Mnazipendea nini hidden roof house?

sizipendi hata kuziona,naonaga ni nyumba za kiarabu na jangwani. na ndio asili yake huko. huko jangwani kuna upepo, hawaweki roof wakiogopa upepo utaanua.
Pia hakuna mvua nyingi. Huko kwenye paa hata huwa wanaweka mikeka na kukaa. Ndiyo maana ya lile andiko la biblia linasema ni bora kuishi kwenye pembe ya paa kuliko kuishi na mwanamke mgomvi. Kuna watu kabisa walikuwa wanaishi kwenye hayo mapaa. Na kwenye zile wanaita sikukuu za vibanda Waisraeli walikuwa wanajenga vibanda juu ya paa. Sasa wabongo wameambiwa ni za kisasa wamezuzuka.
 
Huu ujenzi tuwaachie tu waarabu wasiokua na mvua ya maji,zaidi ya mvua ya vyumbi na upepo mkali.Nimekaa Abudhabi kwenye nyumba tofauti zenye ujenzi huu ila sijawahi ona zikivuja.Ebu mafundi mangungu waulizeni waarabu wanajengaje?
 
Hii taswira ya kusema contemporary inapunguza garama ndo inafanya nyumba hizi zijengwe kwa ubora mdogo hapa tanzania. Kiukweli hizi nyumba si za kupunguza garama kwani lazma ukubaliane na uhalisia kuwa ili iwe katka ubora mzur uwekeze kwny system za drainage ya maji na mifereji mizur ya maji iliyojengwa kwa zege imara na duct za kutosha kwahio huwezi kubana bana zege lisiwepo la kutosha.
Hizi nyumba kigarama hazitofautiani sana na nyumba ya kawaida tu kwahio km unaamua kujenga jenga kwa kupenda muonekano si kwa kusema utapunguza garama
 
Kwa uhakika zaidi bora nimpe kazi mchina kujenga hizo contemporary 🏠
Siri kubwa ya contemporary wanapofeli mafundi wengi ni kuetengeneza system ya maji iende sambamba na uwiano wa kiwango cha slope na kasi ya maji yanayokusanywa kwny paa. Hii inahitaji experience expertice wa hii kitu ukikurupuka tu ukamchukua fundi yoyote tu bila mtaalamu wa kukudesignia roof structure ya contemporary lazma ulie kilio cha simba aliyepigwa bao tano
 
Tunapotaka kujenga contemporary kwa kuona km tunabana matumiz kulko nymb za kawaida ndo shida ila swala la kujenga sehemu yenye mvua zitaleta shida nakataa si kweli hapa hapa tanzania kuna mikoa ya kasakzini zimejengwa na mvua zinapiga balaa lkn hakuna tatizo lakuvuja
 
Huu ujenzi tuwaachie tu waarabu wasiokua na mvua ya maji,zaidi ya mvua ya vyumbi na upepo mkali.Nimekaa Abudhabi kwenye nyumba tofauti zenye ujenzi huu ila sijawahi ona zikivuja.Ebu mafundi mangungu waulizeni waarabu wanajengaje?
Hawajawahi kushindwa kitu mafundi wetu
 
Mafundi wetu mtaani wengi ni wale hawashindwagi kitu hata kama hana ufaham nacho matokeo yake wanaharibu kazi.

Mwaka jana tulifumua tyles nyumba ya vyumba 7 sababu n hiyo hiyo fundi rangi kajifanya mjuaji anaweza kuweka tyles.
Ndo umemaliza kil kitu yeye anajua ni rahisi kujenga kama hizo nyingiene na hata siku moja huwa hawakubali kuwa hawawezi bali hungangania tu
 
Ujenzi unahitaji 'ufahamu' wa mambo, sio ukanjanja. Mafundi wengi hawana ufahamu wa mambo mengi sana, kwenye ujenzi unahitaji kupata ufahamu kabla ya kufanya lolote.
Mimi nimejengewe hizi nyumba wala haina shinda yoyote ,tatizo ninaloliona na mafundi hawajui lolote kuhusu hizi nyumba hasa hapo juu ,kwenye bati material za kupaua zipo nyimgi sana
 
Ujenzi unahitaji 'ufahamu' wa mambo, sio ukanjanja. Mafundi wengi hawana ufahamu wa mambo mengi sana, kwenye ujenzi unahitaji kupata ufahamu kabla ya kufanya lolote.
Umeongea kila kitu mimi ninafundi wangu na hajawahi kuniangusha amenijengea nyumba kama tatu hivyo hakujawahi kuwa na shida yoyte
 
Kuna mtu anaogelea akiwa ndani huku 🤣🤣

View: https://twitter.com/BarakaMaviatu/status/1722613511883567461?t=NYDeJG2StXqtU_fNLZDs7w&s=19
 
Naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…