Yote uliyosema ni majibu sahihiUnaweza kueleza sababu za kutokuwepo kwa uthibitisho wa uchawi?
Je ni kwa sababu tu wanaoamini uchawi hawajathibitisha? Au walijaribu kuthibitisha ila hawakuweza au uchawi hauwezi kuthibitishika kisayansi?
Mbona unatoa mifano ambayo sio sahihi, tunakubaliana kwamba anayetoa madai au kutuhumu ndio anayepaswa kutoa ushahidi hivyo mtu akidai mie ndio muuwaji atapaswa kuthibitisha hilo kinyume na hivyo basi hakuna ushahidi wa mimi kuwa ndio muuwaji hivyo naweza nikawa kweli muuwaji au sio muuwaji ila hakuna ushahidi wa hilo.Kukosekana uthibitisho ndio ushahidi wa kutokuwepo, kama hakuna uthibitisho wa kitu kuwepo ina maana hicho kitu hakipo. Vinginevyo itakuwa dunia ya wendawazimu kama vitu ambavyo havipo vinahesabika kuwepo au kutokuwepo, yani mtu anaweza kuamka tu kesho akasema wewe ndiye uliyemuua jirani yako na akataka ufungwe kwa sababu huna ushahidi kwamba hukumuua jirani yako.
Ni uhakika gani tena hapo mkuu unaoutaka kutoka kwangu zaidi ya wewe sasa kueleza nilichoona na kuamini sio sahihi na ukaeleza usahihi wake ni upi?Umetolea mfano wa hirizi zilizokutwa kwa panya road na ukasema zilizuia wasife na zilivyotolewa wakafa na hayo ndio mambo unasema kwa kinywa chako kuwa ni uchawi
Swali una uhakika hirizi ndio zilizuia kifo kwa hao panya road? Au ni iman yako tu potofu?
Kuona uone wewe nieleze Mimi?Ni uhakika gani tena hapo mkuu unaoutaka kutoka kwangu zaidi ya wewe sasa kueleza nilichoona na kuamini sio sahihi na ukaeleza usahihi wake ni upi?
Hata superman anaweza kuelezewa yupoje ila hiyo ndio itafanya superman yupo kweli?Uchawi haupo kama upo thibitisha upoje ili tumalize mjadala
Mifano yako haiendani na uhalisia sasa Superman anaingiaje hapo? Acha kuhamisha madaHata superman anaweza kuelezewa yupoje ila hiyo ndio itafanya superman yupo kweli?
Unajua hadi sasa sijaona ukitoa hoja yenye kueleza kwanini unasema hakuna uchawi zaidi ya kupinga uchawi na kudai uthibitisho.
Hata kwako wewe uchawi si ni kama maigizo sio real, kwahiyo hata ukielezewa huo uchawi ukoje ni sawa tu na kumuelezea superman yukoje.Mifano yako haiendani na uhalisia sasa Superman anaingiaje hapo? Acha kuhamisha mada
Uchawi ni Iman sio kitu real tena mnaamini nyie msio na utashi wa kufikiri huwezi kulinganisha na movie za Superman ambazo ni maigizo
Elezea hiyo Imani yako potofu na uthibitishe huo uchawi upoje mimi Sina Imani hizo wataka nithibitishe kitu gani sasa
Nikuulize swali labda utaelewaHata kwako wewe uchawi si ni kama maelezo sio real, kwahiyo hata ukielezewa huo uchawi ukoje ni sawa tu na kumuelezea superman yukoje.
Wewe huwezi kuelezea kwanini unapinga hakuna uchawi unaishia tu kusema ni imani potofu, yani kupinga kwako uchawi ni kama imani uliyokuzwa nayo tu toka utotoni ndio maana hakuna unachoweza kuelezea kwanini unasema hakuna uchawi ili nasi tuone kuwa kumbe tunachoamini kuwa ni uchawi sio kweli bali ni imani potofu tu.
Ndio naamini upepo upo.Nikuulize swali labda utaelewa
Hivi unaamini kuwa upepo upo? Jibu ndio au hapana
Thibitisha kwanini unasema upepo upoNdio naamini upepo upo.
Kwanini uchawi hauwezi kuthibitishika kisayansi?Yote uliyosema ni majibu sahihi
Nithibitishe kwanini nasema upepo upo ndio nini? Sijakuelewa unataka nieleze kwa nini nasema upepo upo au nithibitishe kuwepo kwa upepo?Thibitisha kwanini unasema upepo upo
Yes! Thibitisha kuwepo kwa upepo unaoamini kuwa upoNithibitishe kwanini nasema upepo upo ndio nini? Sijakuelewa unataka nieleze kwa nini nasema upepo upo au nithibitishe kuwepo kwa upepo?
Ndiyo, naweza kukubaliana na wewe na hili kuwaondoa police kabisa katika hizo tuhuma nitataka tume huru ya uchunguzi. Pia kwa sababu police ndio wana wajibu wa kulinda raia na wanasema sio wao wanaoteka watu, wameshindwa kuwatambua watekaji na wameshindwa kuzuia utekeji uliokithiri kwenye utawala wenye uwajibikaji itabidi viongozi wake wajiuzulu pamoja kukubali tuwatafutie usaidizi kutoka vyombo vya nje nje vyenye weledi zaidi mfano FBI.Tukisema kwamba kutokuwepo kwa ushahidi ndio ushahidi wa kutokuwepo, hivi mie nikisema kwamba polisi hapa Tz hawahusiki na matukio ya utekaji yanayoendelea nchini na ushahidi wa hilo ni kutokuwepo kwa ushahidi wa polisi kufanya hayo matukio. Je utakubaliana na mimi?
Utapoteza muda bure mkuu,HUU UZI SIO KWA AJILI YA KUBISHANA, NJOO TUKUTANE TUFANYE KAZI, KAMA UPO MBALI USILETE UBISHANI WA KIJINGA
Kwanini uchawi hauwezi kuthibitishika kisayansi?
Kwa sababu uchawi sio "objective reality"Kwanini uchawi hauwezi kuthibitishika kisayansi?
Mfano wa changamoto za kichawi ni zipi mkuuNaona mnabishania sana kwenye Hili suala.
Uchawi upo.
Pengine hauelewi maana ya Uchawi na ukaishia kujua kwamba uchawi ni kuroga tu.
Sayansi haithibitishi kila jambo.
Mfano. Je mwanadamu ana roho?.
Kama hujawahi kukumbwa na changamoto za kichawi basi mshukuru Mungu.
Na kama Hauamini.
Nataman sana ukumbane Nazo na zikudhuru. Ili ujue kuwa uchawi upo.
Na useme tawile.