So me naona japo ni suala dogo ambalo hata private sector inaweza kuifanya ikipewa tender ila naona hela Kwa watu wa mjini ikatwe tu juu Kwa juu aidha kwenye vocha au luku au hela ya maji kiasi kidogo hata 1000 Kwa mwezi ikikatwa inatosha kabisa kuajiri watu na Shirika likafanya vizuri..
Hii inabidi ifanyike sambamba na ku arrange takataka kwa categories. Mfano chupa zikae eneo lake, plastics eneo lake,makaratasi eneo lake,vitu vya kufanana materials vinawekwa pamoja,takataka za kuoza mfano maganda ya mbogamboga, matunda,mabaki ya vyakula hivyo vinakaa sehemu yake. Halafu marufuku kuweka maji kwenye hizo vyombo ili kupunguza risk ya kuleta uozo.Tukitumia akili hii inaweza kuwa chanzo cha mapato kizuri na ajira, sasa hivi ukitupa chuma dakika kumi nyingi hukikuti kimeshaenda kupimwa chuma chakavu, ukitupa chupa ya maji dakika kumi ishabebwa.
Kinachopaswa kufanyika ni kuweka mfumo wa vituo vya kuzoa taka, ukipeleka kiroba cha taka unalipa shs mia kwa kilo, nae mwenye kituo likija gari analipa elfu tano kwa tani moja, na huyu wa gari akipeleka dampo atalipa elfu moja kwa tani moja, mwenye dampo atatengeneza mbolea atauza, atatoa plastic atauza, atatoa chuma aluminium atauza, hapa hautaona hata ganda la ndizi mtaani