Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Leo Mo Dewji ametangaza kumteua Bw. Magori kuendelea kuwa mshauri wake kwenye masuala ya michezo, ni jambo jema sana kwa sababu Magori ni mmoja wa wana Simba wenye mchango mkubwa sana tangu akiwa NSSF.
Hata hivyo, tangu amteue Bw. Magori hajajibu kwenye post yake Instagram kushukuru kwa uteuzi na kuahidi kumsaidia mwekezaji huyo mwenye utata mwingi kwenye transformation ya Simba.
Kwa desturi zetu waungwana, ukiteuliwa lazima ushukuru. Baada ya Mo Dewji kumteua, nimepita kwenye kurasa ya Insta ya Bw. Magori zaidi ya mara 10, sioni shukrani yoyote kana kwamba hajui kilichotokea.
Sisi wadadavuzi wa mambo tunajua Magori hajakubali uteuzi huo na hivyo mgogoro ndani ya Simba bado haujapoa.
Magori inadaiwa alifanyiwa vitendo vya hovyo wakati wa mchezo baina ya Simba na Raja. Watu waliona akizuiwa kuingia uwanjani bila sababu.
Inadaiwa Magori hakumuunga mkono Mangungu wakati wa uchaguzi na ndio sababu hadi sasa hajapost kukubali uteuzi wa Mo Dewji.
Mo Dewji anampenda Murtaza Mangungu, wakati Magori na wenzake baadhi wa Friends of Simba wanaona kwa Mangungu hatutoboi. Sasa anawezaje kukubali kukufanya kazi na mtu ambaye anadhani hawezi kuifikisha Simba ilipo?
Lingine, walioshinda uchaguzi wamewatukana sana akina Magori na wenzake na hadi hawajaomba radhi.
Lingine, wajumbe aliowateua Mo Dewji kwenye bodi sio watu wa mpira, ni wanasiasa tu wanaokwenda kutangaza biashara ya Mo Energy.
Mimi ni mnyama, lakini nawahakikishia, tusipoweka silaha chini, hatumfungi Vipers wala Horoya. Period.