Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti, amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kesho kupiga kura kama walivyojiandikisha.
Pia, amehimiza wananchi kuhamasishana katika ngazi ya familia na mtaa ili kuhakikisha hakuna anayeacha kupiga kura, kwani ni haki ya kila Mtanzania kufanya hivyo.