Mo Dewji kuichukua Simba baada ya miezi mitatu, leo atoa 100 Mil za usajili

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Nachukua nafasi hii kumshukuru Dewji kwa kukamilisha ahadi yake na pili kuchangia pesa za usajili - AVEVA

Zimebakia siku chache za usajili na tunatakiwa tulipe Milioni 420 za usajili - AVEVA

Sasa tunaweza kusajili wachezaji na tutatoka kifua mbele - AVEVA

Kupata pesa hizi tunaweza kutamba kwa kupata pesa kutoka kwa Dewji - AVEVA

Tunatoa rai kwa mashabiki wengine kujitoa kama Dewji na sasa tumebaki na hitaji la kama Milioni 300 za usajili - AVEVA

Mchezaji huyo ni Fredrick Blagnon kutoka Ivory Coast. Hakuna makubaliano yoyote ni ahadi niliyoitoa kama shabiki - AVEVA

Mimi sijapinga mabadiliko na mimi ndiyo niliunda kamati. Mabadiliko yapo na mimi kama rais wa Simba naahidi mchakato wa mabadiliko utafanyika, Hili jambo haliwezi kukamilika kwa muda mfupi itachukua muda haiwezi iwe imebakia siku tano ndiyo jambo likamilike.

Nilitaka mchakato ukamilike miezi mitatu iliyopita tutume maskauti kutafuta wachezaji bora Afrika. Simba inawanachama wengi watajitoa watasaidia tutasajili na kuna makampuni tunaongea nao - AVEVA

Swala la mabadiliko ya Simba likipita bajeti itakuwa zaidi ya Bilioni
 
Mabadiliko simba hayaepukiki.. ilikuwa lazima wakubali tu.
 
Kwa hili.. Naweka akiba ya maneno.
 
Mpira wetu bhana! Kama siasa..

Wacha tu niendelee kutazama la liga.. Hata tambwe siku hizi sijui yuko timu gani! Sijui kashahama, sijui yuko Ruvu shooting... arrrrgh
 
Hongera,angetoa hizo 300 kabisa ili tufanye vyema.Hasa viungo na washambuliaji.
 
Sasa yanga si watu wakupigwa siku zote yaani garasa kama chirwa unamnunua vipi 200 ml.
Hamuwezi kujadili magonjwa yenu bila Yanga eti?

Siku zote tunawalalia...
Chuji
Twite
Yondani
Kessy
Ngassa
Tambwe
Na bado, kwenye ligi mmetupa...mmetupa tena. Garasa ni lile mlilochukua kwetu...Kiiza

Mwambieni huyo moo awape hela haraka mnenepe, ligi inapoanza mtuchangie tena points 6 na magoli ma4 twende airport
 
Sasa yanga si watu wakupigwa siku zote yaani garasa kama chirwa unamnunua vipi 200 ml.
Unampima Chirwa garasa kwa mechi 3 alizocheza bila kuangalia historia yake ya nyuma...

Hata Donald Ngoma mlisema ni garasa...

Sasa hizo Milioni 100 sijui mtasajili wachezaji wangapi wa Kimataifa?
 
Simba Mshachumbiwa hvo....bdo 19,900,000,000
Mumpe 51% yake
 
Mwisho wenu umefika.. zile 5 zitarejea tena maana hata bajeti yenu ya mwaka kwa msimbazi mara mbili..! hivyo tabia yenu ya kupora akina Twite ndo hivyo tena
 
Unampima Chirwa garasa kwa mechi 3 alizocheza bila kuangalia historia yake ya nyuma...

Hata Donald Ngoma mlisema ni garasa...

Sasa hizo Milioni 100 sijui mtasajili wachezaji wangapi wa Kimataifa?
Simba inatulia katika usajili wewe.. hizo 100 utaona matunda yake

Au nikumbushe kwa Okwi na Samatta tulitumia kiasi gani kusajili..!?
 
Unampima Chirwa garasa kwa mechi 3 alizocheza bila kuangalia historia yake ya nyuma...

Hata Donald Ngoma mlisema ni garasa...

Sasa hizo Milioni 100 sijui mtasajili wachezaji wangapi wa Kimataifa?

Mchezaji bora anapimwa hata kwa mechi moja, huyo wa kwenu anataka acheze games ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…