Ni kweli kuwa Lau Masha,william Ngeleja na Nimrod Mkono,Prof Mwakyusa na Prof Mwandosya nao wamepita bila kupingwa na kufanya CCM hadi sasa iwe na wabunge zaidi ya 17 wa kuchaguliwa waliopita bila kupingwa?
Nihabarisheni tafadhali maana kama kweli sio jambo zuri hata kidogo kwa wana mageuzi maana hawa waliopita bila kupingwa watatumwa kwenye majimbo korofi ili kuongeza nguvu ya CCM!
Iweje basi CHADEMA isipate hata jimbo moja bila kupingwa likiwepo lile la Nzega na ZNZ kwa Masauni ambalo ni wazi ksbisa wagombea wa CCM walidanganya kwenye hati zao za viapo?
CHADEMA makao makuu wamejipanga vipi kuhakikisha majimbo kama Singida ambayo wagombea wao walienguliwa kufanya warudishwe kwenye mchakato wa uchaguzi huu?
Ni kweli Mkuu mpaka sasa ni Wabunge 18 wa CCM ndio hawana wapinzani katika Majimbo yao,Wabunge hao ni.
1;Anne Makinda (Njombe kusini)
2;William Lukuvi (Ismani)
3;Celina Kombani (Ulanga Mashariki)
4;Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki)
5;Christopher Ole Sendeka (Simanjiro)
6;William Ngereja (Sengerema)
7;January Makamba (Bumbuli)
8;Deo Filikunjombe (Ludewa)
9;Job Ndugai (Kongwa)
10;Philip Mulugo (Songwe)
11;Gregory Teu (Mpwapwa)
13;Nimrod Mkono (Musoma Vijijini)
14;Lau Masha (Nyamagana)
15;Mohammed Dewji (Singida Mjini)
16;Prof.Anna Tibaijuka (Muleba)
17;Prof.David Mwakyusa (Rungwe Magharibi))
18;Prof. Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki)
Chadema Wamesimamisha Wabunge katika Majimbo
167 kati ya majimbo 239.