Mimi pia nilikuwa nafikiri kama wewe lakini nikawa sitaki kumletea ubishi Yoda tu kwa sababu niliona kwa kiasi fulani hili ni suala la opinion na halihitaji kubishana. Nikataka kumshukuru Yoda kwa kunipa upande anaofikiri yeye tu.Hawezi! Hawezi!
Sielewi ni mkorogano gani umeandika hapa, yani Rais mstaafu ndio amuhakikishie Rais aliyepo madarakani usalama wake wakati na baada ya kustaafu?!Samia hana mizizi ndani ya chama kuweza kufanya hayo mabadiliko.
Ni rare case kupata kiongozi ambaye atazingatia kuacha legacy huku akihatarisha pensheni zake za kustaafu na hata maisha yake. Inahitaji huyo kiongozi awe na conviction ya jambo husika ambayo ni wazi huyu hana. Ni rahisi kumpelekesha mtu wa aina hiyo. Anaona bora amalize awamu yake aende zake. Kama kuna mabaya anayafanya along the way, wanajuaga jinsi ya kuwasafisha mbele ya safari.
Kwa mtazamo wangu, nafasi ya mwisho ya kupata hayo mabadiliko ni wakati wa Rais Mstaafu Mkapa huku Magufuli akiwa Rais. Kutokana na historia zao, Mkapa angeweza na nadhani alikuwa anaelekea kumshawishi Magufuli afanye baadhi ya mambo hata kama ni ya kuanzia tu, ila wote tunajua kilichotokea.
Yaani kiufupi kwa mfumo wetu wa kisiasa ulivyo, kupata mabadiliko kupitia maamuzi ya Rais mwenyewe ni upate Rais mstaafu ambaye bado ana nguvu ndani ya chama amuhakikishie Rais aliye madarakani usalama wake wakati na baada ya kustaafu, halafu amuongoze katika kufanya hayo mabadiliko.
Mfumo wa kidemokrasia wa Marekani nao umekuwa corrupted mno na ndiyo mapungufu aliyokuwa anasema Obama kuwa pamoja na mapungufu hayo ambayo wakati mwingine yanatoa upenyo kwa populist leaders kuingia ambao wanaweza kuvuruga mambo, bado ndiyo mfumo bora zaidi kuliko mfumo mbadala wowote tulionao duniani.Obama ni mzungumzaji/mjenga hoja mzuri; lakini bado haisaidii kitu. Angalia chama chake kilikofikia sasa!
Hapana. binafsi sishabikii "'amri za mtu mmoja'", bila ya ushiriki wa maauzi ya wengi katika swala lolote. Ni muhimu kabisa kulibainisha hili na kuonyesha tofauti iliyopo.
Ngoja nitumie mfano wa aina ya viongozi tuliokwisha shuhudia staili ya uongozi wao hapa kwetu.:
Tukianza na Mwalimu Nyerere, sikumbuki mfano wowote wa yeye kutoa "amri" ya yeye pekee juu ya swala zito la nchi bila ya kushikisha vikao vya chama kufanya maamuzi na hata kuliwahi kuwepo na ushirikishwaji wa vikao vya chini kabisa vijijini kabla ya utekelezaji wa maswala husika.
Mara nyingi nasita kutumia mfano wa Pombe Magufuli, lakini sina mfano wa karibu zaidi wa kuonyesha tofauti yake katika maamuzi ya "mtu mmoja" (amri ya mtu mmoja kama ulivyo sema). Na swala ninaloweza kuweka kama mfano ni wakati ule wa UVIKO.
Nilitaja mfano wa China; na hata Vietnam; ambako kuna vyama vya kikomunist vinavyo tawala nchi hizo. Hata huko hakuna maamuzi ya "amri ya mtu mmoja". Ni vikao vya chama vinavyo amua
Hapa kwetu sasa hivi, chini ya Samia. Wanaotuamria ni GENGE kupitia kwa Samia. Mifano ipo mingi sana.
