Mnyika: Msajili Jaji Mutungi ameitisha kikao cha Makundi mbalimbali kujadili Katiba Mpya 26/5/2023, Sisi CHADEMA hatutaenda Hatuna Imani naye!

Acheni kenge nyie hamna impact yoyote hata ofisi ya chama chenu imewashinda
Acha kwanza watu wenye akili.timamu wajadili hoja iliyoletwa. Mambo kama haya hayaletwi JF kwaajili ya watu kama ninyi. Ni kwaajili ya watu wenye akili timamu tu.
 
Mutungi ana mandate gani kwenye suala la katiba ya nchi? Ni sawa na Mkurugenzi wa ATCL aitishe kikao cha wamiliki wote wa vyombo vya usafiri.

Uwezekano mkubwa asiye na akili kichwani ni wewe. Tambua kuwa katiba ya nchi ni ya makundi yote. Mutungi atayaķutanisha makundi yote kwa mamlaka gani?
 
..Jaji Mutungi ajiuzulu nafasi hiyo kupisha wengine wanaoaminika na wadau wa siasa.
 
Kwani mnataka nini? Mbona hamueleweki? Au wamelogwa? Ney wa mitego aliimba
 
Hata Mungu alisema msipo muimbia mawe nayo yataimba..... Serikali Iendelee nao ambao wapo tayar isimubumbeleze mtu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI 💪
 
Mutungi ni mtungi hasa. Na alijidhihirisha kuwa ni mtungi kwelikweli kwenye mgogoro wa Lipumba na CUF.
Baada hiyo kazi ya kishetani aliyoifanyia CUF na hivi karibuni NCCR-Mageuzi sasa anapewa jukwaa la kutumia matunda ya kazi yake kuua vuguvugu la katiba mpya. Na wanasiasa wetu wasivyokuwa na maadili wala dhamira ya kujenga taifa la kidemokrasia, tusishangae mtaji wa hii kazi yake mpya aliyopewa muuaji wa vyama vya siasa ni pamoja na ACT ya Hayati Maalim Seif, mhanga mkuu wa ushetani wa hicho kinachoitwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa! Raia yeyote mwenye mapenzi mema na nchi hii hawezi kushiriki mchakato ambao tungu mwanzo ni dhahiri utashi wa kisiasa haupo. Utashi wa kisiasa ungekuwepo mashauriano na wadau yangefanyika kupata utaratibu mwafaka.
 
Hili jukumu wangeachiwa watanzania mashuhuri, wasomi na wanaokubalika k.m. Mzee Warioba; Paul Kimiti; Jenerali Ulimwengu Jaji Samata n.k.
 
..Huenda hicho kikao ni mbinu nyingine ya kuchelewesha mchakato wa Katiba Mpya.

..Ngoja tuone kama Jaji Mutungi na wenzake kama wataleta matokeo mazuri.
Hivi vikao wanatumia hela za nani? Kama havina nia ya kuleta matokeo? nani anawajibika kwa matumizi yasiyo ya lazima?

I think by now, wanajua namna nzuri ya kuendesha hili zoezi. Mwanzoni, ilileta shida, sababu ya baadhi ya watu walitaka kuifanya hii ni personal project yao. Wakasahau ni Tanzania na project ni ya watanzania. Ndio maana ikafa kifo cha mende...
Mfano, kuna haja gani ya kuwa na serikali tatu? Bora ijulikane moja tu kuliko kuanza kudanganyana mchana kweupe mambo ya serikali tatu
 

..Znz wanataka mamlaka kamili.

..hivyo serikali 3 ni njia ya kuwapoza wasitoke kwenye muungano.
 
Safi, Mutungi aachie ngazi akasuke ukili na kupigia stori wajukuu zake
 
Ccm hawaitakii kabisa Katiba Mpya! Hii ni mbinu mbadala kutoka kumfivia mtu ugaidi ili kutisha watu kudai katiba mpya hadi kutangulia kuandaa ya kwao feki!
Hivyo vyama mbali na kuwa na makaratasi ya usajili, vina wanachama wangapi?
Mimi naamini hila yao haita fanikiwa kabisa, tena watakwama!
Na kama watafanikiwa basi Wazanzibari ndiyo watakao kuokoa!
 
..Znz wanataka mamlaka kamili.

..hivyo serikali 3 ni njia ya kuwapoza wasitoke kwenye muungano.
Na hiyo ndio obstacle kubwa ya katiba pendekezi ya awamu ya nne. Kwa sasa tuweke mambo mengine sawa. Labda watoto na wajukuu zetu watapindua meza. Ila lazima tuwe na pakuanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…