NEC RUKWA SULTAN SEIF ANAVYOKWAMISHA MRADI MKUBWA WA TAZA
Mradi huu Mkubwa wa Umeme sasa upo kwenye mashaka kutekelezeka kwa sababu ya hila Chafu za Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif.
Tangu 2019 Tathmini ya Maeneo yote yanayopitiwa na Mradi huu ilishafanyika na kawaida Serikali huwa inazuia maeneo ambayo yashafanyiwa tathmini kuendelezwa. MNEC Huyu kwa ushawishi wake mwaka 2023 aliweza Kujipatia Hati ya Eneo lake lenye ukubwa wa Square Mita 3000 sawa na Robo tatu heka. na kuhesabika kama mmoja wa wanufaika wa mradi huu huku akilazimisha kulipwa Fidia zaidi ya Milioni 61 wakati wananchi wote wanaopitiwa na Mradi wamelipwa Milioni Tatu tu kwa Heka.
Endapo MNEC huyu atalipwa Milioni 61 kwa Heka anazotaka kulipwa wakati wananchi wengine wamelipwa Milioni 3 kwa heka hiyo ni haki? Kwa nini anatumia ushawishi wake na Cheo chake kuhamasisha wananchi kwenda mahakamani kuzuia Mradi kisa maslahi binafsi?
Ikumbukwe wananchi wanaopisha eneo la Mradi Wilayani Sumbawanga wote walilipwa Fidia ya Sh. Milioni Tatu kwa Hekali Moja kwa Maeneo ambayo yalikua hayaendelezwa.. kutokana na kutokuwa na Hati lakini MNEC huyu kwa ushawishi wake aliweza Kujipatia Hati ya eneo na kuitumia kukopa kiasi kikubwa Benki huku akitengeneza mazingira mradi uweze kumlipa fidia kubwa tofauti na wananchi wengine, baada ya hila hizi kutozaa matunda sasa anatumia ushawishi wake kuwahamasisha wananchi kugomea mradi huu mkubwa jambo ambalo limesababisha wakandarasi kusimamisha ujenzi kutokana na Vurugu zinazoendelea.
MRADI WA TAZA NI NINI?
Ni Mradi mkubwa wa usafirishaji umeme unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia (TAZA) pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagamenda, Kisada, Iganjo, Nkengamo na Malangalali ambao utaunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia ambao unafadhiliwa na wafadhili Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) ambao kwa pamoja wametoa zaidi ya shilingi trilioni moja za kutekeleza mradi huo ambao pia unahusisha ujenzi wa vituo vitano vya kupoza umeme.