Mnaosema hamuamini uchawi, njooni niwathibitishie

Yoda

Hebu msaidie huyu mwenzako kumueleza uthibitisho ni nini maana yeye anang'ang'ania kuwa kaweza kuthibitisha upepo hapa na si kwamba kaeleza njia za kuthibitisha upepo.
Acha kumtagi mtu usilazimishe mawazo yangu yawiyane na Yoda au yako yawiane na mtu mwingine jibu kama wewe

Sema kuthibitisha ni kufanyaje?
 
Wajinga hawawezi kuisha duniani,
Kuna watu wanaamini dunia ni tambarare(flat earthers) ila haindoi ukweli wa dunia kuwa duara, mambo yote duniani yanaendeshwa kwa mantiki ya dunia kuwa duara.
Kuna watu wanaamini hakuna UKIMWI duniani, wengine wamewahi kuwa hadi marais.
Kuna watu wanaamini lizard/reptilians people ndio wanaendesha dunia na huwezi kuwaaminsha hakuna kitu kama watu mijusi
Sijui hoja yako ni ipi hapa!
 

Man Created God.
Its true in some people perspectives.

But It is better to believe and find that there is No GOD than NOT to believe and find out there is GOD.
 
Huwezi kuwa na uthibitisho wa uchawi kwa sababu wewe hukubali chochote kitakachoitwa uchawi, mbona hili ni simple sana tu halisumbui akili.

Turudi kwenye mfano wa polisi, hayo yote uliyoeleza ni tuhuma tu ila hakuna ushahidi. Huo mfano wa polisi sijautoa kwa bahati mbaya mkuu, wote tunaelewa kwamba polisi wanahusika katika utekaji ila hakuna ushahidi na wewe unasema kutokuwepo kwa ushahidi ni ushahidi.
 
Kwahiyo unanifundisha namna ya kufanya kazi? Wewe tumia aina ya uchawi huo ambao unauelezea wangu unafanya kazi tofauti.
Huna lolote, ungekua mchawi ungekua umeshafanya jambo kupitia maandishi tu, eti nipe kucha na nywele zako na jina la mama ako ili iweje wewe si mchawi umeshindwa nn kujua jina la mama ake
 
Tuchukue hilo la ukimwi, ukimwi ni upungufu wa kinga mwili na nachojua watu hawapingi kuwepo ukimwi bali wanapinga uwepo wa virusi vyenye kusababisha ukimwi.
Na katika hao watu sio marais tu bali wapo wanasayansi na madaktari.

Wakati wewe unadai hakuna uchawi na hilo hukufanya kukataa matukio na mambo yote yenye kuhusishwa kuwa ni uchawi hata kama huwezi kuyaelezea hayo mambo nje ya kuhusishwa na uchawi, basi unakuwa sawa na wale wenye kupinga uwepo wa virusi vye kusababisha ukimwi hata kama watu walishuhudia janga la vifo vya watu vyenye kuhusishwa na ukimwi kabla ya Arv.
 
Kusema tu haiwezi kuwa uthibitisho wa jambo, inahitajika ushahidi kuthibitisha jambo.
Kuhusu tuhuma kwa police lazima kuwe na uchunguzi ili kuthibitisha wanahusika, tuhuma tu haziwezi kuwa uthibitisho, hata hivyo kwenye sayansi ya uchunguzi kuna kitu kinaitwa leads au viashiria ambapo uchunguzi lazima uanzie hapo( inaweza kuwa tuhuma, kitu, uzoefu n.k)
Ili kuthibitisha uchawi mtu anatakiwa aanzie wapi?? Yani mtu akisema amekuwa masikini kwa sababu amelogwa utaanzia wapi kuthibitisha kama kweli amekuwa masikini kwa sababu amelogwa? Mtu akisema alikuwa anaendesha gari akaona jini ndio maana akasababisha ajali unaanzia wapi kuthibitisha jini alikuwepo barabarani? Ukisema timu fulani imefungwa kwa sababu uliona mtu anaweka uchawi golini unaanzia wapi kuthibitisha uchawi ndio umesabibsha washindwe au washinde mechi na sio mambo mengine??
 
Man Created God.
Its true in some people perspectives.

