WAR
Member
- Dec 16, 2016
- 49
- 36
Kipindi cha nyuma tulipozungumzia ubunge tulipata picha ya mtu fulani mwenye umri mkubwa pamoja na hela za kutosha. Wabunge wengi walichaguliwa kwa sababu ya kununua kura kutoka kwa wapiga kura. Wenye nguvu ya pesa ndio walikuwa wana asilimia kubwa ya kuwa viongozi hata kama hawana karama ya uongozi hii iliwanyima vijana wengi fursa ya kuweza kupata nafasi ya kuwa viongozi kwa asilimia kubwa.
Leo hii natoa pongezi za dhati kwa Rais wetu Dr John P Magufuli kwa kuichukua rushwa pamoja na kuwaamini vijana katika nafasi za uongozi ndio maana tuliona wakati analivunja bunge hakusita kusisitiza kuwa atapenda zaidi kuona wanapata vijana wengi bungeni. Hii tafsiri yake ni kuwa Rais ni mtu wa kazi tu anahitaji watu ambao akili yao inafanya kazi kwa haraka na watakaoweza kwenda na kasi yake ya kuleta mabadiliko katika nchi hii.
Ninachoamini Mlimwengu akipata nafasi ya kupewa ridhaa na wana Muleba Kaskazini watakuwa wampempata mtu sahihi. Ingawa jamii nyingi za kiafrika zimekuwa na imani ndogo na vijana katika nafasi za uongozi. Ni wakati mwafaka wa wananchi kubadilisha mindset zao na kuwaamini vijana ambao kwa sasa ni taifa la leo siyo la kesho kama tulivyozoea.
Mlimwengu tumesoma wote Udom nakujua misimamo yako na fikra zako chanya tangu kipindi kile ukiwa waziri wa Michezo na burudani nadhani ni wakati ambao wanamichezo wengi walifurahia uongozi wako. Hata baada ya kumaliza chuo hukusita kuwa mwanaharakati kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii. Nimefurahi sana kuona nawe ni mtia nia wa nafasi ya ubunge. I wish watu wangekupatia nafasi ukapate kutafsiri ndoto zako katika utendaji halisi.
Ninachokushauri hata usipopata nafasi ya ubunge usikate tama wewe ni kiongozi wa kipekee ingawa wengi huwa wanapenda ucheshi wako na utani wako lakini linapokuja suala la usiriasi huwa unamanishaa. Wewe bado ni kijana na wala siongei maneno hayo kukatisha tama kwamba unaenda kufeli hapana ila naomba ukubaliane na kitakachotokea ingawa mimi nina imani uwezo wako mkubwa na utaenda kushinda.
Wewe siyo mwoga katika kuwakilisha mawazo na strength yako kubwa ni kujiamini pamoja na kujenga urafiki na watu wa kila aina. Nikutakie kila la kheri katika harakati zako za kugombania kiti cha ubunge. Mimi nakuombea dua ushinde ili vijana wengi wapate kujifunza kutoka kwako.
Nimemzungumzia Mlimwengu lakini ninatamani vijana wa kariba ya Mlimwengu wapate nafasi katika uchaguzi huu mkuu. Tuwapate vijana wengi ambao watakua chachu ya mabadiliko katika nchi hii. Rushwa ni adui wa haki watu wasichaguliwe kutokana na vipande vya kanga wanavyogawa bali wachaguliwe kwa uwezo wao na namna wanavyojipambanua katika kuleta maendeleo.
Niwatakie harakati njema vijana wote mnaogombania katika nafasi mbalimbali za kiungozi.