Mnyororo wa thamani uko wapi; Malighafi za Tanzania au bidhaa zinazozalishwa Kenya?

Mnyororo wa thamani uko wapi; Malighafi za Tanzania au bidhaa zinazozalishwa Kenya?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
MNYORORO WA THAMANI UKO WAPI; MALIGHAFI ZA TANZANIA AU BIDHAA ZINAZOZALISHWA KENYA!?

Je, ni kweli kilimo ni biashara kichaa!! Jibu ni hapana. Je, hakuna masoko ya Kilimo!? Jibu ni hapana, wapo watakaokushawishi kulima lakini mazao yakikomaa watakukwepa!! Hii ni sababu ya mnyororo wa thamani, uwepo wa Viwanda unaongeza mnyororo wa thamani, kukosekana kwa viwanda kumeondoa uthamani wa bidhaa na kuleta madalali,walanguzi na matapeli na kuondoa wanunuzi wa uhakika, wanunuzi waliojua kuwa udhaifu wa Watanzania ni mnyororo wa thamani wameleta wababaishaji, na hata mashirika nayo hayana ushirikiano.

Mnyororo wa thamani unajulikana kama (value chain creation) ni mtiririko wa shughuli zote zinazofanywa katika uzalishaji hadi kumfikia mlaji,mtiririko huu unajumuisha shughuli mbalimbali hadi kufika kwa mlaji ambae ni mtumiaji wa mwisho wa bidhaa au zao lililozalishwa,kila kazi inayofanywa kutimiza mzunguko mzima huongeza thamani ya zao au bidhaa husika,kwa mfano;

✓Uzalishaji.
✓Usafirishaji.
✓Usindikaji.
✓Uhifadhi.
✓Upangaji wa madaraja.
✓kufungasha na,
✓masoko.

- Kwa sasa,nani ameshikiria mnyororo wa thamani kati ya Kenya na Tanzania!?

Mjadala uliopo sasa ni kuiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuondoa mipaka, nitoe rai yangu kwa Watanzania kuwa tayari,maana wengi hata ukipitia maoni yao ama comments zao mitandaoni utagundua asilimia kubwa bado ni wajinga wa kupindukia, huwezi kufananisha na Waganda au Wakenya,najua humu humu kwenye mitandao watu watabisha lakini atakwenda kumpa maisha yake Mkenya, nimekutana nao mara nyingi nje ya nchi kuanzia Kenya niliposoma, Uganda nilipoenda kutembea na hata Uingereza nilipoenda kuongeza elimu, nchi za Afrika ya kusini wana vipengele muhimu vya kuongeza thamani nchini mwao, nadhani maswahibu mengi walitopitia yamewapa maarifa mengi!

-Tanzania for Raw Materials and
Kenya for Manufactured goods.

Ni kweli Wakenya wanaongoza kwa kununua bidhaa za Tanzania,lakini ni bidhaa ambazo hazijaongezwa uthamani, malighafi(raw material) na Kenya wanaongoza kwa kuziongeza uthamani bidhaa hizo na kuja kuziuza tena Tanzania, ni kitu iko iko, kinanunuliwa kwetu kama malighafi halafu kinarudishwa tena Tanzania kama bidhaa iliyoongezwa uthamani na itauzwa kwa pesa ghali tofauti na ilivyonunuliwa kwa pesa kidogo,so anufactured goods kutoka Kenya zinauzwa tena hapa hapa Tanzania kwa kutolea mfano sabuni za vipande, sitazitaja jina kwa sababu za kimasoko lakini pia zipo kandambili zimejaa hadi vijijini achilia mbali kwenye mainstream markets kumejaa manufactured products kutoka Kenya kwa (malighafi) raw materials zilizotoka hapa hapa Tanzania.

Kule Kenya manufactured products kutoka viwanda vya Tanzania ni kama hakuna ukienda mipaka ya kenya magari yamejaa ng'ombe hai bidhaa za mashamba na ndio maana Kenya anaongoza kuuza kila kitu kwenye soko la ndani na nje ya Afrika Mashariki kuliko Tanzania kwa sababu wameigeuza Tanzania kama shamba lao la kupata malighafi na wao kwenda kuziongezea uthamani kisha kurudi tena Tanzania kutuuzia sisi,tuchukulie mfano gas inakwenda Kenya wakati Dar es Salaam Pwani, Morogoro, Tabora, Kigoma, Mwanza, Tanga, Dodoma hakuna na hakuna plan yeyote ya kuipeleka kwa viwanda vya huko, sasa kwenye biashara wenzetu wanachukua kila aina ya malighafi(raw material)na sasa tunawapa gas kwa kipaumbele kisha bidhaa zao zitakuwa na soko la ushindani mkubwa(competitive selling price) dhidi yetu sisi Watanzania zikija hapa hapa Tanzania. Je, tumejiandaa kushinda au tumejiandaa kushindwa?

