Mnataka kupunguza wachezaji wa kigeni wakati wanang'arisha ligi yetu, mna shida ya Afya ya Akili

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Nasikiliza redio moja nashangaa sana wachambuzi wa kuheshimika hawajui madhara ya wanayoongea. Eti wachezaji wa kigeni wapungue. Wapungue waende wapi? Bila wa kigeni leo hii ligi yetu isingekuwa na ubora.

Timu zetu zisingekuwa za ubora. Au mnataka uwanjani waende ndugu zenu.

Katafuteni dawa za mapenzi sio ligi yetu.
 
sanabia sijui wanaweka sumu gani
 
Najiuliza hili swali kama ni hapana ina maana wachezaji wetu wa ndani hawana vipaji? na viongozi wetu wa mpira kama Eng. Hersi na Mo wanabebwa tu na wachezaji wa kigeni?

Je bila wakina Chama, Ngoma, Diara, Che Malone, Ateba, Pacome, Camara, Aziz Ki, Debra Fernandez na wakina Dube ligi yetu ingetamba kimataifa?
 
Soka letu lina changamoto nyingi sana,
Bongo kuna vipaji vikubwa mnoo, pitia mitaani utaona, wengine wana hadhi ya kucheza mpaka ligi kuu lakink wapo mtaani, hapa mambo ya kujuana na 10% yanatuangusha.

Pili mpira unatakiwa ufundishwe kuanzia ngazi ya chini.. Tunavuka hii stage.

Jibu lako kama kina pacome wakikosekana, ligi yetu itakuwa ni kichekesho, labda tubadilike.
 
Hiv ushawahi ona ligi yeyote ya maana duniani inaendelea bila wachezaji wa kigeni?
 
Jiulize, EPL ikiwatimua foreigners wote pale wakabaki kina Saka, Walker nk, utapata mood ya kuangalia tena mechi zao?
 
Najiuliza hili swali kama ni hapana ina maana wachezaji wetu wa ndani hawana vipaji? na viongozi wetu wa mpira kama Eng. Hersi na Mo wanabebwa tu na wachezaji wa kigeni?

Je bila wakina Chama, Ngoma, Diara, Che Malone, Ateba, Pacome, Camara, Aziz Ki, Debra Fernandez na wakina Dube ligi yetu ingetamba kimataifa?
Kuwepo kwa hao wachezaji ndio kumefanya tusiwagundue wachezaji wazuri wa kitanzania na mbona zamani tulikuwa na wachezaji wazuri kushinda hao wa kigeni waliopo sasa.?
 
Hiyo zamani tulifanya nini kimataifa
 
Lazima tukubali kushikwa mkono ili tufikie mafanikio wakati huu tukipambana. Leo hata kama mchezaji mzawa itakuwa rahisi kupata timu nje kutokana na ubora tu wa ligi.
 
Hiyo zamani tulifanya nini kimataifa
Tuliyafanya hayo tuliofanya kipindi hicho na ambacho kiwango cha mpira kilikuwa cha juu sana ukilinganisha na leo ambapo kiwango kiko chini kabisa.

Kiwango cha mpira kimeshuka duniani kote na Afrika ndio kabisa kwani akili ya kila mchezaji inawaza zaidi pesa kuliko kucheza soka.

Enzi hizo kwa ubora wa wachezaji tuliokuwa nao hatukuhitaji kutoa wachezaji nje kuja kuchezea vilabu vyetu.
 
Hujajibu swali langu bado
 
Ukitaka kujua kwamba wachezaji wazawa hawana viwango itizame taifa stars
 
Nasikiliza redio moja nashangaa sana wachambuzi wa kuheshimika hawajui madhara ya wanayoongea. Eti wachezaji wa kigeni wapungue. Wapungue waende wapi? Bila wa kigeni leo hii ligi yetu isingekuwa na ubora.

Timu zetu zisingekuwa za ubora. Au mnataka uwanjani waende ndugu zenu.

Katafuteni dawa za mapenzi sio ligi yetu.
Siyo watangazaji wato upeo wao wa kuelewa uko juu naomba niishie hapo ili nisichafue hali ya hewa
 
Back
Top Bottom