ebu leta hiyo tuone uwezo wako
Go ahead,uanze na kabila lako
Idea si mbaya sana.
Wasiwasi wangu ni kutoa taarifa bila kufanya utafiti kwanza. Vema ungetuambia umejiandaa vipi ili taarifa isiwe na upotoshaji.
Nasema hivi kwa sababu nimekuwa nikisikia vitu vya ajabu ajabu kuhusiana na makabila kadhaa ambayo mimi nikekaa visivyokuwa na ukweli wowote.
Siku moja nilikuta jamaa fulani akiwasimulia watu kuhusiana na mila za kabila langu kwa namna ambayo watu wote waliokuwapo pale waliamini, lakini kiukweli ulikuwa ni uongo mtupu. Nilipomtafuta baadaye kumuuliza kama yeye ni wa kabila lile, aliishia kusema tu kuwa alisimuliwa na jamaa yake aliyepata kukaa kule!
Sasa hiki ndicho sipendi kuona tunaletewa hapa JF. Kifupi, kama hujafanya utafiti ni bora ukakaa kimya tu. Lakini pia naona itakuwa ngumu kufanya utafiti ktk makabila zaidi ya 160, mi naona tu ungeachana na jambo hili, maana mwisho wa siku utatuletea uongo tu.
idadi ya kura za ndiyo imefika nne mpaka sasa, bado 11
yap, ntaanza na kabila langu wala usijali. wasiwasi wangu kwa hao wengine ambao hawatapenda kuona ukweli wa mila na desturi za makabila yao kuanikwa hadharani kama sehemu ya historia au uhalisia wa mambo ya kabila lao
usihofu mzee. haitakuwa rahisi kuandika historia ya makabila yote ya kitanzania. Hapa history department ya UDSM kuna research nyingi zimefanyika na taarifa zipo za kumwaga, sioni wasiwasi wako unatokana na nini. Kama ni mvivu wa kujisomea siku zote utakuwa mtu wa mashaka, lakini kama upstairs kuko updated huhitaji kuwa na hofu kama hii yako. Dunia hii bado inakua na taarifa zipo nyingi sana kwa anayejisomea
Mkuu hicho unachoita ukweli, hauwezi kuwa ukweli ni hadi ufanye utafiti. Na utafiti ni strategic plan, sio kukaa sebuleni Tandahimba halafu unaelezea ukweli kuhusu wajaluo wa Tarime. Wasiwasi wangu hapa ni kwamba wewe umekuja na wazo, tena zuri tu, lakini hujatuambia umejiandaa vipi ili kuhakikisha kuwa taarifa yako itakuwa haina hata chembe ya uongo.
Upi mpango-mkakati wako? Naamini unafahamu idadi ya makabila tuliyonayo. Naamini hapo ulipo unaweza kuyaorodhesha yote kama ukitakiwa kufanya hivyo (ambalo ni jambo zuri angalau linaweza kutuonyesha ufahamu wako juu ya makabila yote).
Vininevyo mkuu GT lazima atatilia mashaka uwezekano wa hiki unachotuahidi hapa.
So, una wasiwasi na upstairs kwangu?
Kweli wewe ni mtafiti mzuri, kama utafiti wako utakamilika kwa kila kitu hapo Hist. Dep UDSM, bravo.
Kimsingi sikatai wazo lako, il kama GT ninaona umuhimu wa kuhoji uwezekano kwa zoezi hili na usahihi wa outcomes zake.