MO amenunua gari inayoaminika kuwa na mfumo mkubwa wa ulinzi wa kidigitali

Nimekumbuka huu wimbo 🎢 mwombee adui yako aishi siku nyingi ili unapofanikiwa ajionee kwa macho .........!!πŸ‘πŸ™‹
 
Hili suala micro chip lilikuwa kweli au propaganda tuu wajameni?
 
Reactions: y-n
Kuwajua watekaji ni jambo moja na kuwakamata ni lingine.
Wa awali mbona wanawajua!
 
Reactions: y-n
Tatizo aatatumia mbinu nyingune kumteka, watamteka yeye pamoja na gari yake wakaitumbukize baharini unless awe ameuganisha kamera za gari na simu yake na ndugu zake au na sourse nyingine inayoweza kutunza ushahidi ili hata wakiangamiza gari ushahidi usipotee
 
Umesahau kusema kuwa lina mfumo wa Auto Pilot ambapo gari linaeza kujiendesha lenyewe though tesla wenyewe ukinunua unasaini mkataba kuwa hutoliacha gari lijiendeshe pasipo wewe kuwa makini pia.
 
Hana lolote kaogopa kusema waliomteka.Hicho kigari mikoani hakiendi bumps
 
Inapendeza...

That's all about business, tajiri kama huyo kununa hilo gari ni kutangazia biashara Tesla...

Sheria zetu za usalama barabarani zinasemaje kuhusu gari isiyokua na mfuno uliozoeleka(engine) badala yake ni umeme tuu na yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe? Zinaruhusiwa au inakuaje?


Cc: mahondaw
 
Kwa wasiojua hio tesla model 3 ndio the cheapest car kwny magari ya Tesla,iko targeted kwa watu wenye kipato cha kawaida tofauti na model nyingine za Tesla.

Ku-charge tesla nyumbani kwako inahitaji "NEMA 14-50 connection" ambayo Labour+Material itagharimu $1500 only(dolla elfu moja mia tano tu) ingawa pia mwenye 240V-outlet anaweza ichaji gari so mfumo wake wa kuchaji sio ghari kama tunavyotaka kudanganywa hapa.

By the way hapa hapa dar kuna mtu ana tesla model X ya 2018 ambayo kuinunua tu ni usd 102,000 bila mambo za TRA.

So kwa utajiri wa MO kununua hio gari ya MRP $35,000 sio inshu wala.
 
Baada ya kile kinachooneka kuwa ni kuimarisha ulinzi na kutuma salaam kwa watekaji, MO amenunua gari inayoaminika kuwa na mfumo mkubwa wa ulinzi wa kidigjtari.



Muda mfupi baada ya MO kuposti picha hiyo (Tesla Model 3), mtandao unaoaminika kule Nigeria wa Pulse, uliandika kuwa MO amenunua gari hilo kwa dola za Marekani 35,000 (Sh80 Milioni). Hata hivyo, mtandao wa Tesla wenyewe unaandika kuwa Model 3 inauzwa dola 46,000 (Sh106 Milioni).

Makadirio ya kununua Tesla Model 3, kulisafirisha mpaka nchini, kodi na kuwatela wataalamu wa kumfungia mfumo wa kuchaji gari lake nyumbani kwake, inaweza kufikia kati ya Sh250 milioni. Watekaji wote salamu zenu kutoka kwa MO. Ni salamu za kufungia mwaka 2018.

Tesla Model 3 ni gari linalozalishwa na Kampuni ya Tesla Inc ambayo yenyewe imejikita kutengeneza magari yasiyotumia mafuta. Magari ya Tesla yanatumia gesi na umeme tu.

Tesla M3 halina injini kabisa. Gari lote ni umeme. Halina muungurumo. Linatembea kimyakimya, kama huelekezi macho lilipo, litapita nyuma yako pasipo wewe kujua kama kuna gari limekupita.

Lina camera za dashboard, yaani dashcam. Zenyewe huchukua matukio yote mbele, nyuma na pembeni kuzunguka gari. Ni kamera za mzunguko wa nyuzi 360 na huchukua video zenye ubora wa hali ya juu, yaani HD.

Sifa nyingine ni Tesla Model 3 ni gari kamili la kidigitali. Halina ufunguo, linatumia rimoti yenye umbo la gari lenyewe. Ukishaingia kwenye gari, kwenye dashboard kuna kitu mfano wa tablet. Hiyo ndiyo unaitumia kuendesha gari.

Ukiamua hata hiyo rimoti yake si muhimu sana. Unaweza kuweka App ya gari kwenye simu, kisha utaitumia simu yako kuendesha gari, kufungua milango, kufunga na kulidhibiti.

Tesla Model 3 lina mfumo wa autopilot ya kiwango cha juu kama ndege. Autopilot huwezesha ndege kujiongoza yenyewe ikiwa angani kwa kutambua sehemu hatari kupita na kuchagua uelekeo salama.

Kwa Tesla Model 3 kuwa na autopilot, inalifanya gari hilo kujiendesha lenyewe. Lina kamera za kutosha zenye kuona mbali (autopilot cameras), hivyo hata dereva akilikimbiza, lenyewe hutambua hali halisi ya barabara mbele ya safari, kwa hiyo hupigia kengele ya alarm. Dereva asipotii, gari lenyewe hufunga breki. Gari lina automatic break.

Gari haliwezi kugonga. Unaweza kuliendesha hata ukiwa umelala, maana likikaribia kugonga gari lingine au kitu chochote, linaona na kufunga breki lenyewe (umeambiwa lina automatic break). Ni gari ambalo limepiga hatua kubwa kufikia kiwango cha kuwa gari lenye kujiendesha bila dereva.

Tesla Model 3 haliwezi kuibiwa kabisa. Kwani katika dashboard limefungwa kitu kinaitwa Smart Summon. Kwa hiyo popote pale litakapokuwa, mmiliki wa gari kwa kutumia rimoti au simu yake yenye App ya Tesla Model 3, ataweza kuliita gari, hata likiwa nchi nyingine. Kumbuka linaweza kutembea bila dereva.

Kwa mantiki hiyo, kama MO angekuwa anatumia Tesla Model 3 kipindi kile alipovamiwa na watekaji Hoteli ya Colosseum, October 11, 2018;, maana yake sasa hivi gari hilo lingerekodi matukio yote, na pengine watekaji wangejulikana kwa picha zao siku ya kwanza.

Ref. Jeuri ya Mo Dewji atuma salamu kwa watekaji
 
Kwani hao watekaji mbona hadi sasa hatujaambiwa ni kina nani?ina maana hawajakamatwa kama wale walio mshambulia Lissu?
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…