- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekutana na hii poster, ni kweli?
- Tunachokijua
- John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la kibamba 2015-2020, lakini pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la ubungo 2010-2015. Tarehe 08-10-2024 John Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alielezea mambo mbalimbali kuhusu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania bara unaotarajiwa kufanyika 27-11-2024 .
Baada ya mkutano huo kumekuwa na taarifa mbalimbali zikitolewa na kuhusianishwa na mkutano wake aliofanya 08-10-2024 mojawapo ya taarifa hizo ni grafiki inayosomeka kuwa “Tunawakaribisha wale wote waliokatwa CCM waje CHADEMA tutawapa nafasi” ikionesha kuwa maneno hayo yamesemwa na John Mnyika tarehe 08-10-2024 Mikocheni Dar es salaam
Ukweli upoje kuhusu taarifa hiyo
JamiiCheck kwa kupitia ufuatiliaji wa kimtandao imebaini kuwa taarifa hiyo haina ukweli mathalani kwa kufuatilia katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya CHADEMA na katika kurasa za mitandao ya kijamii ya John Mnyika hakuna taarifa inayofanana na hiyo. Grafiki hiyo inaonesha ni kutoka katika ukurasa unaojulikana kwa jina la Chademakaskazini lakini tumefuatilia katika ukurasa huo na kukosa uthibitisho wa kuwepo kwa grafiki hiyo.
Kwa kupitia ufuatiliaji kwa njia ya Google image reverse hakuna uthibitisho wa grafiki hiyo kuwepo katika vyanzo vya habari vya kuaminika na kubaini kuwa picha iliyotumika hapo si ya hivi karibuni na inaonekana kutumika miaka kadhaa iliyopita ikiwemo mwaka 2014 .
Aidha JamiiCheck imefuatilia pia mazungumzo aliyoyafanya John Mnyika siku ya 08-10-2024 na vyombo vya habari ambayo yalikuwa pia yakirushwa katika Chanel mbalimbali za youtube na kubaini kuwa hakuzungumza maneno hayo kuhusu kuwakaribisha waliokatwa na CCM kuwa waende CHADEMA na watapewa nafasi.