Kusema kwanini rufaa haijasikilizwa au Kwa nini chadema hawajaenda mahakamani ni kutokuwa mkweli. Chadema kwenda mahakamani haina maana Kwa sababu mbali mbali, moja ni kupoteza resources, muda, na kuwapa muda na sababu wavunja katiba kuendelea kuivunja Kwa kisingizio cha kusubiri maamuzi ya mahakama.
Pili ni kuweka precedence ya kukubali maamuzi huru ya chama kupokwa. Kama chama hakiwezi hata kuamua uanachama wa mwanachama kwa kutumia taratibu zao wenyewe wanabaki na haki gani? Hata hii wakaipiganie mahakamani? Wengine huko nyuma walipitishwa kwenye vigingi hivi walipofukuza wanachama? Kupeleka wanasheria na rasilimali nyingine za chama mahakamani ni kukubali kupokwa mamlaka, na pia ni kama wanapambana na kina Halima ambacho sidhani kama ni kweli au kina maslahi kwao. If anything, chenye maslahi zaidi ni wao kuwa na sababu ya kuonyesha uvunjwaji wa katiba, na kuhoji legitimacy ya chaguzi zilizosimamiwa na NEC, ikiwa moja ya taasisi zilizoshiriki kwenye hili pamoja na Nusrat kuachiwa huru na kuapishwa kesho yake. Mahera alifikia hatua ya kutuambia watanzania wanachotaka kwenye viongozi wa kuwachagua tukiwa kwenye uchaguzi. Kama hii haitoshi kuonyesha clear lack of credibility, hili la wabunge na Nusrat linaongezea chumvi kwenye kidonda. Kilichobaki ni kutafuta pa kuchomokea bila uwajibikaji, bila kushiriki kupaka tope chaguzi, bila kuruhusu ziibuliwe hoja za uhalali/ubatili wa vyombo na viongozi wake.