MO & Manara Shida sio mashabiki, timu ni mbovu sana

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,292
Reaction score
7,867
Mimi ni shabiki wa yanga a.k.a ombaomba, vyura fc na majina mengine mengi mnyotuita ila ndo nipo huko. Niliiona press yako Bw Mohammed na nimeona posts zako Manara kule insta. Wote mnomba mashabiki wafike kwa wingi uwanjani ili kuisapoti timu imuue mwarabu. Ni rahisi kwa viongozi kufanya hivyo lakini kiuhalisia timu yenu ni mbovu sana.

Mechi ya mwisho mmecheza na mwadui na kushinda 3-0, lakini kwa forward ya Boko ile hapana kwakwel. Yaani timu labda kiungo ila beki mbovu, forward mbovu, mfumo mbovu, yaani kocha mfumo wake ni mmoja tu bila kujali yupo ugenini au nyumbani, amefungwa au amefunga, timu kubwa au ndogo.

Mashabiki wa All ahly walikuwa 10,000 tu lakini shangwe lao ndio lile la simba day pale taifa. Mashabiki wa kibongo wanashangilia pass, chenga na magoli. Mkifungwa tu ndo watu kuzimia, kujikunyata na wengine kuondoka uwanjani tofauti na wenzetu.

Ukweli mchungu ni kuwa kwa Simba hii hata uweke kiingilio 500 kuna watu hawatakuja kisa waliitwa watumia Tecno za 70,000 jambo ambalo ni la kipuuzi kabisa.

Niwatakie maandalizi mema na walau mtoe sare tu sio mbaya. Sisi tunaendelea kubahatisha huku ligi kuu maana kwa mwendo tunaoenda nao mh! hatuwezi kuchekana.

Barafu la moto
 
Nimesikitishwa na Muheshimiwa Spika na Rage..kutaka mechi ichezwe saa nane mchana...CAF wamesikia na kukataza..
 
kwa hatua ya makundi simba aliyofikia kajitahidi sana.. ila hapo ndipo mwisho wa kujitahidi.. mashindano ya caf hatua zinazofata ni ya timu zile zile miaka yote.. timu zinazojua zinachofanya ndizo zinabaki tu... simba hata wacheze 20 hawawezi kufika hatua zaidi ya hapo...


mo dewji na manji sio mashabiki wa simba wala wa yanga.. ni wajanja wajanja tu wanaotumia hizi timu kujinufaisha wao...

manara siwezi mlaumu sababu yeye anatafuta ugali tu wa familia yake.. so lazima awe mjanja mjanja
 
Hatua ya makundi ni 16 bora. maana yake ushinde mechi mbili tu.
Yanga ilikuwa 16 bora 2016.
 
Hatua ya makundi ni 16 bora. maana yake ushinde mechi mbili tu.
Yanga ilikuwa 16 bora 2016.

yes ndio level zetu sisi timu ndogo ndogo.... kuanzia robo huko mpaka ubingwa ni timu ambazo ni brand tu africa
 
Kwa nini unateseka na ya simba wakati wewe yanga?
 
Reactions: Tui
Write your reply...Vp kuhusu chelsea na yo ni mbovu waliofungwa gori sita ? sasa kma simba mbovu timu ipi nzur ambayo haifungwi kaz kuleta ushabiki usio na maana tu
 
Sasa bro ulitaka Manji na Mo waendeshe hizi timu bila wao kunufaika?! We ungeweza?!
 
Nimesikitishwa na Muheshimiwa Spika na Rage..kutaka mechi ichezwe saa nane mchana...CAF wamesikia na kukataza..
Spika alikosea sana lile swala kulizungumza bungeni tena kwa namna ile
 
Underpaka wabishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…