Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mwanangu yuko katika hatua za kuomba nafasi chuoni mwaka huu, lakini anapata usumbufu mkubwa kubadilisha majina kwenye cheti chake cha kuzaliwa ili yaendane na yale yaliyo kwenye vyeti vya shule. Hii ni hatua muhimu ili aweze kuendelea na mchakato wa kuomba chuo.
Vivyo hivyo, hata wakati wa kujiandikisha kwa Kitambulisho cha Taifa, anakumbana na kero kwa sababu jina la pili kwenye cheti chake cha kuzaliwa limeandikwa vibaya.
Ili kutatua tatizo hili, ameshauriwa kupata barua kutoka kwa mwanasheria, jambo ambalo ni kero kubwa na linaongeza gharama zisizo za lazima.
Mara nyingi, watu wanalazimika kupitia usumbufu mkubwa kubadilisha majina kwenye nyaraka kama TIN Number, NIDA, vyeti vya kuzaliwa na vya kifo, wakati mwingine hadi kufika mahakamani kuapa.
Soma Pia: Tatizo katika uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wanaoomba Mkopo na huduma za RITA kwa ujumla
Wahusika wa kutoa nyaraka hizo muwe makini ili tuepuke huu usumbufu na gharama