Demokrasia ni nzuri; hasa inapohusu kuchagua viongozi kwa njia zilizo wazi na Haki, ili viongozi hao wakawawasilishie wananchi wao maoni na matakwa yao katika mhimili wa Bunge. Hapa kwetu sasa hivi ni aibu kubwa kusema tunalo Bunge.
Ngoja nimalize kwa kurudi kule kwenye mifano ya viongozi wetu hapa hapa Tanzania. Na ninarudi kwa mfano niliosema ni mbovu kiuhalisia; wa Pombe Magufuli.
Maamuzi ya mtu mmoja ambayo yanafanywa kwa nia thabiti kwa maslahi ya wananchi, na yakitekelezwa kwa amri thabiti; huleta tofauti kubwa sana. Lile bwawa la umeme kule Rufiji, wakati huu wala tusingekuwa tunaliwazia kabisa. Ule ujenzi wa reli ya SGR, sijui tungekuwa tumefikia wapi. Serikali ingekuwa bado imeganda Dar es Salaam; n.k., n.k..
Maana yangu hapa ni kwamba, katika hali yetu ya kimaendeleo tulipo sasa; kuna uwakati kuwepo na ulazima wa kuwa na kiongozi mwenye maamuzi magumu.
Ukiwatazama vizuri wenzetu; kama vile Korea Kusini, Taiwani. Singapore; hawa wote hawakufikishwa walipo kutokana na "demokrasia" zao kuwa bora. Walikuwa kwenye u-dikteta walipokuwa wakijijenga kuja kufikia walipo sasa.
Mwisho, mwisho...; tunachohitaji Tanzania ni viongozi wanaoghuswa kwa karibu sana na hali duni za wananchi wao na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kuibadilisha hali hiyo katika muda mfupi iwezekanavyo. Sasa sijui kama ni "demokrasia" ndiyo itatufanya tuwapate hawa au vipi; SIJUI!
Mbona Magufuli alifanya mambo mengi tu ambayo yalikuwa yanapingwa vikali na vigogo wa CCM wenye chama haswa?!Sawa labda hana mizizi na hazingatii. Lakini akiamua kuzingatia ataweza?
Yoda anasema ataweza kwa sababu rais na mwenyekiti wa chama ana nguvu kubwa sana Tanzania.
Wewe unasema hawezi?
Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa sana katika utawala wa Mwinyi. Mabadiliko aliyofanya Mwinyi yaliwezekana kwa sababu ya kinga na baraka za Nyerere.Sielewi ni mkorogano gani umeandika hapa, yani Rais mstaafu ndio amuhakikishie Rais aliyepo madarakani usalama wake wakati na baada ya kustaafu?!
Kuna mengi yatasemwa kuhusu hao marehemu kuhusu waliyozungumza nyuma ya pazia na makusudio yao ya mbeleni ila yote yanabaki kuwa speculations tu, jambo nina uhakika nalo ni kwamba jiwe sio tu kwamba hakuwa mpenda demokrasia bali hakuwa hata ana uelewa wa msingi kuhusu demokrasia na haki za binadamu, sasa sijui angeshawishiwa vipi kufanya mabadiliko katika mambo ya demokrasia ambayo hakuwa anayelewa au kuyapenda.
Moja ya puzzle ambayo sijaweza kuisolve mpaka leo ni kumjua mastermind aliyekuwa nyuma ya Magufuli. Mtu aliyekuwa anamuongoza maana alikuwa hakosei ingawa kwenye issue ya siasa za upinzani ndiyo naona alibugi ingawa naelewa kwa nini walienda mlengo huo walioamua kuchukua.Mbona Magufuli alifanya mambo mengi tu ambayo yalikuwa yanapingwa vikali na vigogo wa CCM wenye chama haswa?!
Kumteua Bashiru Ally outsider kuwa Katibu mkuu wa CCM lilikuwa jambo dogo?
Kwenye sakata la korosho si alisema alitaka kuondoa wabunge wote wa CCM Kusini?!
