Mnaotumia TTCL fiber mlifanyaje kuunganishiwa?

Mnaotumia TTCL fiber mlifanyaje kuunganishiwa?

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Wana Jamvi, Habarini.

Nimekuwa nikijitahidi sana mwaka huu kutafuta fiber ya TTCL ofisini kwangu. Hii ni jambo ambalo nimehangaika nalo sana. Nimefika ofisi zao na wamesema niombeni mtandaoni. Nilijibu kuwa tayari nina maombi 17 yangu mwenyewe, na hizi ni order numbers. Waliniambia andika jina lako, namba ya simu, order number, na unakoishi. Kisha, nilipohoji kuhusu hatua inayofuata, walijibu kuwa mafundi wao watakuja kunihudumia, na nisubiri nyumbani.

Toka Januari hadi sasa ni Desemba, lakini bado sijaweza kufanikiwa kupata huduma hii.

Wakuu, nyie mmepambanaje hadi mmepata? Mbona mimi miezi 12 inakwisha lakini bado ngoma nzito? Japo nina namba za watu wa TTCL zaidi ya 20, kila mmoja ananiambia ni subiri.

Eneo la kufungiwa ni Dar es Salaam, wilaya ya Kinondoni, sehemu ** Inbox**

Mod ujumbe mmeubadirisha sana haukupaswa kuwa huo.
Inatakiwa kuonekana kuwa nmeenda mara nyingi na marabzote naambiwa nijaze form na kwenye karatasi ya wenye tatizo ambapo katika hyo karatasi najaza jina, order number, nakoishi na namba ya simu.

Maelezo ya mod yanaonesha nimeenda mara 1 wakati original message nimeeleza kuwa mara zote napoenda ofisini kwao (yaani zaidi ya mara moja)

Mod mnaharibu thread inakuwa sio yangu niliyoandika bali ni yenu ila anayeonekana ameandika ni mimi.

Yaani mnaharibu content kisha mnasingizia kuwa content ni yangu. Hii si sawa
 
Kwanini usiwatafute Zuku tu kama wamefika maeneo yenu.TTCL ilishajifia tokea mwendazake aondoke.
 
Rushwa ,Rushwa ,Rushwa!!
Hta rushwa hawataki. Nmeshawafata hao mafundi 20 niwape buku buku za nusu mishahala bado wanagoma. Inaonekana kma wamekatazwa kuwaunga wateja fiber na mamlaka kutoka juu labda. BAadhi ya mafundi nliongea nao na walikuwa honest kuwa sisi hatuungi mtu yyte ni mpaka bosi aseme nendeni sehemu fulan mkamuunganishie fulan na mara nyingi bosi mwenyewe ndio anayekuwa kwenye gari anawachukua kuwapeleka site. Kinyume na hapo wao ni kukaa ofisini kusubiri tar30 waende nbc kuwithdraw bucks
 
Hawajafika huku
Pole sana subiria tu starlink sasa kama itaruhusiwa Tanzania mwakani...nna uzoefu na ttcl walinisumbua sana kwenye kuunganishiwa.Uzuri maeneo ya Mbezi Beach zuku ipo niliwapigia ndani ya masaa 24 nilipata huduma na bando lao la elfu70 tu kwa mwezi nateleza
 
Uko mkoa Gani nikusomeshe ramani
 
Pole sana subiria tu starlink sasa kama itaruhusiwa Tanzania mwakani...nna uzoefu na ttcl walinisumbua sana kwenye kuunganishiwa.Uzuri maeneo ya Mbezi Beach zuku ipo niliwapigia ndani ya masaa 24 nilipata huduma na bando lao la elfu70 tu kwa mwezi nateleza
Starlink sahau mtu wangu
 
mm nimeshafunga TTCL ofisin km huna connection km hutotoa rushwa kwa maofisa na mafundi sahau ni uhun mtupu utajaza formu adi ukome utapiga simu jibu lao pendwa vifaa hamna serikal yenyewe ipo io tu hawashughulishwi
 
Inboxed
 
wadau wengi wamenifuata inbox ngoja nijibu hapa kwa msaada wote

instalation TTCL sio free ni paid 100k

acha ujuaji nenda ofisi za wilay au kata mpe engineer 100k yke utapewa lift mpka site na siku io io unafungiwa fast
 
Dah! Embu ngojea nisubiri subiri, Tigo au Halotel wasipo expand mapema hadi eneo langu nitawaendea TTCL ofisini na hiyo laki yao
 
huku kwetu kinondoni tunabembelezwa aisee waliomba wote washaungwa na wanakupa na simu ya mezani unlimited call 10k kwa mwezi.niliwakatalia mimi natubia fiber ya netsolution 70k per monthly 20mbps
 
Kama Rostam Mungu ataendelea kumuweka hai hilo shirika litakufa na hiyo huduma hutopata. Nakushauri nenda Halotel na hutojuts
 
Mods wamekuwa wakifanya editing za ajabu sana wakati huu.

Mimi niliwahi kuwa na issue kama yako ila waliniambia wana shortage of materials ila kwa sasa wanayo.

Je umejaribu kuwatafuta tena hivi karibuni hasa mwezi huu december?
 
Back
Top Bottom