Baada ya internet kuwashwa , baadhi ya watu maarufu kama ndumi la kuwili Boniface mwabakusi raisi wa TLS, na wengine wengi wameanza kuibuka na hoja za maridhiano ya kitaifa?
Swali langu kwenu nyinyi vichwa nazi, hayo maridhiano yenu mnataka yafanyike baina ya nani na nani? Na kwa faida ya nani?
Hili suala la madai ya haki , mpaka hapa lilipofika lilibebwa na wananchi . Ni wananchi ndio wameipush serikali dhalimu ya CCM mpaka kwenye Kona ya ukuta. Ni wananchi ndio wametoa sadaka damu Yao kwa ajili ya kutetea uhuru wao wakuchagua mtu wanae mtaka, lakini pia kukomesha vitendo vya kijambazi kama utekaji na dhulma nyingine nyingi za mamlaka.
Sasa nyinyi mnaozungumzia hayo maridhiano kwa wakati huu mmetumwa na nani? Mnataka kutumia damu ya waTanganyika kama daraja lenu la kisiasa?
Hakuna takataka yeyote mwenye haki ya kuzungumzia masuala ya maridhiano nchi hii isipokuwa wananchi wa Tanganyika. Na kwa umoja wao waTanganyika wataamua ni nani wakuwasemea katika mambo yao muhimu dhidi ya madhalimu..Kama mlidhani vifo vya waTanganyika vitageuka fursa za kisiasa kwenu basi Hilo mlisahau ..!!