Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
Mnyika atafutwa na polisi mkoani Mbeya
Na Felix Mwakyembe, Mbeya
VIONGOZI wawili waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walikamatwa na Jeshi la Polisi, mkoani Mbeya na baadaye kuachiwa kwa dhamana, huku Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, John Mnyika akiendelea kutafutwa.
Taarifa za uhakika zilizoifikia Mtanzania zinawataja viongozi waliokamatwa jana na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mbeya kuhojiwa kuwa ni Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbeya Vijijini, ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Mkoa huo, Ipyana Seme na Mhamasishaji kutoka Kurugenzi ya Taifa ya Chama hicho, Jomba Koy.
Mkurugenzi wa Vijana wa Chama hicho ngazi ya Taifa, John Mnyika, anaendelea kusakwa na jeshi hilo kwa ajili ya kuhojiwa na kisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zelothe Stephen, hakupatikana jana kuzungumzia sakata hilo, kutokana na siku hiyo kuwa ya mapumziko. Kukamatwa kwa viongozi hao kunaelezwa kumetokana na Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Juliana Malange, kuwatuhumu kuwa wanaendesha kampeni kinyume cha sheria.
Inadaiwa kuwa msimamo huo unapingana na maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame, aliyenukuliwa na vyombo vya habari akielekeza kuwa vyama visivyokuwa na wagombea katika jimbo hilo vinapaswa kuendelea na shughuli zao za kisiasa kama kawaida.
Kwa maelekezo hayo ya Jaji Makame, Chadema iliendelea na shughuli zake za kukiimarisha chama hicho mkoani Mbeya kama kawaida, hata baada ya mgombea wao, Sambwee Shitambala na yule wa DP kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho cha ubunge katika jimbo hilo ambapo vimebaki vyama vitatu tu.
Chanzo: Mtanzania