Mo Dewji ameonyesha sura yake halisi,wanasimba tutarajie u-Dictator Mo akishakabidhiwa Hisa

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Tumeshuhudia juzi tu mfanyabiashara Mohammed Dewji akipitishwa kama mwekezaji atakayepatiwa Hisa 49% za klabu hivyo kuwa mwanachama mwenye hisa nyingi.


Lakini kabla hata hajakabidhiwa timu rasmi tayari tumeshuhudia na kuona sura Halisi ya Mo

1.Kauli aliyotoa Jana Mo kupitia ukurasa wake wa Twitter imeonyesha chembe chembe za u-Dictator ,hapo bado hajaanza kazi rasmi je akianza si ataonea wafanyakazi wa klabu ,


2.Wafanyakazi wa klabu ya simba watakuwa na uoga na furaha kuwaondoka sababu bosi mkuu akikasirika basi ataweza kuwaadabisha na kuwadhalilisha kupitia mitandao ya kijamii

3.Mwalimu Omog kateleza mechi moja lakini mwanahisa huyu kaamua kumtolea povu kupitia Twitter na haikupita masaa 3 viongozi walioshika hatamu simba wakajawa na hofu na kuamua kumtimua mwalimu

Hapa Dewji hajakabidhiwa rasmi Hisa na kuanza kufanya kazi tayari tumeshaona sura yake je akikabidhiwa Hisa si itakuwa hapatoshi hapa mitaa ya msimbazi
 
Huyu Omog alikuablia na zacharia kuwa kila mwezi atamkatia million 2 kutoka kwenye mshahara wake.Sasa huyu omog hatekelezi walichokubaliana wakatai anamuajili hivyo basi wachezaji waliambia wahahakikishe OMOG anashindwa ili atimuliwe.Kwakweli wamefanikiwa
 
Unaanzaje kua billionea bila maamuzi magumu nchi kama Tanzania....acha tu atusomeshe namba timu yetu ilishaprove failure kwa kua kijiwe cha wapigaji...sasa ianze endeshwa kitaaluma huwezi kua meneja wa Kiwanda na kama hujafikia lengo ni kuachia ngazi tu
 
Sema nyie majamaa mna ujasiri, yaani timu inaongoza ligi halafu mna timu kocha?
 

Hii ni habari njema sana na ndilo jambo simba inalolihitaji kwa muda mrefu. Timu inapokuwa kampuni ni ndoto ya mwenye kampuni ndio inayofuatwa na sio ya mfanyakazi wa kampuni wala mkereketwa yoyote yule. Na mpaka sasa ni ndo ya mwenye stake kubwa ndio ya ukweli. Hivyo vitu vidogo vidogo sio vya kumzuia mtu anayetaka kuipeleka kampuni kwenye viwango vya juu. Kama kuna haki zinakiukwa mahakama ziko za kuishtaki kampuni. Asante sana kwa taarifa. Simba oyeeeee
 
Upo udikteta WA Aina nyingi tu lakni udikteta WA kataka maendeleo huo ni udikteta mzuri. Wazungu wana udikteta wa kataka taratibu zifuatwe ndie mn wanaendelea Sana. Tofauti na sisi tunapenda maendeleo lkn Siri ya maendeleo hatujui. Tunapenda maneno ya kwenye kahawa tu yn majungu. Nampongeza mo kwa kutomungunya maneno. Omog alikuwa hawezi panga timu. Muda wote Omog hakuwa na timu ya kwanza alikuwa anabahatisha muda wote
 
Kuna wachache hawakukubali Dewji kuchukua timu, hivyobinaeleweka!!
Mo anaenda ijenga simba, wewe ni eidha mwanayanga au mmoja wa wachache waliompinha Dewji. Ni kawaida.
Na awe dictotor tu, hatutaki mazoea mazoea. Kama anawalipa wachezaji vizuri ni wajibu wao kudeliva, uongozi pia.
 
Mleta uzi unamfahamu Abromovic au Perez ambavyo hawana utani na makocha huoni ubabe wao ndo unawaletea mafanikio kwenye klabu zao
 
Unamzungumzia Zacharia Hanspope ama zakaria yupi.kam ni hanspope basi unakichaa.jamaa katoma kunu nua petrol station kwa bilioni mbili juzi kati tu atakuwa na shida ya kula ganji kwenye mshahara wa kocha?
 
Unajua maana ya udictetor au unaendeshwa n.a. miemko n.a. fikra finyu ya kukariri udictetor. Meanwhile maendeleo ya tanzania yanahitaji maamuzi magumu ili n.a. ninyi mnaoishi kwa kukariri muelewe kuwa maendeleo ili yaje yanahitaji maamuzi
 
Acheni kuongea vitu ambavyo havina mantiki mo ana wafanyakazi wangapi kwenye makampuni yake kuna siku ulisikia kawazalilisha kwenye mitandao ya kijamii au kwenye vombo vya habari tatizo ni kocha hakuna mwana simba asiyelitambua ilo tumemfukuza tunatalajia simba ss itaimalika
 
Sijaona tofauti kubwa ya Falsafa (Kiuongozi) kati ya Dogo (Mo) na Kiongozi kutoka Korea ya kaskazini Dogo (Kim)

Wote hawa wanasukumwa/wanaendeshwa zaidi na ngunvu za UMIMI..!

Kwa mwanzo huu wana Simba (japo mimi Yanga Damu) mtarajie kuongozwa KIDIKITETA.

Poleni watani zangu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…