Mo Dewji toa billion 20 ambazo zipo kimkataba, acha kutengeneza mazingira ya kuonewa huruma na ujanja ujanja

Sasa hapo miaka mitatu anafanya nini wakati mkataba bado?? Elewa kwanza😁😁
Nielewe nin mkuu? Mo ni mwanachama halali wasimba yupo hapo kama ambavyo wanasimba wengine wanavyoweza kuwepo. Kwan katiba ya simba inasemaje mkuu?!
 
Pesa gani sasa wakati wao tayari wana klabu yenye thamani, hivyo wanatoa sehemu ya klabu kwenda kwa Mo kwa 20 billion, sasa waweke pesa gan tena
Hivi unajua maana ya hisa au umeendika kujaza saver ya JF mkuu 😁😁
 
Hisa ni unapewa sehemu ya umiliki, kama mimi namiliki gari, halafu nakuuzia wewe sehemu ya umiliki kwamba tunamiliki kwa ubia, mimi nitoe pesa ya nini tena?
Hivi unajua unacho kizungumza mkuu, hebu rejea kwenye maelezo juu ya mchakato wa mabadiriko ya klabu. Mali ni dhamana kwenye uwekezaji. Ndio maana upande wa simba hisa zake zitagawanywa na kuuzwa kulingana na thamani ya klabu, pesa hiyo itakayo patikana itakuwa sehemu moja na ile ya upande wa mwekezaji mwenye hisa 49%. Kiufupi hisa ni umiliki unaokupa wajibu wakuchangia mtaji kwenye sekta ya biashara na faida itakayo patikana hugawanywa kwa wanahisa
 
Kwani memorandum of understanding, ilikuwa inasemaje? Kwa kukusaidia ilikuwa inasema kuwa muwekezaje ataweka hiyo bilioni 20,kwenye escrow account ndani ya miezi mitatu tu!! Tukubali huu uwekezaji una tatizo, tusiendeshwe na ushabiki, na changamoto nyingi zinaweza zikawa ni za mfumo uliokuwepo sasa kuuunganisha, ndio shida ipo hapo, ndio maana sasa unaona simba inaendeshwa kana kwamba mchakato umeshakamilika wote!!
 
Mimi siufahamu huo mkataba wala unachosema, nimeongelea concept ya hisa objectively; sasa kama huo mkataba unamtaka hadi mmiliki wa awali wa 100% ambae sasa amegawa sehemu ya mali yake kwa Mo at a fee ya 20billion na bado yeye tena anatakiwa atoempesa basi huo mkataba ni wa Kifisadi, uchunguzwe.
 
Hiyo B20 sielewagi walikubaliana kutoa yote kwa mkupuo au kwa awamu, maana MO alisema anatoa kwa awamu sasa nani yupo sahihi, utopolo tuacheni tukawatafutie viti maalum vya club bingwa
 
Si bure utakuwa una uhusiano na Amsterdam 😂 😂 😅

Everyday is Saturday................................😎
 
Nielewe nin mkuu? Mo ni mwanachama halali wasimba yupo hapo kama ambavyo wanasimba wengine wanavyoweza kuwepo. Kwan katiba ya simba inasemaje mkuu?!
Kuwa mwanachama halali sio sababu ya kutaka kufanya mambo bila kufuata utaribu, sababu za vilabu vya ulaya kuwa na ukwasi mkubwa huu utapeli unaofanywa na mo dewji walishauacha mda sana
 
Labda unisaidie kitu kimoja, juzi MO alinukuliwa akisema kwamba thamani ya hisa zitakazo uzwa kwa wanachama wa simba ni sh mil 400 kwa hisa 1%, so kwa logic yako hapo juu fedha za mauzo ya hizo hisa zinatofauti gani na b 20 za Mo kwenye uwekezaji kwa Simba sc?
 
Kuwa mwanachama halali sio sababu ya kutaka kufanya mambo bila kufuata utaribu, sababu za vilabu vya ulaya kuwa na ukwasi mkubwa huu utapeli unaofanywa na mo dewji walishauacha mda sana
Utaratibu gan huo mkuu?
 
Amini nakuambia mashabiki wa izi timu wanataka ushindi tu......hayo mengine hayawahusu
 
Mo aliahidi kwa kinywa chake atatoa bill 20 ikaweka kwenye mkataba, Leo anaambiwa atimize takwa la kimkataba anakua mbogo, alafu Cha ajabu mashabiki Kama wewe wamesha shahau tukio la 2017 ajabu sana
 
Amini nakuambia mashabiki wa izi timu wanataka ushindi tu......hayo mengine hayawahusu
Ndo hao hao mashabiki wanaenda kuwa viongozi wa hizo timu za mpira, ndo maana timu Zina miaka 80 viwanja havina, na mpira wetu kuendelea inakua ni ngumu sana
 
Landa unifahamishe, Simba SC kabla ya kutaka kugawa hisa zake kwa kuuza, ilikuwa inamilikiwa na nani?
 
Eti thank you for guidance on simbas development Pique ndo mtoa guidance hahahaha jamaa anawajulia sana hawa mambumbumbu yaaani kila akiambiwa atoe bil 20 yeye anakuja na kituko
 
Eti thank you for guidance on simbas development Pique ndo mtoa guidance hahahaha jamaa anawajulia sana hawa mambumbumbu yaaani kila akiambiwa atoe bil 20 yeye anakuja na kituko
Ni Msanii sana, balaa aongee na kina Daniel levy, au Ed Woodward unaongea na pique ambaye ana zero knowledge kwenye management jamaa ni mjanja mjanja sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…