Mnyika: Kumejitokeza vitendo vinavyoashiria kuvunjwa kwa miongozo na baadhi ya wanachama (wa CHADEMA)

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Narudia kwa mkazo wakati natoa wito kwa wagombea, wanachama na mawakala wa wagombea kuzingatia katiba kanuni maadili na itifaki ya chama katika mchakato mzima wa uchaguzi.”

“Hata hivyo katika kipindi hiki cha uchukuaji na urudishaji fomu kumejitokeza vitendo ambavyo vinaashiria kuvunjwa kwa miongozo na baadhi ya wanachama mbalimbali kuna tuhuma za namna hiyo.”

“Iwapo kuna kiongozi au mwanachama au mgombea atakayeona yeyote anayekiuka miongozo hii aweze kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chama au mamlaka za ngazi zinazohusika na anayetuhumiwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka ili kudhibiti hii hali ya kuwepo kwa ukiukwaji wa miongozo na taratibu za kampeni na uchaguzi.” - Mnyika.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz, John Mnyika akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam, tarehe 7 Januari, 2025.
 
Chadema Kila MTU ni msemaji wa chama😳😳😳😳😳😳
 
Hapo inatafutwa namna ya kumsaidia mwamba kwa kumdhibiti lissu, ikumbukwe mwamba hana hoja za kung'ang'ania madaraka!.
 
Bila shaka anaongelea kuhusu rushwa za Mbowe
Anaongelea baadhi ya viongozi mfano wa Katavi na mwenyekiti wa BAWACHA taifa kutangaza kumuunga mkono Lisu hadharani kabla ya kura
 
Team mbowe wanaongoza kwa hili, matusi, kashfa na lugha za kejeli
 
Narudia kwa mkazo wakati natoa wito kwa wagombea, wanachama na mawakala wa wagombea kuzingatia katiba kanuni maadili na itifaki ya chama katika mchakato mzima wa uchaguzi.”

“Hata hivyo katika kipindi hiki cha uchukuaji na urudishaji fomu kumejitokeza vitendo ambavyo vinaashiria kuvunjwa kwa miongozo na baadhi ya wanachama mbalimbali kuna tuhuma za namna hiyo.”

“Iwapo kuna kiongozi au mwanachama au mgombea atakayeona yeyote anayekiuka miongozo hii aweze kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chama au mamlaka za ngazi zinazohusika na anayetuhumiwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka ili kudhibiti hii hali ya kuwepo kwa ukiukwaji wa miongozo na taratibu za kampeni na uchaguzi.” - Mnyika.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz, John Mnyika akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam, tarehe 7 Januari, 2025.
Hana jipya, ye mwenyewe anatuhumiwa kuchukua pesa za Abdul.
Hiki chama chetu kinapaswa kujisafisha, kuna uozo mwingi sana.
 
Back
Top Bottom