Wana Jamvi nahope mko poa.
Hivi hawa itel wanawachukuliaje wateja wao. Aisee nimeletewa itel mpya na mtu nimsetie aanze kuitumia, ile kila kitu tayari akaweka memory card a play music, ebana simu si haina music player. Yaan file la mp3 haiwezi kusoma inaweka alama ya ?. Nkajua labda kapigwa airudishe simu dukani. Tumeenda kufika karibu simu 4 model tofauti tukakuta hazina music player ni hadi udownload. Kwa karne hii ya teknolojia bado kuna mtu anatengeneza simu bila mp3 player?