Mbona Musiba alikuwa anawaburuza vigogo wa CCM na hawakuweza kufanya kitu?
Mbona Manji alienda kulalamika hadi kwa JK akaambiwa atulie tu?!
Aliwezaje kung'oa mizizi ya kina Rostam, Manji, Nchimbi n.k ndani ya CCM na serikali akawa yeye ndio kila kitu?!
Na Magufuli kama angetaka angeweza kuleta katiba mpya, angeweza kuongeza mihula na hakuna mtu angemzuia, jambo mojawapo kubwa alilokuwa nalo ni maamuzi na uthubutu wa kufanya chochote, huyu wa sasa anaweza pia ila sidhani kama ana maamuzi na uthubutu.
Huyo Magufuli ndo jitu hatariMbona Magufuli alifanya mambo mengi tu ambayo yalikuwa yanapingwa vikali na vigogo wa CCM wenye chama haswa?!
Kumteua Bashiru Ally outsider kuwa Katibu mkuu wa CCM lilikuwa jambo dogo?
Kwenye sakata la korosho si alisema alitaka kuondoa wabunge wote wa CCM Kusini?!
Mbona Musiba alikuwa anawaburuza vigogo wa CCM na hawakuweza kufanya kitu?
Mbona Manji alienda kulalamika hadi kwa JK akaambiwa atulie tu?!
Aliwezaje kung'oa mizizi ya kina Rostam, Manji, Nchimbi n.k ndani ya CCM na serikali akawa yeye ndio kila kitu?!
Na Magufuli kama angetaka angeweza kuleta katiba mpya, angeweza kuongeza mihula na hakuna mtu angemzuia, jambo mojawapo kubwa alilokuwa nalo ni maamuzi na uthubutu wa kufanya chochote, huyu wa sasa anaweza pia ila sidhani kama ana maamuzi na uthubutu.
Kama kuna mtu alikuwa anamuongoza alikuwa anakosea ndio maana aliwasulubu wapinzani ambao hakuwa na madhara kwake au kumkwamisha na pia akaharibu bunge kabisa.Moja ya puzzle ambayo sijaweza kuisolve mpaka leo ni kumjua mastermind aliyekuwa nyuma ya Magufuli. Mtu aliyekuwa anamuongoza maana alikuwa hakosei.
Utawala wa Magufuli uliniambia kumbe hiyo mnayoita deep state ya Tanzania inajua shida iliyopo Tanzania na nini kinatakiwa kufanyika. Kwa nini hawafanyi maamuzi sahihi katika tawala zingine, hapo sina jibu! Labda wanaona siyo wajibu wao, au labda Magufuli pekee alikuwa na akili hiyo ya kuwaambia wamuongoze wakati wengine wanataka wajiongoze.
Kuna mambo mengi.
I am going to state some unpopular observations.
Please note, simtetei Samia. Samia ana mabaya mengi sana, kama aliyokuwa nayo Magufuli.
Naelezea tu kwa nini watu wanaona afadhali Magufuli kuliko Samia.
Ni kweli - wapk watanzania hawamkubaki Samia kwa sababu ya uanamke wake tu.Nimegundua Watanzania wana mfumodume sana.
Good analysis - hakuna kipya alichofanya Samia mabacho Magufuli hakuwahi kufany kwenye mambinya haki na demokrasiaWatu wengi wanamchukia zaidi Samia kwa mambo yaleyale aliyoyafanya Jiwe kwa sababu Samia ni mwanamke.
Mwamba alikuwa ni yule mwanaume conservative wa kisukuma - self imposing , mtata tu na hakubali kukosea mbele ya familia. Hapa umefany analysis nzuri sanaPia Samia hajui kuleta figisu kibongobongo kwa show za kibabe complicated kama Magufuli. Magufuli alikuwa anaweza kuwa kakosea yeye lakini akaku gaslight wewe mpaka ukajiona wewe ndiye umekosea. Unambana kumwambia habari za kikatiba, halafu yeye anakwambia mihimili yote iko sawa lakini mmoja umechimbiwa chini zaidi. Samia hawezi show hizo.
