GWAMAKA USWEGE
JF-Expert Member
- Feb 23, 2023
- 2,017
- 7,406
Siyo kila mapinduzi ni mazuri au yana nia njema kwa raia. Haiti, Zaire, Ghana (Nkrumah) kote huko walipata mapinduzi ambayo hayakuwa chanya na hayakutokana na matakwa ya wananchi.
They sound like you.Kwani mapandikizi huwa wanaongeaje?
Ila wanamtandao ndiyo wanaojitambua sio?Nilikaa mbali na mijadala ya kisiasa kwa muda ila nimelazimika kulisema hili. Huu uzi nilikusudia kuuleta kitambo sana ila nikawa napotezea au kuahirisha kuuleta.
Kuna watu kutokana na sababu wanazojua wao wamekuwa wanatoa kauli za kutaka JWTZ lichukue uongozi wa nchi. Kuna wakati hadi nahisi kuna wanaharakati ambao ni mapandikizi waliowekwa ili kuwalinda CCM na viongozi wake pale hali itakapokuwa ngumu sana kwao.
Nasema hili la jeshi linaweza kuwa pona ya CCM. Kama mnataka mrudi nyuma hatua 50 kwenye demokrasia basi mkubaliane na hilo.
Sehemu kama Sudan, harakati za demokrasia zilizikwa rasmi baada ya jeshi kuingilia kati. Misri ni hivyo hivyo. Maeneo mengi tu demokrasia ilirudi nyuma sana baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Mnapopambana kupata uchaguzi huru na wa haki, msitamani kamwe njia za mkato kama hizo za kutaka jeshi lichukue nchi.
Nilidhani uko smart. Hauwezi kuwa pandikizi halafu uongee lugha ya kuwapinga huko ulipopandikizwa. Inabidi uonekane unasapoti mambo wanayofanya ili uaminike zaidi na upande huo.They sound like you.
Enemies of progress and a negative force.
njia zipi hizo?Hiko unachotaka jeshi ikifanye, raia na taasisi za kiraia wanaweza kukifanya kwa ufanisi zaidi. Ukiruhusu jeshi liingie leo, nini kitalizuia kesho kuingia tena?
Mashinikizo ya kisiasa ndiyo njia pekee sahihi ya kuiondoa CCM. Ilibidi kuishinikiza hadi kuipeleka katika meza ya mazungumzo. Njia za mashinikizo zipo na mnazijua ila hamtaki kuzitumia kwa sababu ya woga, uvivu na kutegeana.