OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tuzo za Mo Simba zilianzishwa na Mwekezaji katika klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji kwa lengo la kutoa zawadi kwa wanafamilia wa Simba ambao wamesaidia klabu kupata mafanikio kwa msimu wa 2018/2019.
Tuzo hizi zitakuwa na vipengele 12 ambavyo vitahusisha wachezaji na mashabiki.
Kama shabiki wa Simba na soka kwa ujumla unaombwa kupiga kura kuchagua Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka na Shabiki Bora wa Mwaka.
Kama kawaida yetu Simba SC vijana wakishafanya kazi ngumu mwisho wa siku tunawapa tuzo. MwanaJF bila kujali unazi biga kura yako kuchagua mchezaji bora katika categories tofauti tofauti. Ingia katika link mosimbaawards.co.tz
Karibu kwa maoni pia