Mo anajenga klabu, Manji anatafuta sifa na manufaa

Mkodisho fc




ACHA ACHUKUE AU AKODISHIWE KWA ZAIDI YA MIAKA LAKI 8....

CHA MUHIMU NI PALE NINAPOIONA YANGA SC IKIMNYONYA SIMBA (NDAMA FC) LITA 2 ZA MAZIWA WAKATI AKIWA NYUMBANI (ZIZINI) & LITA 2 NYINGINE AKIWA UGENINI (MALISHONI)
 
Mo na manji ni wahind matajil,wanafanya biashara,hivyo sis mashabiki wa mpira tanzania tunakalia maneno,majungu,na ushamba,wenzetu wanaandaa hela kwa ajili ya familia zao,na ni utajili wa familia zao,tuwaunge ili watusaidie timu zetu yanga na simba zidumu,kwan mashabiki wengi hatuna hata uwezo wa kununua kiatu cha mchezaji,hongera zao manji na mo,tusaidien ili hiv vilabu vya simba na yanga vipunguze umasikin
 
huna lolote la maana zaidi ya ushabiki Tu,hivi Kuna tathmini gani ya kiuchumi mliyofanya kuhusu hizo hisa51 kwa bilioni 20?kipi Nora kiiza au kukodisha?rage hakukosea kuwaita mbumbumbu
 
Kaa tena chini uandike kitu cha maana,binafsi siafiki hizi timu kumilikiwa na hao kuchkuch i know nia yao kubwa ni kutengeza hela kwanza.

Kutoa hiyo 100 m ya usajili ndio unaona msaada mkubwa ?


MILION 100.

Hapa niliamini kuwa wamatopeni wako desperate sana hata wameshindwa kuona mauza uza kama haya ya milioni 100.
 
mkuu bado hujajibu swali...mbona kabla Mo hajataka kuwekeza Simba Manji alikuwa hakodi timu kwa miaka 10?


Kila jambo linakuwa motivated na jambo lingine.....

Kilichotokea kwenu (mchangani) kimefumbua wazo jipya la ziada ambalo halikuwahi kitokea barani Afrika.

Unakumbuka hata nyinyi mmekuwa motivated na suala la kupiga bei klabu yenu, mara baada miaka ile ya nyuma Yanga kuwa na lengo na hata kudiriki kufikia hapo. (Licha ya kuwa na migongano ya Mawazo)
 
Uzi wa mambulumundu huuu!!
Hivi anayenunua timu forever, kwa maana nyingine anaye jimilikishaa timu kinyemela yeye na familia yake adi siku ya kiama na anaye kodi timu kwa miaka 10, kati ya hawa wawili ni yupi jizi lililokubuhu?
Kama hujui basi na wewee *********
 
Mpira Bongo hauna faida,yaani haupo kibiashara kabisa,kwani hakuna kampuni zinazowekeza kwenye michezo,tofauti na nchi kama afrika ya kusini au nchi za kaskazini mwa Afrika ambapo uwekezaji kwenye michezo ni mkubwa kuliko hapa kwetu, na hasa kutokana na ukubwa wa uchumi wa nchi zao,tofauti na hapa Bongo ambapo wawekezaji kwenye soka wanawekeza kimapenzi au kimsaada na sio kibiashara.MO kaenda kuwekeza Simba ili akuze jina lake na jina la biashara zake ,hakwenda pale kwamba eti Simba ina uwezo wa kumwingizia hela ,HAPANA amekwenda kuongeza CV tu katika biashara zake na yeye afanane na Moise Katumbi wa Mazembe ,kwani biashara kuu ya timu za mpira ni Haki za matangazo ya Tv ,Mauzo ya jezi na bidhaa mbalimbali za klabu,udhamini wa kampuni mbalimbali kwenye jezi za klabu kama ilivyokua kwa KILI LAGER kwa yanga na simba n.k.
 
Kaa tena chini uandike kitu cha maana,binafsi siafiki hizi timu kumilikiwa na hao kuchkuch i know nia yao kubwa ni kutengeza hela kwanza.

Kutoa hiyo 100 m ya usajili ndio unaona msaada mkubwa ?
Kwani wao wakipata maslahi na timu ikapata matokeo mazuri kuna tatizo gani? Mnawalaumu tu kina jimi jimi jimi mbona kina wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika hatuwaoni kujitokeza kusaidia timu hizo kwa nia njema?
 
SIMBA NA YANGA Tuachane kabisa na Matajiri hawa wenye mrengo wa CCM Au hata wa Vyama vingine vya Siasa... wote ni wapenzi na washabiki wa kutupwa wa CCM ..Tuachane kabisa kuuza timu au kukodisha hizi timu ambazo zinaunganisha Watanzania wote bila ya kujali tofauti za Kisiasa au Dini Kuna Hatari zake.
Nitakupeni Mfano wa wazi.
Kabla Ya Uchaguzi wa Kwanza wa Vyama vingi Kule Zanzibar Football ilipanda Juu sana. Timu za Zamani kama
Malindi
Miembeni
Vikokotoni
Kikwajuni
KMKM
Jamhuri