But It is better to believe and find that there is No GOD than NOT to believe and find out there is GOD.
Heri kuamini Mungu yupo uende usimkute, kuliko kuamini hayupo afu umkute🥲
 
Huna lolote, ungekua mchawi ungekua umeshafanya jambo kupitia maandishi tu, eti nipe kucha na nywele zako na jina la mama ako ili iweje wewe si mchawi umeshindwa nn kujua jina la mama ake

Bro hajasema yeye ni mchawi.
Kasema ambaye haamini kwenye uchawi na anataka kuamini basi wakutane na apewe vitu ABC vya huyo mtu alaf asubirie wiki 2 aone majibu.

Mbona ni rahisi tu.

Yeye hawez jua nyuma ya mandishi yuko nani. Kwasababu sio Lengo.

Kuna kaburi la mganga maarufu Iringa. Umeme ukipita juu yake hauwaki.
Pia Tanroads waliojaribu kulihamisha walikufa.
Ikabidi ngozo za umeme ulikwepe na waliache pemben ya barabara hivyo hivyo na liko hadi leo.

Na hii nayo tuiteje? Kazanazo
 
Acha kumtagi mtu usilazimishe mawazo yangu yawiyane na Yoda au yako yawiane na mtu mwingine jibu kama wewe

Sema kuthibitisha ni kufanyaje?
Sio suala la mawazo binafsi hapa bali tunazungumzia uhalisia wa jambo lenyewe.

Sasa unaulizwa swali haujibu unamgeuzia swali aliyekuuliza.
 
Ukiniambia rais wa Cambodia ni Nape naweza kupinga bila hata kumjua rais wa Cambodia au kujua kama Combodia ina rais au mfalme, ukiniambia mlima Meru ndio mlima mrefu kuliko wote duniani naweza kupinga bila hata kuujua mlima mrefu duniani, ukiniambia magenge ya dawa za kulevya ya Mexico ndio yanaoteka na kupoteza raia bongo naweza kupinga bila hata kujua ni wakina nani wanateka na kupoteza watu.
 
Unataka tujadili chunguzi za kichawi zinavyofanyika?
 
Point???
 
Story za uchawi ni rahisi sana kuonyesha matobo yake,
Tuanze hapa uone hii story inavyo collapse,
Huyo mganga maarufu wa Iringa anaitwa nani?
Yuko kijiji/mtaa na wilaya gani huko Iringa ?
Majina ya wafanyakazi wa TANROADS waliokufa wakijaribu kuliahamisha kaburi yako wapi na walikuwa wangapi?
Hilo tukio ilikuwa mwaka gani?
 
Hebu upload hiyo taarifa kutoka kwa tanroad au Tanesco kuthibitisha hizo hearsay zako
 
Sio suala la mawazo binafsi hapa bali tunazungumzia uhalisia wa jambo lenyewe.

Sasa unaulizwa swali haujibu unamgeuzia swali aliyekuuliza.
Wewe na mimi nani anageuza swali na kutoka nje ya mada

Umeniuliza unafahamu kuthibitisha ni kufanyaje nikakuambia hebu niambie kwa uwelewa wako badala ya kueleza au kutoa ufafanuzi kwa wewe unaelewa nini kuhusu uthibitisho unamtga Yoda anahusikaje

NB bado hujatoa maana ya kuthibitisha kitu kuwepo ni kufanyaje naomba jibu
 
Hebu upload hiyo taarifa kutoka kwa tanroad au Tanesco kuthibitisha hizo hearsay zako

Google Kaburi la Martin Kiyeyeu.

Sio kwa ubaya ila Mm nataman sana ambao hawaamini Ushirikina wakumbane nao.

Yaan kama ikiwa ni kazin, nyumban au kwenye ukoo wenu.

Kwasababu weng wanaobisha ni wale ambao hawajakutana nao.

Maana tunaweza ongea hapa siku nzima na msisadifu kwasababu haijawatokea . Basi na iwatokee.

Maana ubishan huu ni kama ule wa kuamini kuwa Mungu yuko au hayuko.
Wanaoamin yuko ni kwa kuwa kuna miujiza Ming wamefanyiwa na wakaona ile ni kwa uweza wa Mungu.

Bas na wasioamini. Ipo siku mtakumbana na Uchawi na ushirikina ili ndio muamini.

Yangu ni haya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…