Tajiri wa matajiri
Senior Member
- Apr 17, 2024
- 166
- 649
Barua Ya
Kabla ya yote Jasusi anawaomba radhi kwa ubashiri wake kwamba Kamala Harris angeshinda urais wa Marekani kwenda fyongo. Waungwana wakikosea huomba msamaha badala ya kukimbilia kutoa visingizio, au kuhalalisha makosa yao.
Jasusi anawashukuru mamia - pengine maelfu - mliomsihi afanya ubashiri huo kwa sababu moja kuu: imani yenu kwake. Na japo hakuwa na uhakika mkubwa kutokana na sababu mbalimbali, alilazimika kutimiza matakwa yenu.
Hata hivyo, japo huu si utetezi, intelijensia sio sawa na sayansi timilifu (intelligence is not an exact science). Wakati kwenye sayansi 2 jumlisha 2 mara zote huwa 4, kwenye intelijensia jawabu linaweza kuwa 10, au kwa kukatisha tamaa zaidi, jawabu linaweza kuwa 0.
Waafrika na ushindi wa Trump
Jana ilikuwa ni siku ya shangwe na vigelegele sehemu nyingi barani Afrika kutokana na ushindi wa Trump. Na hata kabla ya ushindi huo, ukweli kwamba Kamala Harris ana u-Weusi flani haukumsaidia kuwafanya Weusi wenzie barani Afrika wamuunge mkono.
Kuna sababu kadhaa za kwanini Trump anapendwa sana barani Afrika lakini moja ya msingi ni kwamba Waafrika wengi wanapenda ubabe. Ndio maana udikteta unastawi vema barani Afrika.
Kwa ambao mlikuwa hamjazaliwa zama za dikteta Iddi Amin wa Uganda, alikuwa na mashabiki wengi kutokana na ubabe wake, licha ya ubabe huo kupelekea vifo maelfu kwa maelfu.
Na japo Amin alivamia Tanzania mwaka 1978, kuna vijana wengi tu wasiojihangaisha kuelewa historia, wanaomuona Amin kuwa ni shujaa licha ya ukweli kwamba laiti angefanikiwa dhamira yake ya kuiteka Tanzania, vijana hao pengine wasingezaliwa kwa maana kwamba huenda wazazi wao wangekuwa wahanga wa unyama wa Amin.
Kuna dikteka mwingine Kanali Muamar Gaddafi. Huyo anaendelea kuonekana shujaa wa bara la Afrika akisifiwa kwa “mema yake lukuki”. Lakini kinachosikitisha kwenye mahaba haya kwa Gaddafi ni ukweli kwamba vijana wengi tu wa Kitanzania wanamhusudu mno dikteta huyo licha ya ukweli kwamba ndiye aliyemfadhili Amin kuvamia Tanzania.
Mahaba ya Waafrika wengi kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, na viongozi wengine “wababe” yanapigia mstari ukweli mchungu kwamba Waafrika wanapenda siasa za kibabe.
Na katika hili, ndio maana hata “Shujaa Mwendazake” John Magufuli alipata mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania licha ya ukweli usiopingika kuwa kiongozi huyo alikuwa dikteta wa mchana kweupe.
Kamala angekuwa rafiki bora wa Afrika kuliko Trump
Tatizo la mahaba ni kwamba hayachagui huyu mwema kwako au mbaya kwako. Ni kama vile mwenza aliyemo kwenye uhusiano wa kinyanyasaji. Hujibidiisha sio tu kuangalia “mazuri” ya mnyanyasaji hata kama ni ya kufikirika bali pia huenda mbali zaidi na kuhalalisha kuwa anastahili manyanyaso anayopewa.
Ukipata wasaa, fanya ku-Google kitu kinachoitwa “Stockholm Syndrome”, utaelewa zaidi anachokieleza Jasusi.
Ni kwa muktadha huo, ndio maana licha ya Trump kuzitukana nchi za Kiafrika, na kutoficha hisia zake kwamba Bara hilo sio kipaumbele chake, bado haijawazuwia Waafrika wengi kumsujudia mwanasiasa huyo.
Wakati msimamo wa Trump kuhusu Afrika upo wazi, Kamala sio tu alizuru Afrika akiwa Makamu wa Rais wa Marekani bali pia alishaunda timu maalum ya watu 25 kwa ajili ya kuisapoti Afrika.
Kwa Tanzania, Balozi wa sasa wa Marekani, Michael Battle, amekuwa mdau mwema kwa wapenda haki nchini humo ambapo majuzi “alijilipua” kwa kujibu malalamiko ya Rais Samia Suluhu kwamba nchi za Magharibi zisiingilie masuala ya ndani ya Tanzania, kufuatia wito wa balozi mbalimbali za nchi za Magharibi kulaani mauaji ya kiongozi mwandamizi wa Chadema, Mzee Ali Kibao. Balozi Battle alisisitiza kuwa kama mdau wa kweli wa Tanzania, nchi yake haiwezi kufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu.
Sasa subiri aje balozi wa Tump. Kama mfanyabiashara, Rais huyo mpya wa Marekani anafahamika kwa kugawa vyeo vya washkaji zake, wahafidhina ambao wanajali zaidi maslahi yao binafsi ya kibiashara.
Miongoni mwa watu walioshangilia sana Kamala kushindwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni wafuasi wa vyama vya upinzani hususan Chadema. Na sababu yao kuu ni “uswahiba kati ya Kamala na Mama Samia.” Kwa mtazamo wao, Urais wa Kamala ungemnufaisha “mbaya wao” Mama Samia.
Lakini laiti busara kidogo tu zingetumika, wangebaini kuwa wakati Balozi Battle “anajilipua” kuhusu mauaji ya marehemu Mzee Kibao, alikuwa anatumikia serikali ya Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala.
Na haihitaji ufahamu mkubwa wa siasa za kimataifa kujua kwamba Kamala, na si Trump, ndiye angekuwa mdau mwema kwa Wapinzani, ikiwa ni pamoja na hao wa Chadema, kwa sababu ya imani yake katika utawala bora, haki za binadamu na mambo mengine mazuri.
Ofkoz, kama itakavyokuwa kwa Trump, Kamala pia angeendelea kuisapoti Israeli kuiteketeza Palestina, lakini angalau Kamala alieleza bayana dhamira yake ya kuona operesheni za Israeli huko Palestina zinafikia kikomo ilhali Trump alishaahidi kuwa akishinda urais, atamsapoti Netanyahu kuiangamiza Palestina.
Hitimisho:
Pamoja na kutoafikiana na wanaoshangilia ushindi wa Trump, Jasusi kama muumini wa haki ya kikatiba ya mtu kupenda/kuchukia anachoona kinastahili kupendwa/kuchukiwa, anaheshimu wanaoshangilia ushindi huo.
Endapo huko mbeleni watabaiani kuwa walijiingiza mkenge au la, muda ndio utaongea.
Lakini unaweza kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa kamwe Jasusi hawezi kumpongeza Trump, na laiti Jasusi angekuwa na uwezo, angefanya “udekiteta” kuhakikisha Trump hashindi nafasi hiy