Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Hemed Chale, ametoa msaada wa chakula kwa wahanga wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha tarehe 28 Desemba 2024 na tarehe 2 Januari 2025 wilayani Songea, mkoani Ruvuma.
Mvua hizo zilileta uharibifu mkubwa wa miundombinu, ambapo nyumba 155 ziliharibiwa. Msaada huo ulijumuisha mchele kilo 345, Maharage kilo 138, na mafuta ya kupikia, na umekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea ili kusaidia wahanga katika kipindi hiki cha maafa, ambapo wanajitahidi kurejesha hali ya kawaida na mazingira bora ya kuishi.
Pia, Soma: Waziri Dkt. Ndumbaro Awafariji Waathirika wa Mvua Songea
Akipokea msaada huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile, alimuhukuru kiongozi huyo kwa msaada alioutoa kwa jamii iliyokumbwa na maafa.
Vilevile, Ndile alitoa wito kwa Maafisa Tawala na Viongozi wa Serikali ya Mtaa kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa kwa usahihi na kwa wakati.