Mo aungana na Bakhressa kuichinjia Yanga baharini

Mo aungana na Bakhressa kuichinjia Yanga baharini

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
pic+mo.jpg

WAKATI wanachama wa Yanga wakiwa hawafahamu wanakwenda kujadili kitu gani katika mkutano mkuu wa klabu hiyo keshokutwa Jumamosi, rekodi za bilionea kijana Afrika, Mohammed Dewji zimeibua hofu katika klabu hiyo yenye makao yake makuu katika makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo.

Uchunguzi wa Mwanaspoti umebaini kuwa MO amewahi kuidhamini Simba kwa awamu mbili tofauti ambapo ni kati ya mwaka 1999-2001 na kisha 2001-2004 kipindi ambacho Yanga ilipotea kabisa kabla ya kuja kupata afueni baada ya MO kuondoka.

Katika udhamini wa kwanza wa miaka miwili MO aliwapa Simba sh 900 milioni kabla ya baadaye kutoa Sh 1.5 bilioni katika udhamini wa pili uliomalizika mwaka 2004.

Rekodi zinaonyesha kuwa wakati MO anaingia Simba mwaka 1999, timu hiyo ilikuwa imetoka kukaa miaka minne bila kutwaa taji lolote la Ligi Kuu Bara ambapo ubingwa wao wa mwisho ulikuwa wa Ligi Kuu Bara mwaka 1995, ambapo pia mwaka huo ilitwaa ubingwa wa Kombe la Tanzania (Tanzania Cup).

Katika kipindi cha miaka yake mitano ya udhamini ndani ya Simba, timu hiyo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu wakati watani wao Yanga waliambulia patupu. Simba ilitwaa ubingwa huo mwaka 2001, 2002 na 2004 huku Mtibwa Sugar ikitwaa mara mbili 1999 na 2000.

Katika kipindi hicho Simba ilitwaa pia ubingwa wa Kombe la Tusker mara tatu mwaka 2001, 2002 na 2003 na Kombe la Kagame 2002 ambapo ilikuwa imelikosa tangu mwaka 1996.

Katika kipindi hicho Simba ilitamba Afrika na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia jambo ambalo liliishtua Yanga ambayo ilionekana kumbwelambwela na kupoteza muda tu nchini.

Katika hatua hiyo ya makundi Simba ilikusanya pointi saba ambazo hazijawahi kufikiwa na timu nyingine ya Tanzania ambapo, Yanga mwaka huu mbali na kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ina pointi moja tu mpaka sasa ikiwa imecheza mechi nne.

Hata hivyo, licha ya rekodi hiyo ya kuvutia ya MO bado kumekuwa na hali ya sintofahamu Msimbazi juu ya uwezekano wa kuruhusu bilionea huyo kumiliki asilimia 51 ya hisa ama chini ya hapo kwa hofu ya kuweka maamuzi yote ya klabu katika mikono ya mtu mmoja.

MATAJIRI WAUNGANA

Katika hatua nyingine matajiri Said Salim Bakhresa na Mohammed Dewji ‘MO’ wameonekana kuungana kuongeza nguvu ndani ya Simba huku kila mmoja akipitia njia yake.

Azam ambayo inamilikiwa na Bakhresa imeipa Simba nyota wawili ambao ni kipa Mwadini Ally na straika Ame Ali huku MO Dewji akiipa timu hiyo ya Msimbazi Sh 100 milioni kwaajili ya kufanya usajili.

Mwadini na Ame tayari wametua kambini mjini Morogoro kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Eti Yanga huwa inacheza mpira kwa media. Huu hapa ndiyo ushahidi wenyewe.
 
Kwanza ondoa mafisadi wote. Aviva &co. Wamekula hela sana ya simba....tuweke uongozi mpya lakini sio hawa wapiga ma deal
 
Kwanza ondoa mafisadi wote. Aviva &co. Wamekula hela sana ya simba....tuweke uongozi mpya lakini sio hawa wapiga ma deal
Unadhani Rais wa Club ya Simba SC anachaguliwa kama anavyochaguliwa kiongozi wa standard 3?

Hivi hata haujui kuwa uchaguzi wenu unazingatia katiba....?

Subirini miaka yake 4 iishe kwanza!
 
Kukamatwa kwa Aveva na wenzake ni fitna za yanga baada ya kuona wanazidiwa kete na Simba. Roho mbaya hiyo!
 
Kukamatwa kwa Aveva na wemzake ni fitna za yanga baada ya kuona wanazidiwa kete na Simba. Roho mbaya hiyo!


Sidhani kama Yanga wako desperate kiasi cha kufikia hatua hiyo......!

By the way! Unamaanisha yanga ndio wamemshawishi aveva ahamishe pesa za Okwi kutoka akaunti ya klabu aziweke kwenye akaunti yake binafsi?

Kama ni kweli basi mtakuwa mnaendeleza tamaduni yenu ya kuchagua viongozi V.I.L.A.Z.A....!
 
Kukamatwa kwa Aveva na wemzake ni fitna za yanga baada ya kuona wanazidiwa kete na Simba. Roho mbaya hiyo!



Shutuma kwa Yanga SC kwamba ndio wanawahujumu si kweli....

Mnaanza kujishtukia kwa makosa mliyofanya ya kumruhusu mtu kujipangia thamani ya klabu yenu mpaka akaja na kusema Asilimia 51% ya thamani ya Simba ni Bilioni 20/=Tsh.

Hata hivyo, Sidhani kuwa Uwepo wake huyo MO pale utawafanya Simba SC iwe bora zaidi ya Yanga ndani ya miaka ya hivi karibu.... Sikatai kuwa mtakuwa bora kidogo ila mpaka ifike hatua ya Simba SC kuwa bora zaidi ya mtakuwa mmeshangoja sana tena kwa kipindi kirefu mno....

Si mnajua kuwa watz si wavumilivu? Hapo ndipo mtaanza kujiuliza umuhimu wa huyo jamaa wenu hapo klabuni ikiwa mtashindwa kuwa bora zaidi ya hao Yanga SC kwa kipindi cha muda mfupi.....

Nasema kuwa mtasubiri kutokana na mipango ya mtani wenu pia! Msifikiri pale ndio wamemaliza.... La hasha, bado.

Unajua nini kitatokea MKUTANONI?.... Ahhhahh
 
Heheh tambo za wamatopeni,na mwaka huu mtaendelea kupanda fastjet tu kwenda mbeya
 
Ndiyo zao hao wamatopeni. Wameanza kutoa dozi kwa vitimu vya mchangani wakaanza kuchonga. Ghafla wamekwaa kisiki huko mchangani na kelele zimeisha
Hivi ilikuwaje kile kisiki, siku hizi niko mbali sana na vyombo vya habari.
 
Nawaambia Yanga mwaka huu mtafute chaka la kujificha. Spidi ya Mo hamtaiweza.
 
Back
Top Bottom