Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Anaandika Mo Dewji:-Leo nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa: Uwanja wa Benjamin William Mkapa.
Amesema Itakuwa ni heshima kubwa kama uwanja wetu pendwa utaitwa jina la Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Tunamuomba Rais John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya Hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa na hasa kwa vizazi vijavyo.
Tunawaomba Watanzania wote bila kujali ushabiki wa klabu muunge mkono kwa kuweka sahihi ili tumuombe Mhe Rais kubadilisha jina la uwanja huo uitwe Benjamin William Mkapa Stad.
Ujenzi wa Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ni miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa.
Uwanja huo kwa namna mmoja au nyingine umesaidia kuendeleza mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania. Uzuri na ukubwa wa soka letu umedhihirishwa kwa sababu ya uwanja wetu huo ambao unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa Afrika.