Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Mohammed Dewji 'MO' ameguswa na hali ya sintofahamu inayoendelea kwenye klabu ya Yanga na kuwaombea waweze kupita katika kipindi hicho kigumu kwao huku akiwataka watulie kisha waungane upya.
MO kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kwamba "Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba. Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulia na waungane upya". Ameandika MO Dewji.
View attachment 816384