Mnyakyusa wa Kwanza London(utani)

Mnyakyusa wa Kwanza London(utani)

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
Wadau hii nimehadithiwa juu ya jamaa wawili Mwakipesile na mwenziwe Mwakalobo.
Hawa walipelekwa na chama chao cha ushirika kusoma huko London miaka ya 50's.
Walipofika tu wakahifadhiwa katika hoteli moja ndefu sana ya ghorofa 25 na wao wakaka ghorofa ya 18.
Kwa vile hawakuuona mji wa London kwa vile walifika usiku asubuhi sana Mwakipesile akaamua kudamka na kuuona mji mapema.
Mwenziwe Mwakalobo alipoamka na asimwone Mwakipesile akawa na wasi wasi hivyo akaenda balcony, na chini kabisa akamwona Mwakipesile akifanya window shopping kwa kutazama bidhaa madirishani.
Kwa vile Mwakalobo yeye bado hakuwa ameoga na kunyoa(shave) asubuhi akatafuta wembe asiuone, hivyo katoka tena balcony na ikaw hivi
Mwakalobo akipiga kelele kwa sauti:MWAKIPESILE MBAPO ULWEMBE!!
(Mwakipesile nipe wembe)
Mwakipesile hakusikia na akaendelea na widow shopping, lakini polisi mmoja akaona tukio hilo na aielewe jamaa anasema nini kwa vile helewi kinyakyusa.

Mwakalobo akiendelea kupiga kele:"MALAFYALE MWAKIPESILE MBAPO ULWEMBE!"

Yule polisi akifikiri huyu jamaa nataka kujiua akaenda mbio mpaka ghorofa ya 18 , na alipomkuta Mwakalobo chumbani akamuuliza :"whats wrong sir"

Mwakalobo akamjibu:" Mwakipesile , there, shaving blade, no me"
Polisi akaenda balcony akatoa kiona mbali(binoculars) ambayo Mwakalobo alikuwa hajapata kuiona.
Baada ya kumfocus Mwakipesile, polisi yule akamwonyesha Mwakalobo kama ndiye anayemtafuta.
Mwakalobao alipomwona rafikiye yuko karibu saaana, hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" Mwakipesile mbapo ulwebe!!"
 
Duu,
Wanyakyusa kumbe WAZUSHI. Na ujanja wote huo wa kukaa UK kumbe hivi ndivyo mlivyoanza kuishi huko? Naona sasa kwa nini mkaamua kukimbia London na kwenda kuishi vijijini kwa soo mliloliacha Te teteteee!!!!! Wambeya njooni mjibu mapigo.
 
Hii imekaa vizuri mkuu!!
"hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" Mwakipesile mbapo ulwebe!!"
 
Gwakisa kama wanyaki wenzie ni mzushi; hamna msimamo nyie wanyaki ndio maana mnaishia kugombana wenyewe kwa wenyewe!!
 
what a nice one to start with my day....hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" Mwakipesile mbapo ulwebe!!"
 
what a nice one to start with my day....hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" Mwakipesile mbapo ulwebe!!"

Teh! Teh! Teh! Jamaa angeweza hata kumshika begani!!
 
wadau hii nimehadithiwa juu ya jamaa wawili mwakipesile na mwenziwe mwakalobo.
Hawa walipelekwa na chama chao cha ushirika kusoma huko london miaka ya 50's.
Walipofika tu wakahifadhiwa katika hoteli moja ndefu sana ya ghorofa 25 na wao wakaka ghorofa ya 18.
Kwa vile hawakuuona mji wa london kwa vile walifika usiku asubuhi sana mwakipesile akaamua kudamka na kuuona mji mapema.
Mwenziwe mwakalobo alipoamka na asimwone mwakipesile akawa na wasi wasi hivyo akaenda balcony, na chini kabisa akamwona mwakipesile akifanya window shopping kwa kutazama bidhaa madirishani.
Kwa vile mwakalobo yeye bado hakuwa ameoga na kunyoa(shave) asubuhi akatafuta wembe asiuone, hivyo katoka tena balcony na ikaw hivi
mwakalobo akipiga kelele kwa sauti:mwakipesile mbapo ulwembe!!
(mwakipesile nipe wembe)
mwakipesile hakusikia na akaendelea na widow shopping, lakini polisi mmoja akaona tukio hilo na aielewe jamaa anasema nini kwa vile helewi kinyakyusa.

Mwakalobo akiendelea kupiga kele:"malafyale mwakipesile mbapo ulwembe!"

yule polisi akifikiri huyu jamaa nataka kujiua akaenda mbio mpaka ghorofa ya 18 , na alipomkuta mwakalobo chumbani akamuuliza :"whats wrong sir"

mwakalobo akamjibu:" mwakipesile , there, shaving blade, no me"
polisi akaenda balcony akatoa kiona mbali(binoculars) ambayo mwakalobo alikuwa hajapata kuiona.
Baada ya kumfocus mwakipesile, polisi yule akamwonyesha mwakalobo kama ndiye anayemtafuta.
Mwakalobao alipomwona rafikiye yuko karibu saaana, hata sauti akapunguza kabisa kama anaongea kwa utaratibu sana na mtu aliyekaribu:" mwakipesile mbapo ulwebe!!"

hahahahaaa ... kupunguza sauti kwa sababu ya darubini, iyo kali sana
 
Sijui sasa ni yule Mwakipesile Mkuu wa Mkoa wa Mbeya au vipi!
 
ahaa hawa ndugu zangu bure kabisa..Maloli na mapijo..ila dada zao japo wabaya lakini wana stamina sana..!!!hasa wale wa tukuyu na kyela.
 
Hehehe hii imekaa vizuri ulikuti kiki Mwalyafyale teh teh teh
 
Mwee! twafwilile banyambalal,..heeee haaaaaaa,...
 
Back
Top Bottom