- Malighafi inapokwenda Kenya ni hasara kwa Tanzania, kwa sababu ya mnyororo wa thamani.

Ongezeko la kuuza Malighafi kwenda Kenya kwa mtazamo wa Uchumi biashara na mauzo ni hasara kubwa kwa Tanzania, kwa sababu mnyororo wa thamani (value chain) inakwenda kufanyika Kenya katika (processing, packaging) nk, Pia kuwapa gas Wakenya kama kipaumbele wakati sisi hata mkoa wa mtwara pwani, dar es Salaam hakuna mtandao wa gas viwandani haijakaa vizuri, kwa muktadha wa ongezeko hilo kubwa la kuuza Malighafi kwenda Kenya, Wakenya wamejaa hadi wanaenda kwa wakulima kununua mazao na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vyao kwa bei ya shambani huko vijijini, Pia wamejaa huko vijijini kwa wafugaji kununua ng'ombe mbuzi na mifugo hai kwa bei ya vijijini na minadani kisha kupeleka Kenya kufanya processing and packaging kuuza kwenye masoko mbalimbali ikiwemo dubai kwa pesa nyingi za kigeni.

Binafsi ningefurahi sana Viongozi wetu wafundishwe kuwa (Economy business and trade minded leaders) maana sasa vita kubwa duniani ipo kwenye Uchumi, biashara na mauzo,hatupo kwenye biashara ya kisiasa kama zamani.

- Tunahitaji nini Watanzania kwenye mnyororo wa thamani.

Utekelezwaji wa mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani katika bidhaa na malighafi za Tanzania utanufaisha watu wengi hasa wa kipato cha chini kwa kuwa Tanzania ndio shamba la malighafi za bidhaa zote zinazopatikana Afrika Mashariki, tukiweza hili la mnyororo wa thamani, Tanzania tutachukua nafasi kubwa katika biashara na mauzo,kwenye mnyororo mzima wa thamani kwenye kilimo (agricultural value chain)kitengo Cha kurahisisha mahusiano na mawasiliano kwa washikadau (stakeholders) wote ambao wanaingia kwenye sekta hii ya kilimo na ufugaji,taarifa zote muhimu za mkulima ambaye ni mdau muhimu kwenye uzalishaji wa mnyororo wa thamani,uwezeshwaji kama mkulima atataka kupata mafunzo yoyote kutoka kwa taasisi yoyote, mafunzo hayo yanaweza kua, jinsi ya kulima kisasa ( good agricultural practice) mafunzo ya kifedha (financial education) nk,taarifa zote za kimikataba, ikiwa mkulima au wazalishaji watakua na mkataba na mnunuzi wa malighafi au bidhaa,na mwisho taarifa zote za mbegu na mbolea ambazo mkulima alitumia mwanzoni mwa shughuli yake, pia kurekodi taarifa za mavuno mwishoni wakati wa mavuno, baada ya hapo twende kwenye viwanda tukaongeze uthamani wa malighafi zetu ili ziwe bidhaa adimu, tukatae kuwa wachuuzi wa finished goods zilizotokana na malighafi zetu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Asante hoja nzuri mkuu,swali langu unafikiri ni serikali pekee ndo imepelekea haya kama jibu ndio kwa nini na kama sio kwa nini
 
-Tanzania for Raw Materials and
Kenya for Manufactured goods.
Mkuu 'Mwande na Mndewa', andiko lako ni refu, na ninakuhakikishia tabia moja wa waTanzania, na hasa wa hapa JF wanaoakisi tabia hiyo kikwelikweli, hawatapata muda wa kulisoma lote, na si ajabu mada yako ikakosa uchangiaji unaostahili kwa swala zito kama hili.

Mimi nimeamua tu kubeba hayo maneno uliyoandika katika misttari mifupi hapo juu.

Kuna waziri mmoja toka Kenya miaka hiyo ya nyuma alikuwa akizungumzia swala hilo hilo, hasa katika ushirikiano wetu mpya katika jumuia ya Afrika Mashariki.

Waziri Mukhisa Kitui, ambaye wakati huo alikuwa ni waziri wa biashara alilizungumzia swala la ushirikiano wetu akitumia mfano wa zao la pamba na uzalishaji wa bidhaa zitokanzao na pamba. Akaeleza kwamba jukumu la Tanzania itakuwa ni kulima pamba, Uganda wataichambua pamba hiyo na kutengeneza nyuzi ambazo Kenya watazalisha nguo na kuuza kwenye soko letu na nchi za nje.

Kwa hiyo, haya uliyoandika hapa si mageni kwa wengi, isipokuwa kinachoshangaza ni kwa nini waTanzania hawajifunzi kitu kutokana na haya yote.

Yule rais, ambaye pengine yasingekuwa matatizo yake mengine ya kiakili, John Magufuli, kidogo alilielewa hili, ila kutokana na shida zake hakuweza kulishughulikia kwa njia ambazo zisingeleta tafaruku nyingi.

