Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; Bravo JK



Hivi umesahahu kuwa ni wewe mwenyewe uliyeanzisha thread hii ya kutaka tumpongeze Kikwete. Baada ya hapo umekuja mbogo sana kwa kila aliyekujibu kwa kutokubaliana nawe. Hebu kuwa mkweli urudi nyuma uangalie idadi, aina na maudhui ya post ulizoweka hapa tangu uanzishe thread hii. Ukaichia ile uliyotumia kufungua thread, post nyingine zote ni za kumshambulia kila aliyejibu bila kukubaliana nawe.

Kutokukubaliana ni sehemu ya demokrasi ambayo inafundisha kuwa wengi wape. Wachache wasiokubaliana wengi huwa hawawalazimishi wengi wakubaliane nao, badala yake huwaelimisha kama kweli wanadhani kuwa hao wengi wamekosea. Na endapo wakishindwa, hawawezi kwenda wakipiga makelele mtaa mzima; hunyamaza wakaendelea na maisha yao kama kawaida.

Unataka sisi tufuate mkumbo wako wa kumsifia Rais wakati tunaona wazi kabisa kuwa hajafanya kazi yake; tabia ya kufuata mkumbo ni mbaya na inachangia kurudisha nyuma maendeleo. Wewe hujafanikiwa kutufanya tufuate mkumbo wako kwa hiyo hujachangia lolote kuturudisha numa kimawazo.
 

Kichuguu,
Napenda kukuhakikishia kuwa sijakuja Mbogo hata kidogo kwani hiyo siyo tabia yangu. Mimi nina kawaida ya kubadilishana mawazo kama ambavyo nimekuwa nikifanya tangu mwanzo wa thread hii.

Pili, kama umenielewa vizuri, mimi sijalazimisha mtu yeyote akubaliane na mimi, nilichokuwa ninafanya ni kujibu hoja pale ambapo nimeona ninahoja ya kujibu na kuchangia. Kufanya hivyo ni muhimu kwani majadilianao ndiyo huleta maelewano kwa aina yeyote, iwe ni kukubaliana-kukubaliana au kukubaliana-kutokukubaliana.

Kama unaona haya majadiliano hayako upande wako na unakereka sana, basi unahiyari ya kutokuchangia kwani hapa hakuna anayekulazimisha kuingia kwenye thread hii.
Nadhani umenielewa.
Hongera Mh Rais kwa ku-handle vizuri suala la EPA
 
Jamani nafikili watu lazima tubadilike hata kama baba yako ni kikojozi siku atakapofanya mazuri anastahili kupongezwa kwa hayo mazuri. suala la fedha za epa kwenda kutumiwa na wakulima wadogowadogo ni la msingi na lina hitaji kuungwa mkono na mpenda maendeleo yeyote
 
Bubu ataka kusema,
Wewe siyo msemaji wa 'Watanzania wengi' hizo zako ni hisia tu na ambazo hazijengi hoja ya nguvu katika majadliano.

KAZI IPO. wenzetu mwataka rais awe pia Polisi na mahakama, awakamate watuhumiwa wote wa EPA bila kukusanya ushahidi. alishindwam kesi tumlaumu sisi hao hao.

FUTA TENA
 
In fact sioni wapi pa kubadilisha pamoja na maelezo yako marefu ndiyo umezidi kuharibu na kuonesha kwa kiasi gani umepoteza mwelekeo. Tafuta mtu atayeweza ku-refresh your mind.

Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu! Wenye muelekeo ni mafisadi tu wanaofilisi nchi hao siku zote utawaona wana muelekeo. Mind yangu haina matatizo yeyote labda kwa mafisadi na masupporters wao ndiyo wanaona hivyo.
 
Tatizo ninaloliona hapa ni kuwa EPA imegeuka kuwa ajenda ya kisiasa badala ya kuchukuliwa kama criminal act ambayo ina taratibu zake za kushughulikiwa.Yangu macho.
 
wadau naona mtatoana macho bure.hakuna marefu yasiyo na ncha,na hili la EPA iko siku litafikia mwisho wake,tuombe uhai.
 
Hivi Nyerere aliposema,..."Kama mtu mwenye akili akikupa wazo la kijinga akijua na wewe una akili nawe ukalikubali (wazo hilo) atakudharau..." alikuwa anawaambia watanzania wepi?{May 1,1995 Mbeya}
 
Tatizo ninaloliona hapa ni kuwa EPA imegeuka kuwa ajenda ya kisiasa badala ya kuchukuliwa kama criminal act ambayo ina taratibu zake za kushughulikiwa.Yangu macho.

EPA ni mfano mmoja tu. Fisadi mkapa kaiba Kiwira mpaka leo hakuna kilichofanyika kuhakikisha Kiwira inarudishwa chini ya miliki ya Watanzania. Mzee wa vijisenti kakuta na shilingi bilioni kwenye bank account nje ya nchi, hadi hii leo hatujui kinachoendelea. Yule mhindi wakala wa ununuzi wa Rada, ndege ya Rais (ambayo sasa inataka kuuzwa kwa sababu ni bomu) na helicopters na magari ya jeshi aliyejipatia shilingi bilioni 12 za walipa kodi wabongo hajulikani yuko wapi. Meremeta ambayo ilijipatia shilingi bilioni 155 tunaambiwa ni habari nyeti hivyo haistahili kujadiliwa. Mambo chungu nzima ya kifisadi hakuna hata moja linaloeleweka lakini pamoja na hayo kuna watu wanathubutu kutamka kwamba wenye dira ya kuongoza nchi ni chama cha mafisadi pekee! Eh! Wadanganyika mtaendelea kudanganyika mpaka lini!?
 

Una nchi wewe? nenda katibiwe hicho kifafa kwanza ndo uje hapa tuargue vzr!
 
Yaani kumpongeza Rais nako ni kujali utaifa? wewe ndiyo pundamilia kabisa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…