Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kuna watu wameanza kuleta hoja yakumtuhumu Mhe. Bashungwa kwamba ametoa uraia kwa wachezaji wa Singida. Nikiangalia aliteuliwa lini na toka ateuliwe anafanya nini naamini bado hana sahihi yake kwenye uraia.
Ndio kwanza anajitambulisha kwa taasisi anazoongoza . Naamini kwa umakini alionao Bashungwa atapeleka hoja yakumwondolea Waziri mamlaka yakutoa uraia bila muhusika kuwa na vigezo. Sheria ya Uraia inampa waziri mamlaka yakumpa mgeni yoyote uraia wakati wowote bila kushauriana na mtu yoyote.
Soma, Pia: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni
Kesho kwa bahati mbaya akipenya RAIA wa kigeni akawa waziri wa mambo ya ndani anaweza kuwapa uraia ndugu zake na hakuna atakaye hoji. Sometimes hata akija waziri akapewa mlungula au akawa na demu mgeni anaweza akampa uraia wa Tanzania bila kuhojiwa.
Uraia siyo jambo la kukabidhi mtu mmoja ni jambo la kiusalama lazima pawepo na vizingiti vya check and balance.