na zile Mpya kama
Small Simba
Black Fighters
Annur
Shangani nk


zilikua katika hali ya kiwango cha Juu na kuweza kutoa wachezaji wengi wazuri kwenye timu Ya Taifa Stars...
Malindi mwaka 1994 ilikua chini ya Mohammed Raza Na Naushad, Mwana CCM kINDAKI NDAKI...iliweza kusajili wchezaji wazuri na makocha wa nje. Ilifanikiwa Kuingia Fainali ya FA la Africa...
Baadhi ya Timu Hizi zimewahi kuchukua Ubigwa wa Tanzania Wakati ule Ligi ni Moja
Small Simba nayo ilikuwa chini ya Raza mdogo
nazo Timu za Shangani , Annur zilipata Ufadhili wa Matajiri wa CCM...Zote zilikuja Juu.
Ukaja Uchaguzi 1995 Na majimbo haya ambayo timu hizo zipo kwa bahati nzuri yaka chukuliwa na CUF.... Hawa wafadhili wakapata pressure na hatimae wakkaacha kufadhili hizi timu...Hatua Hii haikutarajiwa kabisa na hizi timu waliwaachia hawa wafadhili kila kitu ...hizi Timu zikafa kabisa na kushuka Daraja.. Hili likaleta athari kubwa ya Football Zanzibar. ..Kila Mtu atakubali kuwa hali ya Football zanzibar iko chini sana , imeanguka kweli kweli...Sasa hivi hakuna Small Simba wala Malindi wala Miembeni....Sasa hivi Mpira Zanzibar Unachezwa hivo hivo na Timu za Majeshi. Kuna
Mafunzo
Kmkm
JKU
Na Timu ya CCM Valantia au Green Guards....nao hawachezi mpira ..wanajitoa majasho tu kusukuma siku.

Hivyo Tusifanye Makosa hatua hizi zinaweza kuja angusha kabisa Mpira wa Tanzania. Siasa zetu bado sio zile zilizokomaa sana..
Tujifunze na Kusoma Ilikuwaje Simba..Ikagombana na Hatimae Ikagawanyika na Kuundwa RED STARS
Na ilikuwaje Yanga Ikavurugika na kugawanyika na Kuzaliwa PAN AFRICAN......
Pia someni Historia ya Cosmopolitan. Cosmo Ilikua Timu moja Kongwe zaidi na ilokuwa na ushawishi zaidi ya Simba na Yanga Miaka Ya nyuma. Ilikua na Uhusiano Maalum na Timu Kongwe ya Vikokotoni Zanzibar..Hizi Timu zote zilikua zikiongozwa na Ndugu wawili wa Kizanzibari Mansour Magram alikua Cosmo na Said Magram alikua Kocha wa Vikokotoni. Wakati huo huo Mzanzibari mwengine Abdalla Khalifa Salim ( Kinara) ndie alikua Rais wa Cosmo
Cosmo iliporomoka....Karume hakua anaipenda Vikokotoni Akaziwezesha Simba na Yanga....Cosmo Ikabaki kwenye vitabu vya historia.
Pia tusome Kisa na uhusiano wa Mwalimu na Tabu Mangara ..mara baada ya Ile Mechi Maarufu ya Yanga na Simba Kule Nyamagana Mwanza
Moja ya sababu ya migongano hiii ilikua ni Siasa......

kwa heshima na mtag mwanahistoria maarufu nae kama atatusaidia namna gani siasa ziliathiri maendeleo ya mpira Tanzania.
Mohamed Said

HISTORIA NI MWALIMU MZURI
 
Cha ajabu mwenyekikt yeye na anayeitaka kuikodi yeye mwenyew
 
Kukodi ama kununua his a Mimi huko simo! Ila kuna kila dalili kuwa mambo si sawa ndani ya Yanga: Inawezekanaje Yanga ishindwe kupeleka wawakilishi kwenye semina elekezi ya CAF Kule Cairo hadi Yanga ikose jezi za ushiriki? Na inakuaje ishindwe kufanya usajili wa wachezaji kwa mtandao kwa wakati hadi inajiweka katika hatari ya kushushwa daraja...uzembe huo haukuwahi kutokea nyuma lakini chini ya 'Udikteta' wa Manji yametokea! ....tusubiri.
 
Unyonyaji gani kafanya Manji Yanga? Yanga Ina nini? Zaidi ya kujiendesha kwa hasara? Akili zako umeacha wapi?..........naona umeandika kwa kutumia akili za usiku! Wewe unaona Simba Ina thamani ya Bilioni 20?
 
Ligi kuu ikianza stori zitabadilika. Yetu macho tu.
 


Kama kuna wakati ambacho Yanga SC imetipa raha zaidi tangu Mashabiki wake tuanze kuishabikia basi ni kipindi hiki ambacho Manji amekuwa na mkono wake klabuni.
Mimi pia mkuu,jamaa namkubali sana.
Hizi propaganda wanazoeneza Simba wanataka kutuletea mtafaruku tufulie kama wao.
Wanayanga tufanye yetu,tokea lini Simba wakaitakia mema Yanga?
Manji ni Yanga
Yanga ni Manji
Period
 
Manji ni KUPE. Sijui anataka aendelee kuinyonya Yanga mpaka lini.
 
Mimi pia mkuu,jamaa namkubali sana.
Hizi propaganda wanazoeneza Simba wanataka kutuletea mtafaruku tufulie kama wao.
Wanayanga tufanye yetu,tokea lini Simba wakaitakia mema Yanga?
Manji ni Yanga
Yanga ni Manji
Period
Dada tuache ushabiki, klabu toka lini ikakodishwa?

Kama nia yake nzuri kwa nini asinine timu ?

Ubishi wetu ndio maana tukaletewa umeme wa kukodi tukalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…