Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Biashara maana yake muuzaji anafurahi kuuza bidhaa yake huku akiweka kibindoni faida yake, while mteja akifurahia bidhaa ya thamani halisi.
Kama mbele ya safari mteja akigundua kuwa ameuziwa bidhaa bandia au isiyo thamani halisi ya pesa yake hali hiyo tutaiita utapeli. Na huo utapeli ndio hufanyika makanisani.
Mimi ni mkristo. Mlokole na nina misimamo yangu thabiti ila UKWELI ni kwamba haya makanisa ya kilokole mengi yanaendeshwa kitapeli. Sio ya kilokole tu hata haya makanisa mengine yamejaa mifumo ya kitapeli.
Muumini usipoitumia akili yako vizuri kulitazama neno la Mungu utatapeliwa huku ukifurahi.
2007 wakati nakwenda shule nje ya mkoa wetu nilisindikizwa na braza. Wakati nisharipoti shule na yeye anarudi aliuziwa madini na wahuni kwa sh.300k na simu yake ya gharama akawapa.
Alirudi nyumbani kwa furaha, aliishi kwa furaha kwa miezi kadhaa akijua ashaaga umaskini. Braza huwa ana vichenji na hana haraka, aliposema sasa ngoja nikachukue mamilioni kwa kuuza dhahabu sijui almasi zangu ndipo akakutana na mauzauza.
Kwakuwa alishatangaza kuwa ashatoboa maisha kwa majirani zake akaona hana la kuwaambia akaenda bank kuvunja kibubu akajenga nyumba yake ili aonekane kweli kapata mamilioni ya madini lakini mwisho wa siku UKWELI ulikuwa wazi kuwa alitapeliwa.
Utapeli wa kiimani mbaya sana kuliko utapeli mwingine wowote.