Elections 2010 Mo Dewji apita bila kupingwa!

Status
Not open for further replies.

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Habari nilizozipata muda mfupi uliopita zinadai Mhe. Mohammed Dewji mbunge wa Singida Mjini ameshinda kesi iliyokuwa imefunguliwa na wapinzani wake na yeye kuwashinda katika pingamizi alilowawekea hivyo kubakia pekee kwenye kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge kwa jimbo hilo, hIi inamaanisha njia ni nyeupe kurejea mjengoni. Habari zaidi tutapeana kadiri muda unavyosonga

==============
LATEST:

22 Aug, 2010

Kwa mujibu wa Dr. Slaa, CHADEMA wamekata rufaa kwa kushirikiana na CUF dhidi ya Mo, hivyo mpaka rufaa isikilizwe au itupiliwe mbali ndipo itakuwa rasmi kuwa Mo hana mpinzani.
 
Je wagombea ( hasa wa upinnzani) wanajua haki zao chini ya sheria ya uchaguzi endapo pingamizi dhidi yao zinakubaliwa na wao kuenguliwa? Vyama vimejipanga vipi kukabiliana na hali hii? Tutazidi kushangaa.
 
sasa wabunge wa chama tawala wafikia wangapi? ambao ni sawa na asilimia ngapi?
 
Wait a minute! Yaani hao wote wagombea wa upinzani wameenguliwa kutokana na pingamizi lake Mo? Yaani pingamizi dhidi yake limetupwa na lake dhidi ya hao wapinzani wake limekubaliwa?

Takukuru -- fuatilieni account za hawa ma-returning officers!
 
Kimsingi huyu panchoro ni fisadi mkubwa..... ngoja kuna issues zake zinafuatiliwa na watu waliodhamiria kuikomboa Tanzania. Siku yake itafika atakapolia na kusaga meno.
 
Kimsingi huyu panchoro ni fisadi mkubwa..... ngoja kuna issues zake zinafuatiliwa na watu waliodhamiria kuikomboa Tanzania. Siku yake itafika atakapolia na kusaga meno.

Nyerere aliwahi kumtia ndani baba yake kwa kuficha bidhaa. Nyerere alikuwa hatetemeki mbele ya hawa gabachori! Mwafrika alikuwa na heshima kubwa siku zile!
 
Ngoma imeanza tusipoangalia tutabaki na Dr.Slaa na Mbowe .........!
 
Ngoma imeanza tusipoangalia tutabaki na Dr.Slaa na Mbowe .........!

Yeah -- imeanza. Hawa ma kada wa CCM, sorry ma-returning officers na NEC yao kweli wameanza kazi. Ni katika kile kinachoitwa ushindi wa kishindo. Wanaona bora waanzie mezani kwanza.

Kule kwa Pinda nasikia wagombea wa upinzani walikatazwa na vyama vyao kurudisha form. Wadau, chunguzeni hili na mwenye taarifa kamili atujuze.
 
Mkuu kama nimekusoma vizuri unasema kwamba baada ya kushinda kesi hiyo hakuna wagombea wa Upinzani kabisa au au unazungmzia mwakilishi wa CCM Singida hana upinzani tena toka ndani ya chama.

Usitake kunambia hata Singida Mjini vyama vya Upinzani vimeshindwa kusimammisha mgombea, mkoa ambao umeachwa nyuma kuliko mikoa yoite Tanzania tunashindwa kuweka mwakilishi jamani? eeeeh yaani kweli tunawajali wananchi au huu ni mchezo wa kuigiza!
 
wapinzani wamesimamisha watu (chadema + cuf) bali mo kawawekea pingamizi wote wawili na pingamizi lake limekubaliwa
initially hawa jamaa wa upinzani walimwekea mo pingamizi lakini halikupita
 
Naona ccm imeamua kutumia all the dirty tricks available and some more!

Upinzani ungeungana huenda asaa ingesaidia......lkn kwa chama kimoja kimoja tabu.......
 
Kimsingi huyu panchoro ni fisadi mkubwa..... ngoja kuna issues zake zinafuatiliwa na watu waliodhamiria kuikomboa Tanzania. Siku yake itafika atakapolia na kusaga meno.

Mkuu Macho_mdiliko si kila mtu mweupe (Mhindi) ni fisadi.... japo pia kila binadamu anaq udhaifu wake. Ukimlinganisha huyu jamaa na wenzake anajitahidi sana kuukimbia ufisadi, mengine ni matatizo yetu sisi Wazalendo kulazimisha kupewa vijizawadi na hiyo inamfanya mtu atumie akili sana hata kutoa hiyo misaada hasa kwa watendaji na wanasiasa wetu ili kuepuka mitego. Angekuwa ametumia fedha hata hao wapinzani wasingeweka pingamizi na pengine wasingeudisha hata fomu kwa ninavyoijua Singida.
 
wapinzani wamesimamisha watu (chadema + cuf) bali mo kawawekea pingamizi wote wawili na pingamizi lake limekubaliwa
initially hawa jamaa wa upinzani walimwekea mo pingamizi lakini halikupita
Aaaah! siasa za Bongo hata sina hamu nazo..
 
Aaaah! siasa za Bongo hata sina hamu nazo..

Kaka Mkandara pole sana. Watanzania wanapelekwa na upepo hakuna mawazo binafsi, muda si mrefu watakuwa wanaburuzwa na miziki ya kina Komba na Vicky Kamata
 
Aaaah! siasa za Bongo hata sina hamu nazo..

Pole Mkandara these are Tanzania Politics na huu ni Mwanzo naamini mpaka tar 31 NEC watakuwa wameshawazawadia CCM viti zaidi ya 50
 
Kaka Mkandara pole sana. Watanzania wanapelekwa na upepo hakuna mawazo binafsi, muda si mrefu watakuwa wanaburuzwa na miziki ya kina Komba na Vicky Kamata

Bila ya kuwasahau Orijino Komedi Ha ha haaa...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…