Leo hii, tunaye rais mwingine anayeamini kabisa kwamba maendeleo ya Tanzania hayawezekani bila kuwategemea watu toka nje, ikiwa ni pamoja na huyo jirani yetu.
Ndiyo maana, yeye wimbo wake mkubwa sana ni kuuza gesi Kenya ili wakaitumie hiyo gesi kuzalisha bidhaa nafuu zaidi ili watuuzie sisi.

Ruto yeye mkazo wake upo katika kuwainua wajasiliamali wadogo wa huko, wenye viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo, wengi wao waweze kuinua maisha yao na kwa njia hiyo maendeleo yao. Samia anaamini tutauza gesi Kenya ili tupate pesa za kigeni na mradi huo wa bomba utaajiri watu watakaofaidika na kazi hiyo. Katika mlinhanisho kati ya hawa wawili utaona wazi ni wapi palipo na manufaa zaidi kwa wananchi.

Sasa nisije nikaandika sana na nikashindwa kusomeka kama nilivyoeleza kuhusu andiko lako.

Lakini ninayo mifano mingi tu ninayoweza kuiwasilisha hapa kuonyesha ujuha wa viongozi wetu. Kinachoshangaza zaidi ni kwa nini hasa tunajiweka kuwa tegemezi zaidi kwa hawa majirani zetu. Ni kama wametushikiria kama sumaku!
 
Viongozi gani wa kufundishwa business hawa wanaogonga meza kujadili hoja nyepesi?

Yaani unatarajia bunge la kina msukuma na kibajaji lijadili habari za transformation of raw materials to end products, lazima utakua unaota.

Pia chama gani kimetufikisha hapa maana naona unazunguka , elimu yetu kimsingi ni duni ukibisha lazima utakua hujasoma Kenya hebu linganisha graduate wa chuo kikuu Kenya na Tanzania hapo utapata jibu.

Mfumo wa elimu wa Tanzania ni dumavu umejenga vijana kufikiri hapo kwa hapo nje ya box wala angalia wakenya wanavyochangamkia fursa za abroad utakutana na wakenya 20, wanigeria 50, waghana 30, ila wabongo unaweza kuta 5 hadi 0 ukitoka nje ya bongo unaitwa wewe msaliti sio mzalendo kwa mentality hizi unafikiri kuna jipya?
 
EeeeenHeeeee, ninakukumbuka sana wewe kuhusu mijadala kama hii juu ya nchi hiyo. Tulishakutana hapa hapa JF.
Bila shaka ni kwenye uzi wangu ambao nilieleza kuhusu uchumi wa Kenya na Tanzania...
 
Unaacha kukomaa uchangamkie fursa kwa kuongeza thamani unaanza kulalamika Wakenya na kulaumu Serikali,huu ujinga ufikie mwisho.
 
Unaacha kukomaa uchangamkie fursa kwa kuongeza thamani unaanza kulalamika Wakenya na kulaumu Serikali,huu ujinga ufikie mwisho.
Watanzania ni kama tumekata tamaa na kuamua kutoka moyoni kua wachuuzi.

Kila kitu kinafaida zake, ila kama taifa hatuwezi kupiga hatua kwa kua na idadi kubwa la wachuuzi.

Ni jukumu la viongozi kujua shida iko wapi na kuturudisha kwenye mnyororo wa thamani, kitu ambacho sio rahisi kama tutaendelea kupanga mipango kazi ya miaka mitano ya uchaguzi.

Kosa kubwa tunalolifanya siku zote, ni kuamini kupiga marufuku kuuzwa nje kwa mazao ya chakula, hii ina solve tatizo la food security lakini ni kwa mda mchache, na muhanga wa hili ni mzalishaji wa kwanza(Mkulima).

Wakati mwengine serikali inatakiwa kuongea na matajiri hata kama ni wa kutoka kenya waweke viwanda hapa vya kutengeneza unga wa mahindi ili tuuze unga na sio mahindi kama tunavyo fanya, hii inatakiwa kwenda sambamba na kuongeza kodi kwenye kuuza mahindi nje ya mipaka ya Tanzania.

Wakenya wanatumia loopholes tulizo nazo kujinufaisha wao, na sisi watanzania tupunguze lawama tuangalie fursa zilizopo kwenye muungano huu wa EA tuzitumie kama wenzetu wanavyo fanya.

Kuna mfano wa bidhaa mbali mbali zinazotoka kenya(i.e kwenye kilimo) zinafanya vizuri hapa sokoni kuliko zinazo zalishwa hapa kwetu kiasi cha kufanya bidhaa za ndani zishindwe ku compete bila figisu.

Sasa unajiuliza tuendelee kuwalaumu hawa wakenya au Tujitazame sisi kwanza na turekebishe kasoro zetu.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom