Asphalt1961
Member
- Jan 7, 2022
- 7
- 25
Ndugu wana-Jamvi Wakati Vuguvugu la Uchaguzi linazidi kupanda kuelekea mwakani 2025, wabunge matumbo joto kila kona na tayari sarakasi zimeanza. Wilaya ya Mufindi imekuwa kwenye dawati kwanza kuonja joto la jiwe.
Mnamo tarehe 6 Juni, Kundi la Vijana kutoka Jimbo la Mafinga Mji wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Bwana Christian Mahenge lilivamia Ofisi za Vijana na kuweka kufuli za mchina kuhakikisha Mtendaji wa Wilaya haingii ofisini humo na kushinikiza Chama kimuondoe Katibu huyo mara moja.
Tumearifiwa kwamba Vikao vya CCM vimeanza kukutana kujadili jambo hilo, Kikao cha Kamati tekelezaji wilaya kimekutana sambamba na Kamati ya Maadili- Vikao vyote vikajaribu kunasua hali hii hususani mwaka huu ambao Chama cha CCM kinaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.
SWALI KUBWA LINALOKUNA VICHWA VYA WENGI NI NANI YUKO NYUMA YA PAZIA?
Mambo mengi yameacha maswali ila mimi nimeona haya machache
Kwanza, Wilaya ya Mufindi ina Majimbo matatu Jimbo la Mafinga Mji, Mufindi Kusini na Mufindi Kaskazini. Lakini ya waliojitambulisha kwenye Mtanange huo imebeba Mwenyekiti Wilaya, Wenyeviti na Makatibu wa vijana Kata, Greenguard, wauza sura pale CCM na makada wa kawaida, Swali ni Kwanini washiriki wa zoezi hili ni vijana wa Jimbo la Mafinga Mji tu? Je ni vijana wa Mafinga peke ndio wana uchungu sana na Jumuiya hii?
Je Vijana wa Majimbo mengine hawana uelewa wa mambo? Je wamegoma kutumika! Je Mfadhili alikuwa na maslahi gani? Maswali ni mengi kuliko majibu. Jibu moja jepesi ni kwamba kilicho nyuma ya pazia si vita ya Katibu na Mwenyekiti wa Vijana, ni homa ya uchaguzi 2025 na upangaji Safu ndani ya Sekretarieti ya Wilaya
PILI, Kwa wanaoishi hapa Mafinga wanafahamu mnyukano wa Ubunge Mkubwa ni kati ya Mbunge aliyepo Cosato Chumi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya Basil Tweve, Katibu Mwenezi Wilaya Dickson Villa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Aggrey Tonga. Hata hivyo Vita hii inahusu Mafahari wawili (Sitawataja) na katika hao mtia nia mmoja inasemekana anabebwa Kigogo mmoja ndugu yake mwenye ukwasi wa kutisha.
Tatu, Ukirejea nyuma Katika uchaguzi wa UVCCM Wilaya wa mwaka 2022 familia ya Kigogo huyo mwenye ukwasi alimuunga Mkono Mwenyekiti aliyepo wa Wilaya kwa fedha taslimi milioni sita(6m) sambamba na mafuta ya gari. Wakati mgombea mwenza aliungwa mkono na Mwenezi wa Wilaya Ndugu Villa Lutevele. Kwahiyo Anachofanya Majenge si kingine, anakulipa fadhila tu.
Pia, Kila mtu anafahamu kwenye mnyukano wa Mwaka 2025 Mahenge ametangaza hadharani vita kuhakikisha mgombea wake anaibuka mshindi bila kikwazo. Lakini Taarifa zisizothibitishwa zinamtaja Katibu wake anayelalamikiwa Ndugu Isac Mbuya kuendesha magenge ya kuhakikisha kama sio Mgombea mwingine(jina kapuni) anaibuka basi chumi aendelee kuongoza. Akieleza haweza kukubali jumuiya ya UVCCM kuwekwa mfukoni mwa mtu kisa fedha.
Nne, Kundi kubwa la vijana liliobeba mabango, takribani asilimia 90 ni wale wanaomuunga Mkono mgombea wa Mahenge awe Mbunge mwakani 2025 kwa hoja kwamba hawawezi kumwacha mwenzao.
Haijulikani kwa nini anaonekana na mwenzao
Mathlani, Mwenyekiti Mahenge hana kazi ya kumwingizia kipato kikubwa lakini, lakini kila mtu anajiuluza maswali:
i. Je vijana wote walioshiriki na kulipwa posho laki 1 hadi 3 kila mmoja kulingana na umuhimu wake, pesa zilitoka wapi?
ii. Jambo gani lililofanya vijana pamoja na baridi kali ya mafinga, wakubali kuamka alfajiri saa 12 kwenda kuandamana kufunga ofisi ya Wilaya?
iii. Vijana walipanda boda boda kufika MAM Hall sehemu ya kukusanyikia je nani alilipia pesa za pikipiki na kwa maslahi gani?
iv. Kwenye tukio hilo pia Waandishi wa habari wakiwa na kamera za kisasa walidamka mapema kuacha vitanda vyao kuhakikisha tukio linakuwa well covered na kuhakikisha linafikia vyombo vyote muhimu kimkakati kuanzia Mufindi FM, EBON FM, Mwananchi digital na vyombo vingine muhimu. Ni msamaria mwema gani alilipia media hizi na kwa faida gani?
v. Mara baada ya tukio kukamilika kundi la vijana liliekea bar ambapo walionekana wakijichana Supu za mapaja ya Kuku na pombe za kutosha- hakuna anayefahamu nani alitoa pesa zote hizo.
Ikumbukwe Iko hoja kuwa vijana waliijenga kwamba Katibu anapwaya, hatekelezi majukumu yake. Hana uwezo na mpiga dili, Swali:- Mwenyekiti huyu msomi kutoka Chuo Kikuu cha SUA Morogoro anafahamu taratibu za kushughulika na Katibu badala ya Media. Anafahamu viko vikao vikuu vitatu ambayo vya kumshughulikia Katibu. Kikao cha kwanza ni Kamati tekelezaji na cha pili ni Baraza la Wilaya- Vikao vyote hivi anaviongoza yeye. Kikao cha tatu ni Kamati ya Siasa ambacho yeye Mwenyekiti ni Mjumbe. Kwanini hajaamua kuvitumia?? Kuna agenda ganj imejificha?
Ikumbukwe miezi michache Mwenyekiti ametoka kujaza fomu za utendaji wa katibu hyo ambazo alimsifu na kumwelezea ni mtu anayechapa kazi. Kipi kimetokea ghafka??
Ifahamike kwamba, Vijana walipaza sauti kwamba yupo mtu mzito nyuma ya Katibu wa Vijana Wilaya anazuia katibu asitekeleze maagizo. Asihame, Anampa jeuri Katibu. Je mtu huyo ninani? Anakwamisha shughulu za UVCCM kwa faida ya nani na anakwamishaje? Je mu huyo ni Mtendaji wa Jumuiya? Je mtu huyo ana uwezo Kiasi cha kuingilia mifumo ya ajira za Chama? Na ana maslahi gani na jambo hilo.
Kanuni za CCM haziruhusu kabisa alichofanya Bwana Mahenge, adhabu yake ni ama asamehewe, ama apewe Onyo, Ama Onyo kali ama afukuzwe kabisa kwenye Chama. Ikumbukwe kwamba, Tayari Mahenge alishapewa onyo kwa utovu Mkubwa wa nidhamu kuchafua Chama na uchonganishi. Kutoa siri za vikao bk.
Na kwa wanaokumbuka kwenye uchaguzi wa Mwaka 2020 Bw Mahenge akiwa Mwenyekiti alizuiliwa kuhudhuria vikao vyote vya kujadili wagombea kwa sababu ya kuonekana anatumika na makundi ya wanasiasa kutoa siri za vikao. Ni kwanini kijana huyu kila wakati anatumbukia kwenye shimo la kutumika??
Kwa mujibu wa taratibu za Chama huwezi kupewa onyo mara mbili hivyo ama apewe Onyo kali ama afukuzwe kabisa Uanachama.
Jana Nimepita viunga vya CCM, nderemo na vijijo vimeanza kusikika kutoka kwa mahasimu wake ambao wangetamani afukuzwe kwenye Chama mapema iwezekavyo ili uchaguzi uitishwe apatikane mwenyekiti mpya ambaye hatakuwa dalali wa siasa za Mufindi na anaweza endelea utulivu, mshakamano na umoja.
Mwisho, Pamoja na kuungwa mkono kwa mbali na vigogo wachache ndani ya Kamati ya Siasa Wilayani lakini bado hali ni tete na haijulikani hatima ya Bwana Mahenge itakuwaje ingawaje ziko tuhuma mpya kwamba amenunuliwa na vyama vya upinzani ili kudhoofisha CCM kuelekea chaguzi za mwaka huu na mwakani. Na kwamba huu ni mkakati wa kwanza iko mikakati mingine inafuata.
MNYUKANO UMEANZA MAPEMA KULIKO ULIVYOTARAJIWA, JE NINI HATMA YA YOTE HAYA?? YETU MACHO.