Mnyika unalalamika 'charge sheet' kutotaja kiasi cha pesa Mbowe alichofadhili ugaidi; hii ni sababu ya kutokuwa na hatia?

Mnyika unalalamika 'charge sheet' kutotaja kiasi cha pesa Mbowe alichofadhili ugaidi; hii ni sababu ya kutokuwa na hatia?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Kuna masuala ya ajabu sana huwa yanachanganya sana. Maana mwanasiasa ambaye ni katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani kulalama huku akiwa hana hoja zenye mashiko ni kukosa busara.

Mnyika analalama kuwa Charge sheet ambayo ameshitakiwa nayo Mbowe haijataja figure kamili ya pesa ambazo Mbowe alizifadhili ili ugaidi kufanyika. Hivyo rais amfutie mashitak. Je, hoja kama kama hii ina mashiko? Huku ni kukuosa uelewa wa mambo.

Kutotaja kiasi cha pesa hakuondoi kosa la mshitakiwa kama Charge sheet inaeleza kwa ufahasa kifungu kilichovunjwa. Labda kama kungekuwa na mkankanyiko juu ya kosa husika na kiasi gani cha pesa kilichotumika.

My take: Viongozi wa Chadema wamekosa busara, hivyo wasilete papara kushughulikia masuala ya kisheria.
 
Kwani kutotaja figure ya pesa alizofadhili ndio hoja?
Issue hapo ni kuwa haya mashitaka ni ya uongo na ndio maana yako nusu nusu.

Ndio upuuzi ule ule wa kuweka watu mahabusu huku mkidai upelelezi haijakamilika halafu mwisho wa siku mnaishia kufuta kesi lengo likiwa ni kumkomoa mtu kwa kumuweka ndani.
 
Mkuu nchi zote bora pasingekuwepo wanasiasa maana ndio wa kwanza kuleta machafuko kwenye nchi yoyote.
 
Haya tuambie hoja yenye mashiko kwako ni ubambikiaji na uoga wa kuisikia habari ya katiba mpya,au ni ipi?Au hoja ni kuondoa kizingiti cha maslahi hata kwa kuitwa mtu gaidi?
 
Idugunde

Ficha kidogo ujinga wako kama hujui uliza
Tunahtaji solid evidence ,amefadhiri shingapi zilienda kwanan nani alipokea alilipwa

Mnatuboa sana

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Kamanda punguza munkari usije ukapasuka bure, Mbowe ana wanasheria wanaomtetea, watahoji mahakamani pindi ushahidi utakapoanza kutolewa.

Hao kina Mnyika wakae watulie wasije wakaingia kwenye hatia ya kuingilia mwenendo wa kesi iliyoko mahakamani.
 
Tujifunze kudadisi pasipo kuwa hisia upendeleo. Hoja yako hata shetani anakushangaa.ehe mungu mshike mbowe Kwa mkono wako wa kuume.
 
Idugunde

Ficha kidogo ujinga wako kama hujui uliza
Tunahtaji solid evidence ,amefadhiri shingapi zilienda kwanan nani alipokea alilipwa

Mnatuboa sana

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Huo ni ushahidi sasa unataka uwekwe kwenye charge sheet. Subiri ushahidi uanze kutolewa ndiyo hayo ya solid evidence utayasikia. Umbumbumbu unawasumbua sana nyinyi wanasaccos.
 
Kamanda punguza munkari usije ukapasuka bure, mbowe ana wanasheria wanaomtetea, watahoji mahakamani pindi ushahidi utakapoanza kutolewa.
Hao kina Mnyika wakae watulie wasije wakaingia kwenye hatia ya kuingilia mwenendo wa kesi iliyoko mahakamani.
Mimi niccm siokamanda ila makamanda kama mbowe wastarabu hua nawaheshimu sana
Namkumbuka kikwete alisema kutumia polisi iposiku ccm tutapasuka msamba

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Mtanzania halali ni mwana CCM tu, wengine wote mpo mpo tu. Kitaeleweka tu siku siyo nyingi.
 
Mkuu haya yanatoka wapi?
Mkuu mimi napenda nchi iwe na amani na kusiwe na uonevu kisa tofaut zetu kisiasa, tufute vyote kabisa ibaki CCM pekee kaz iendelee, maana vyama vingi ni kuwapotezea polisi focus tu
 
Back
Top Bottom