Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji 'MO' leo Julai 27, 2019 amefafanua kuhusu uwekezaji kwenye Klabu ya Simba SC huku akiwahakikishia wanachama na mashabiki kuwepo kwake kunako Klabu ya Simba SC.
"Nimesikitishwa na mijadala mitandaoni ya kumshutumu Waziri Mwakyembe kwamba ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa, Ndugu zangu si kweli Utaratibu huo upo tangu 2017 kisheria na sisi Simba tulikubali.
Waziri Mwakyembe alituruhusu sisi tuendelee na mwekezaji mmoja. Ndugu zangu Wanasimba mimi nipo na niko na nyinyi siendi popote.
Na sasa tushazungumza na Serikali na mazungumzo mazuri. Nawasihi wanasimba wote twendeni tukaishangilie timu ya Taifa na tukutane Simba Day tarehe 6.
Tulianza vizuri na Serikali na tutamaliza vizuri na Serikali"
•••Ameandika MO kwenye ukurasa wake wa Twitter