Mnaotaka na kulilia jeshi lichukue nchi hamjitambui

Pitia historia yangu. Sijawahi kamwe kuleta mada wala kutoa maoni ya kuisifia CCM, ndiyo nije kufanya leo?
 
CCM wanaweza kufanya udhalimu wao kwa sababu kumekosekana umoja miongoni mwetu. Sisi tunategeana, ni wavivu, wabinafsi, tumekosa ubunifu na hatuko tayari kwa umoja wetu kufanya yale yatupasayo kufanya. Wachache waliojitoa muhanga wameumia na wanaumia huku tunawaangalia.

Tunashindwa hata kutumia njia zetu za kiswahili za kuwasuta huku mitaani hawa wadhalimu? Bado tunasapoti wasanii na matimu ya mpira ambayo yamejipambanua wazi yanasapoti udhalimu. Kama hata hayo yanatushinda, tutaweza nini?
 
Mijitu inayoogopa change ni minyonyaji, ni mijitu iliyoshiba, ikisikia masikini wana mkutano inalia mama weee, mama wee.

Masikini haogopi change maana hana cha kupoteza. Sanasana atapoteza umasikini wake!
Kauli nzuri sana ya Nyerere!
 
Mkuu,

Hata kama jeshi lingekuwa si la CCM.

Wanaharakati wa demokrasia kutaka jeshi lichujue nchi ni contradiction.
 
Wewe ndiye hujitambui. Unataka watu walilie chombo kipi zaidi ya jeshi ? Wewe ukiona wananchi na wanajeshi wanachokifanya ni upuuzi, una matatizo.

Hatuwezi kukubali nchi yetu iwe mali ya watu wachache tuu kana kwamba sisi wengine Mungu alikosea kutuumba tuzaliwe hapa nchini kwetu Tanzania.

Wazalendo tutazidi kupambana, ukiona kuibia kodi za sisi wenzenu ndio kitu cha maana zaidi tulia, acha tuwaoneshe kwamba sisi sio wajinga kiasi hicho.

Umeandika upuuzi, ukikosa cha kuandika uwe unatuliza hiyo mikono yako.
 
Mkuu,

Hata kama jeshi lingekuwa si la CCM.

Wanaharakati wa demokrasia kutaka jeshi lichujue nchi ni contradiction.
Nimefuatilia kwa muda mijadala mitandaoni nikawa nakutana na hizo kauli za kutaka jeshi lichukue nchi ndiyo maana nilisema nilitaka kuleta mada hii kwa muda nilipoona hizo kauli zinakuwa nyingi.

Ni kweli ni contradiction ndiyo maana nikatumia maneno "hawajitambui" kwa sababu wanachokitaka na wanachokisema haviendani.

Sidhani kama ukimuuliza Lissu, atakwambia ni bora jeshi kuliko CCM, sidhani!
 
Mkuu,

Hata kama jeshi lingekuwa si la CCM.

Wanaharakati wa demokrasia kutaka jeshi lichujue nchi ni contradiction.
Njia ipi itawakomboa Watanzania sasa zaidi ya Jeshi kuchukua nchi na kuongoza transition period ya mabadiliko?

Ccm wame compromise kila kitu na hakuna hata Taasisi moja ya kuaminiwa. Tulipofika mbele hakuna mwanga na njia pekee ni Jeshi kuwatoa hawa Wapumbavu CCM na kusimamia mchakato wa Katiba Mpya pamoja na kujenga mifumo imara.
 
Nakuelewa sana.

Kuna Watanzania wengi hawapingi mambo kwa principle.

Wanapinga kuumizwa wao tu.

Hawapingi ubaguzi kwa principle kwamba wanapinga ubaguzi. Wanapinga ubaguzi wanapobaguliwa wao tu.

Wao wakipata nafasi ya kuwabagua wenzao kwa maslahi yao, wanawabagua tu bila kuona ubaya wa ubaguzi huo.

Mfano, leo hapa JF nimekutana na mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa CCM na watawala. Anamshabikia Kapteni Tesha. Nikamwambia mwanaharakati wa demokrasia kumshabikia Kapteni Tesha, mwanajeshi anayechochea mapinduzi ya kijeshi, anayemsifia na kumlilia Magufuli, ni contradiction.

Mwanaharakati huyo hakupenda nilivyomwambia, akaniambia wewe ni mkimbizi tu, huna moral authority ya kutupangia mambo ya nchi yetu.

Huyu mburula haelewi hata wakimbizi wana haki, haelewi kuwa ubaguzi anaonifanyia mimi anayeniita mkimbizi ndio huo huo anaoupinga CCM inapomfanyia yeye kwa kumuita mwanaharakati.

Kimsingi hapingi ubaguzi. Angepinga ubaguzi asingenibagua mimi.

Anapinga kubaguliwa yeye tu, lakini yeye kubagua wengine walio na mawazo tofauti naye anaona sawa.

Kuna Watanzania wengi wako hivyo.

Hawa watu wanaoshabikia jeshi kuchukua nchi, kimsingi si wanaharakati wa demokrasia, ni watu ambao hawapendi utawala uliopo na ukija utawala wanaoupenda hata ujiwa wa kijeshi watafurahi tu.
 
Hujaelewa hoja.

Sijasema kuna njia fulani ni nzuri.

Wala sijasema kwamba njia ya jeshi kuchukua nchi ni mbaya.

Nasema tu mtu kusema anadai demokrasia halafu hapo hapo anataka jeshi lipindue nchi ni contradiction.

Kwa sababu mapinduzi ya kijeshi si suala la kidemokrasia.
 
Mqoinduzi ya kijeshi ndo njia pekee iliyobaki kutupeleka kupata demokrasia ya kweli.

Ghana Luteni Jerry Rawlings alipindua Serikali na akaweka utawala wa kijeshi uliofanya reforms kubwa sana hadi saivi Ghana wana Katiba bora na chaguzi za haki kweli.
 
Hakuna kitakachotokea. Mfumo ni mkubwa na kila kitengo kinajitegemea. If anything, hii inaweza kuwa plan ya Usalama kuwapa the majority wanachotaka ili watulie. Mtoto akilia sana, anapewa uji analala akiwa ameridhika. Honestly, it's a good plan.
Embu fafanua kidogo. Wamewapa au wanawapa nini?
 

Mbona unakuwa mgumu kuelewa hoja hivi?

Hujaelewa hoja.

Sijasema kuna njia fulani ni nzuri.

Wala sijasema kwamba njia ya jeshi kuchukua nchi ni mbaya.

Nasema tu mtu kusema anadai demokrasia halafu hapo hapo anataka jeshi lipindue nchi ni contradiction.

Kwa sababu mapinduzi ya kijeshi si suala la kidemokrasia.

Yakishatokea huna njia ya kuya control useme utayapeleka yaende kama nchi fulani.
 
Mkuu unajisumbua tu, Wabongo ni wajinga sana. moja ya tatizo kubwa linaloitesa Africa ni serikali zilizoingiliwa na majeshi. Sudan wanatamani hata wangelibaki na yule mzee, ila ndo wapi tena
 
Kwani Kikwete si alitoka jeshini?
 
Utabili wa kipuuzi,kuna jema gani lipo kwa, uta wala wa ccm, watu wanakufa kwa umaskini, sawa Sudan jeshi limeshindwa, vipi kuhusu Misri, Burkina Faso, Mali nk?
 
Kwa hali tuliyofikia ni lazima tuwe na Mapinduzi ya kijeshi na Jeshi liongoze kwenye transition yq kutupatia Katiba Mpya na kuweka mifumo imara ili tuwe na Taifa bora lenye mifumi mizuri na maendeleo ya uhakika.
 
Kuna kitu kinaniambia, ukiacha hao wasiojitambua wanaolilia jeshi, kuna kundi lingine ambalo wanachomekea na kusambaza hilo wazo la jeshi kuchukua nchi kama njia ya mwisho ya kuokoa maslahi ya watawala badala ya kukabiliana na "democratic revolution" ambayo ndiyo inaweza kweli kufuta uovu wao bila kuangalia mtu usoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…