Mo Dewji, nakujulisha kuwa Crecentius Magori hajakubali uteuzi wako wa kuwa mshauri wake, vita bado mbichi hii

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Leo Mo Dewji ametangaza kumteua Bw. Magori kuendelea kuwa mshauri wake kwenye masuala ya michezo, ni jambo jema sana kwa sababu Magori ni mmoja wa wana Simba wenye mchango mkubwa sana tangu akiwa NSSF.

Hata hivyo, tangu amteue Bw. Magori hajajibu kwenye post yake Instagram kushukuru kwa uteuzi na kuahidi kumsaidia mwekezaji huyo mwenye utata mwingi kwenye transformation ya Simba.

Kwa desturi zetu waungwana, ukiteuliwa lazima ushukuru. Baada ya Mo Dewji kumteua, nimepita kwenye kurasa ya Insta ya Bw. Magori zaidi ya mara 10, sioni shukrani yoyote kana kwamba hajui kilichotokea.

Sisi wadadavuzi wa mambo tunajua Magori hajakubali uteuzi huo na hivyo mgogoro ndani ya Simba bado haujapoa.

Magori inadaiwa alifanyiwa vitendo vya hovyo wakati wa mchezo baina ya Simba na Raja. Watu waliona akizuiwa kuingia uwanjani bila sababu.

Inadaiwa Magori hakumuunga mkono Mangungu wakati wa uchaguzi na ndio sababu hadi sasa hajapost kukubali uteuzi wa Mo Dewji.

Mo Dewji anampenda Murtaza Mangungu, wakati Magori na wenzake baadhi wa Friends of Simba wanaona kwa Mangungu hatutoboi. Sasa anawezaje kukubali kukufanya kazi na mtu ambaye anadhani hawezi kuifikisha Simba ilipo?

Lingine, walioshinda uchaguzi wamewatukana sana akina Magori na wenzake na hadi hawajaomba radhi.

Lingine, wajumbe aliowateua Mo Dewji kwenye bodi sio watu wa mpira, ni wanasiasa tu wanaokwenda kutangaza biashara ya Mo Energy.

Mimi ni mnyama, lakini nawahakikishia, tusipoweka silaha chini, hatumfungi Vipers wala Horoya. Period.
 
Wote wapigaji, Magori mpigaji, Mangungu mpigaji, Mo anaitumia Simba kunawirisha biashara zake ukifika wakati wa usajili anazoa wachezaji manyanyantore wa bei poa wasio na uwezo.

chini ya uongozi wa Mangungu Simba haitokuja imfunge Yanga abadan.
 
Hivi atamteua bila kuongea naye?
 
Nyie endeleeni kukumbatia majungu na unafiki yanga itaendelea kuwapasua mpaka akili ziwakae sawa, Ni timu ipi inamilikiwa na mhindi na inafanya vizuri tuambiane hapa
 
Ikitokea akaukubali uteuzi utaufuta huu Uzi?
 
New ID ya jamaa yetu😂😂
 
Shida Yako unaamini maisha ya kwenye mitandao wale ni viongozi wanafahamu kipi Cha kuweka public na kipi sio hivyo kama je?. Magori amekutana na MO akamshukuru kwa ilo je wewe unataka Nini uku jf.
 
Shida Yako unaamini maisha ya kwenye mitandao wale ni viongozi wanafahamu kipi Cha kuweka public na kipi sio hivyo kama je?. Magori amekutana na MO akamshukuru kwa ilo je wewe unataka Nini uku jf.
 
Shida Yako unaamini maisha ya kwenye mitandao wale ni viongozi wanafahamu kipi Cha kuweka public na kipi sio hivyo kama je?. Magori amekutana na MO akamshukuru kwa ilo je wewe unataka Nini uku jf.

Umeimaliza. Jamaa anaamini kila jambo lazima alisome kwenye mitandao.
 
Kwamba siku hizi ukiteuliwa na tangazo likawekwa Instagram au Facebook unatakiwa kuja kujibu hiyo post ndio ionekane umekubali uteuzi? Maajau hayaishi nchi hii, umejipa muda kufatilia kuwa ndugu Magori amepokea barua ya uteuzi au laa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…