Sahihi kabisa; zile zote zilikuwa story fake na uhuni. Kimsingi wafanybishara walisuffer. Hata kwenye madini mama kafany major reforms (mfano ile sheria ya kila mwenye dhahabu lazima auze angalau 20% ya dhahabu yake Benki kuu - hii ni major reform sana kwenye monetary policy ya Nchi yetu ili kuhifadhi reserve kwa kutumia monetary gold. Bahati mbaya Samia hafanyi PR nzuri.Pia Magufuki alijua kuwauzia "watu wanyonge" story fake kwamba anawapigania. Kuanzia kwenye makinika na figisu za migodi mpaka kwenye kutunga sheria ya kulinda maliasili (to his credit, kwenye sheria kulikuwa na kitu cha msingi hapo).
Hata la baandari ilikuwa PR issue vs vit y TICTIS kampuni tanzu y hautchson ambao ndio walikuwa wnaarun bandari kwa over 20 years. Kimsingi Samia alibadili tu investor baada ya mkataba wa TICTIS kuisha.. hakuna jipya hapa na mchakato wake ulianza toka 2019 Chuma akiwepo. Kumbuka TICTIS ilikuwa ya karamagi na wenzake; ilikuwa vita ngumu na Samia hakutaka kuwachafua nadhani jambo ambalo JPM angewachafua sana kabla ya kuweka mwingine ili yeye asichafuke.Samia reversed that kwenye kuuza bandari. So at least on this one point kuna sababu ya msingi kabisa ya kuona Magufuli was better. But it is mainly a PR issue, not substance.
Sahihi kabisaPia, Uzanzibari.
Habari za Watanganyika kutawaliwa na Wazanzibari. Habari za Waarabu kuuziwa bandari, Wazanzibari kufanya kazi bara lakini Watanganyika kutofanya kazi Zanzibar, hazimsaidii Samia.
Muhimu andiko lako linaonesha namna mijadala ya JF ya zamani ilivyokuwa ya moto na yenye ushindani wa hoja.. kudos kwenu wazeePia kuna angle ya udini. Samia kuonekana anafungia makanisa haimsaidii kwa Wakristo wengi ambao hata hawajali sana siasa lakini ukiwaingilia kwenye dini wanakuja mbogo.
Pia, Samia kawa disappoint watu wengi. Alivyoanza kuruhusu mikutano ya siasa, watu wengi waliona Samia anakuja kubadilisha pale Jiwe alipoharibu. Alipokuja kujionesha kuwa ni walewale tu, hata 4Rs zake zikaonekana magumashi. Lissu kafungwa kisiasa na haachiwi, nitandao inafungwa mpaka JF tunaingia kwa VPN, watu wengine wakamchukia kuliko Jiwe kwa sababu walikuwa na matumaini naye makubwa sana. Mtu ukiwa na matumaini naye makubwa akaku let down unaweza kumchukia sana.
Na hii habari ya kuweka matumaini kwa mtu emotionally bila ya kuwa na nuance ni tabia inayojirudia sana kwa Watanzania wengi.
Walifanya hivyo kwa Mkapa, kwa Kikwete, kwa Magufuli na Samia. Wote hao wakawa disappoint.
Na sasa hivi Watanzania wanarudia habari hizohizo kwa Gwajima, kwa Polepole, kwa Kapteni Tesha. Kwa jeshi.
Watu tunaoangalia historia tunaona hii pattern ya kuweka matumaini kwa watu, kihisia tu, bila strategy, bila kuweka misingi ya kitaasisi, ya kuwapa nguvu watu kidemokrasia, ni hatari.
Watanzania wengi wanapenda sana shortcuts za kubadili mambo kwa haraka bila kufanya kazi kubwa ya kubadili jamii na kupata mageuzi ya kifikra ya kudumu na yenye msingi mzuri.
