Mnaongeza sifuri kwenye ujenzi!

Mnyiramba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
1,141
Reaction score
3,119
Nyie mnaongeza sifuri kwenye ujenzi mnatutoa sana kwenye reli hata pesa tunaishia kuhonga badala ya kujenga!

Kuja fundi alinitumia hii picha ya nyumba hapo chini na kuniambia hadi hapo ilipofikia imekula milioni 80,yaani nilitamani hata kumtia makofi!

Tuacheni tabia ya kuongeza sifuri kwenye ujenzi ili uonekane umejenga kwa milioni 200 kumbe umeongeza sifuri kwa mbele!


Kweli hadi hapo ilipofikia ni milioni 80???[emoji276]
 
Milioni 80 ni nyingi kwa kuandika lakini kwa mahesabu ya ujenzi (ghorofa) basi hapo ni size yake.

Hapo kuna jamvi la ground floor na jamvi la first floor, ring beams na columns (hesabu saruji na vyuma hapo)

Hujaweka cement na mazagazaga kwenye foundation.

Window grills tayari, halafu bado unapiga kelele ya 80?
 
Akae anajua pia gorofa halina udogo!

kwenye ujenzi mil 80 tena wa gorofa siyo hela ya kukaa mtu unalialia.

Ndiyo maana watu hawajengi gorofa hovyo, siyo kwamba hawataki, ila bajeti inabana.

Mfano ukiwa na mil 50 unaweza kujenga nyumba ya kawaida na ukahamia (ila haijakamilika finishing zote).
Tukija kwenye gorofa mil 50 ni kama hela ya siment na nondo peke yake.
 
Mkuu ujenzi wa mtajo wa mojakwamoja wa pesa huwezi na itakusumbua
Ukitaka kujenga
We anza hatua ndogo kwa kubwa
Kamwe usijipimie kwenye ujenzi
Bali jenga kwa budget uliyonayo mkononi
 

Kwahiyo nyie hapo mnaona ghorofa!
 
Hata kama, hapo labda robo ya hiyo 80
 
Hilo ni ghorofa mkuu inategemea una simu gani kiongozi [emoji276]ni kama vile mpira ukitazama kwenye Tv inchi 14 ni tofauti kabisa na ukitazama inchi 60,huyu wa inchi 14 atalalamika wachezaji ni wadogo sana

Sipo hapa kubishana, upo sahihi.
 
Usisahau pia huo ujenzi unatumia
Nondo (16mm sq),
Blocks (6inch) afu zinalazwa sio kusimama,
Zege inakodiwa mashine,

NB; Hapo kila fundi anafanya kazi yake sio nyumba zetu fundi ujenzi anasuka nondo, anagonga mbao, and so on.

Ungemuomba mchanganuo ungeelewa vzr imefikaje iyo 80
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…