Mnaosema hamuamini uchawi, njooni niwathibitishie

Mababu zetu wale walioishi miaka 150 na 200 iliyopita walidhani mambo mengi ni uchawi.

Walidhani bunduki ni uchawi, walidhani uwezo wa wazungu kitabiri kupatwa kwa jua au mwezi ni uchawi, walidhani muziki kutoka katika kiboksi ni uchawi.

Lakini, mambo yote haya hayakuwa uchawi.

Yalikuwa ni mambo ya sayansi tu ambayo hawakuyaelewa.

Sasa, na wewe leo unaposema huu ni uchawi, unajuaje ni uchawi kweli na si kitu tu ambacho hujakielewa lakini si uchawi?
 
Ujinga tu na Imani potofu.

My good brother Kiranga ametoa fursa ya $5M hamna mtu aliyejitokeza means what hivyo vingine ndio tutaamini??

Kwanini mababu zetu walifanywa watu, vibaraka, wa wakoloni je uchawi wao uliwasaidia nini kama sio ujinga tu
Mkuu,

Sasa hivi kuna nyingine ya $50 million ya kumkamata Nicolas Maduro rais wa Venezuela.

Wachawi wako wapi?
 
Muoga balaa, nimemfuata pm nimemwambia siku ya kwenda kuchukua sampuli kanitukana balaa, halafu akija hapa anapiga kelele hakuna uchawi, wakati yeye mwenyewe anaogopa kulogwa
Ana stress za kukosa kazi masaa 24 utamkuta kule jukwaa la majobless kwanza Hana adabu nilimwambia HAITOKAA apate kazi sababu alimtukana matusi ya nguoni mshana ..
 
Kwahiyo nikifa nimekufa kwa ugonjwa au uchawi?
 
Mkuu,

Sasa hivi kuna nyibgine ya $50 million ya kumkamata Nicolas Maduro rais wa Venezuela.

Wachawi wako wapi?
Hapa huwezi ona mtu tukisema hivi vitu havipo exist watu wanaona tunakosea ila ukijaribu kutumia logic kwenye haya masuala wachawi wa mchongo kina comrade_kipepe na wenzake huwaoni.

Mtu atakae weza kesho kutwa tu tunamsoma Forbes apa
 
Kama uchawi ungekuwepo mngeanza kuwaroga CCM kwasababu kila mtu hawapendi lakini wanapeta.
Turogeeni Mchengerwa na Mwigulu kwa kuanzia then mmalizie na Mkenda.
 
Kama uchawi ungekuwepo mngeanza kuwaroga CCM kwasababu kila mtu hawapendi lakini wanapeta.
Turogeeni Mchengerwa na Mwigulu kwa kuanzia then mmalizie na Mkenda.
Shida ya watu wengi kufikiri uchawi ni issue ya kurogana tu.
 
Jibu swali uchawi na ugonjwa kipi kinaua?
Mimi nafikiri hata ugonjwa unaweza kuwa sababu tu ya kifo na si kwamba ugonjwa kama ugonjwa ndio unauwa, kwa sababu wapo wenye kupata magonjwa na wakapona hawakufa. Sasa uchawi nao unaweza kusababisha ugonjwa ambayo ugonjwa huo ukawa sababu ya kifo.
 
Kama uchawi upo mloge sa100 alale mbele nchi ipumue ukifanikiwa hilo uje hapa jamvini tukuanzishie changizo kabambe kwa kuliokoa Taifa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…