SI KWELI Mnyika amesoma MEMKWA darasa la nne na kajenga ghorofa kwa kuuza geleni za wanafunzi

SI KWELI Mnyika amesoma MEMKWA darasa la nne na kajenga ghorofa kwa kuuza geleni za wanafunzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Nimekutana na hii video je, haya maneno ni kweli anayasema Mnyika


1729258325765.jpeg
 
Tunachokijua
John John Mnyika ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye mbali na nafasi ya ukatibu Mkuu wa CHADEMA pia amewahi kuwa mbunge wa Ubungo, mwaka 2010-2025.

images

Mnamo Oktoba 17 2024 John Mnyika alifanya Mkutano na waandishi wa habari akielezea kuhusu Mwenendo wa zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa Nchini Tanzania, uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Baada ya mkutano huo kumekuwa na video inayomuonesha Mnyika akiwa kwenye Mkutano huku sauti inayosikika inasema: "Sasa mimi nimesoma mpaka MEMKWA la nne baada ya kuwa Msumbufu sana darasani nilikuwa na ujasiliamali wa kulokota hivi vigeleni vya watu maana saa naona mbona ni hela hii ya wanafunzi wanakuja nayo halafu yanachotewa tu maji yanapigwa pigwa mateke mimi ni kuunganisha na kupeleka mpaka soko Kuu ni ujasiliamali na nimejenga mpaka gorofa cha matope"

Je, Ukweli ni upi?
JamiiCheck imebaini sauti inayosikika kwenye video inayomuonesha Mnyika akiwa kwenye Mkutano na waandishi wa Habari kuwa Si sauti ya Mnyika, sauti inayosikika ikisema Mnyika amesoma MEMKWA darasa la nne (Tazama video hiyo hapa) imehaririwa na kuwekwa kwenye video halisi( Tazama kuanzia dakika ya 31 na kuendelea) ambayo Mnyika alikuwa akiongea kuhusu Mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Nchini Tanzania, 27 Novemba 2024.

Aidha, Sauti na maneno yanayosikika kwenye video hiyo ya Mnyika ni Sauti na maneno ya Markuba Majanaba

Katika video iliyopotoshwa JamiiCheck tumebaini:
-Kupishana kwa mwenendo wa midomo na sauti inayosikika, hali inayothibitisha kuhaririwa kwa video na kuingizwa sauti mpya.

-Kasi kubwa ya video na kasi ya sauti inayosikika tofauti na video halisi kama zilizopo kwenye chaneli rasmi za vyombo vilivyorusha mkutano huo.

-Aidha, kwenye chaneli zilizorusha mkutano huo pamoja na kurasa za CHADEMA ipo video yenye maneno na lafudhi tofauti na inayosikika kwenye video iliyopotoshwa hali inayothibitisha hiyo siyo sauti ya Mnyika.

Bonyeza kutazama video hizo
Back
Top Bottom