Ndiyo maana wengine tukionesha hizi contradictions na kusisitiza mageuzi ya kweli, ya kitaasisi, ya kijamii, yasiyotegea watu wachache au hata mtu mmoja, mara nyingi tunakuwa kama hatueleweki, tunaonekana tuko out of touch, tunaonekana watu wa diaspora tu wakimbizi.
Haya mambo ya msingi hatuwezi kukwepa kuyafanyia kazi.
Otherwise tutazunguka kqenye mashairi ya Linton Johnson Kwesi katika "Di Eagle an' Di Bear".
"Dictators get dethroned
Now clown are quickly found".
Ndiyo hiyo habari uliyosema ya kutoka kwa Mubarak mpaka Al-Sisi Misri.
Wrong!Hao Korea Kusini na Singapore tunaowasifia, maendeleo yao yamejengwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Marekani na majeshi yake. Tamaduni zao pia zimechangia siyo tu siasa au udikteta. Tusisahau hilo!
Kwenye hili ninakubaliana nawe; hasa kuhusu kuzalisha "unafiki". Kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu hii ya kiTanzania unafiki umekuwa mwingi sana katika kila jambo; na nitakueleza bila kupepesa macho kwamba hali hiyo mbali ya siasa husika, lakini imechagizwa zaidi na tamaduni za kinafiki zilizo kuwepo katika baadhi ya makabila yetu na tamaduni za kigeni, hasa maeneo ya pwani.Sina uhakika na hiyo mifumo ya Nyerere au China maana ina tabia ya kuzalisha viongozi na wananchi wanafki. Unaweza kudhani agenda zinaanzia ngazi za chini ila mazingira yanatengenezwa chini mnaleteta mpitishe maamuzi ambayo yameshaamuliwa juu
Simtetei kama alikuwa mtu mwema sana, ukweli ni kwamba alifanya haya yote maovu uliyoyataja lakini angalau yeye watu walikuwa wanaona mabarabara, madaraja, flyovers, SGRs, mastendi, kupungua uwindaji haramu wa ndovu, watoto wake hawakutajwa kwenye ufisadi, bandari na maliasili hazikuuzwa n.k Je ilikuwa gharama sahihi na ya lazima? Mimi kwa maoni yangu ni hapana, angeweza kufanya haya yote bila hayo maovu mengine aliyolalamikiwa nayo sana. Ukweli pia ni kwamba hakuwa na uelewa kuhusu mambo ya demokrasia na haki za binadamu, kwake haya ni mambo ambayo aliona kama yanapoteza muda tu na kelele, hakuwahi kusema au kujinadi hata hadharani kwamba angependelea kuona demokrasia, utawala wa sheria au UTU vinakuwepo na vinashamiri katika nchi.Huyo Magufuli ndo jitu hatari
Yaani huyo ndo wa kulaaniwa kabisa
Ndo alileta huu upuuzi wote wa kuharibu uchaguzi, mauaji, uhamasishaji wa kipuuzi na udikteta
Huyo Magufuli ndo hafai ametuharibia nchi yeyu
Kaka Magufuli ndo adui wetu na ndo alitufikisha hapaSimtetei kama alikuwa mtu mwema sana, ukweli ni kwamba alifanya haya yote maovu uliyoyataja lakini angalau yeye watu walikuwa wanaona mabarabara, madaraja, flyovers, SGRs, mastendi, kupungua uwindaji haramu wa ndovu, watoto wake hawakutajwa kwenye ufisadi n.k Je ilikuwa gharama sahihi na ya lazima? Mimi kwa maoni yangu ni hapana, angeweza kufanya haya yote bila hayo maovu mengine aliyolalamikiwa nayo sana. Ukweli pia ni kwamba hakuwa na uelewa kuhusu mambo ya demokrasia na haki za binadamu, kwake haya ni mambo ambayo aliona kama yanapoteza muda tu na kumpigia kelele, hakuwahi kusema au kujinadi hata hadharani kwamba angependelea kuona demokrasia, utawala wa sheria au UTU vinakuwepo na vinashamiri katika nchi.
Kiukweli hata mimi inanishangaza, na hata wakati mwingine kunisikitisha na kunifanya nione aibu kumtaja Magufuli katika maandishi yangu.Simtetei kama alikuwa mtu mwema sana, ukweli ni kwamba alifanya haya yote maovu uliyoyataja lakini angalau yeye watu walikuwa wanaona mabarabara, madaraja, flyovers, SGRs, mastendi, kupungua uwindaji haramu wa ndovu, watoto wake hawakutajwa kwenye ufisadi n.k Je ilikuwa gharama sahihi na ya lazima? Mimi kwa maoni yangu ni hapana, angeweza kufanya haya yote bila hayo maovu mengine aliyolalamikiwa nayo sana. Ukweli pia ni kwamba hakuwa na uelewa kuhusu mambo ya demokrasia na haki za binadamu, kwake haya ni mambo ambayo aliona kama yanapoteza muda tu na kumpigia kelele, hakuwahi kusema au kujinadi hata hadharani kwamba angependelea kuona demokrasia, utawala wa sheria au UTU vinakuwepo na vinashamiri katika nchi.
Lazima alikuwepo na ni swali nilikuwa najiuliza na kutaka kumjua toka alipokuwa anaongoza. Namfananisha mtu huyo na Karl Rove kipindi cha George W. Bush. Hata Trump ana mtu wa aina hiyo.Kama kuna mtu alikuwa anamuongoza alikuwa anakosea ndio maana aliwasulubu wapinzani ambao hakuwa na madhara kwake au kumkwamisha na pia akaharibu bunge kabisa.
This matter is argumentative with no clear metrics.Mbona Magufuli alifanya mambo mengi tu ambayo yalikuwa yanapingwa vikali na vigogo wa CCM wenye chama haswa?!
Kumteua Bashiru Ally outsider kuwa Katibu mkuu wa CCM lilikuwa jambo dogo?
Kwenye sakata la korosho si alisema alitaka kuondoa wabunge wote wa CCM Kusini?!
Mbona Musiba alikuwa anawaburuza vigogo wa CCM na hawakuweza kufanya kitu?
Mbona Manji alienda kulalamika hadi kwa JK akaambiwa atulie tu?!
Aliwezaje kung'oa mizizi ya kina Rostam, Manji, Nchimbi n.k ndani ya CCM na serikali akawa yeye ndio kila kitu?!
Na Magufuli kama angetaka angeweza kuleta katiba mpya, angeweza kuongeza mihula na hakuna mtu angemzuia, jambo mojawapo kubwa alilokuwa nalo ni maamuzi na uthubutu wa kufanya chochote, huyu wa sasa anaweza pia ila sidhani kama ana maamuzi na uthubutu.
kwani sasa raia asiye wa ccm una haki ipi ya kuongeaIla wewe raia hutokuwa na haki yeyote ya kuuliza chochote popote.
Mleta wewe ni mpumbav first class halafu hujijui kma ni mpumbav....Majeshi yote yatimize majukumu yao ya kulinda raia na mali zao pamoja na mipaka ya nchi bila kuingilia mivutano ya kisiasa.
Kuingilia mivutano ya kisiasa ni pamoja na hayo baadhi ya watu msiojitambua mnaotaka jeshi lichukue nchi.
Yule anayekiuka katiba na sheria za nchi ashughulikiwe na majeshi hayo kulingana na sheria zinavyosema bila kujalisha cheo wala chama chake.
It's one and the same kama ilivyo sasa asiye na mrengo wa CCM ambavyo hana haki ya kuongea asivyoikubali CCM, asivyoikubali serikali ya CCM na asivyomkubali Samia hadharani kwani ukijaribu unatekwa mchana kweupe huku watu wa CCM wakishangilia kuwa umejitakia mwenyewe.Ila wewe raia hutokuwa na haki yeyote ya kuuliza chochote popote.